Regia alikuwa anaendeshaje gari? Wakati mguu wake wa kulia ndio wenye ulemavu?

Someni Lena Maria Klingvall. Na Yule mwanariadha wa south Africa ambaye ni mwenye matatizo ya miguu na anataka kushiriki michezo na watu ambao wana miguu.

Thread hii inakera sana ili inabidi tujifunze kuwa watu handicapped wana uwezo wa kufanya vitu vingi sana kuliko hata watu wa kawaida.

Tuamke!!!!!!!!

Swali ni la msingi sana...may be alikuwa anatumia vifaa maalum,na pengine ni matatizo ya vifaa hivyo je,tusipouliza si tatizo litatokea tena?
 
Nimeuliza swali la msingi sasa natukanwa mimi ni mjinga haya....nabaki na ujinga wangu lakini I promise....road accidents will continue to take its deadly toll if the authorities continue with business as usual
Mkuu kama kwa kuuliza hivyo ni ujinga basi wajinga tuko wengi, mimi nimejiuliza hilo swali toka jana nilivyopata habari kwamba alikuwa anaendesha mwenyewe, tunajua kifo hakizoeleki lakini kila siku tunalaumu madreva ajali zinapotokea nyingi ni ubovu wa barabara na uzembe wa madreva pia, hii ya Mheshimiwa lazima watu wajiulize ilikuwaje akaendesha yeye with physical disability tena umbali mrefu kiasi hicho, Mheshimiwa ametangulia mbele za haki na wahenga wanasema ajali haina kinga lakini kuchukua tahadhari kwa ajili ya usalama wa maisha yetu na wengine ni muhimu sana.
 
Jamani tusiwe na dabo standadi hapa, kama kuna hoja ya maana ijadiliwe.
Wamekufa wangapi na maswali kibao yakulizwa?
Kusema kweli we need to know this, je kuna utaratibu gani kwa watu wenye haloi kama yake kupata leseni na aina ya magari wanayotakiwa kuyatumia.
Itakuwa ni upuuzi kukwepa hoja ya msingi kwa kisingizio cha majonzi, na je kama majonzi hayo yameletwa na uzembe wa hoja inayoulizwa?
Kuna watu humu tayari wamesha fungua sredi eti kuna mkono wa serikali na wakaungwa mkono kwa nguvu zote, lakini inapotokea mtu akadadisi uhalisia anakua amekosea timing kipindi cha majonzi
Tujadili now, pamoja na kifo na majonzi tuliyo nayo lazima maisha mengine yaendelee, tujuwe tatizo right now kuokoa wengine na janga hili

Kwa mfano mimi leo ndo najua kuwa hilo eneo la ajali ni baya sana,ina maana bila huu mjadala nisingefahamu.So ndugu tuna majonzi lakini yale ya msingi tuyajadili tu ili tuendelee kujiokoa wenyewe maana tukiwategemea wenye mamlaka bado wako likizo ya x mas na mwaka mpya.
 
Mkuu unahita investigation gani iwapo taratibu zipo wazi kabisa mtu mwenye hali kama yake anatakiwa kuendesha gari lililokuwa modified kwa hali yake, Gari alilokuwa anaendesha halikufanyiwa chochote.

Hapo kwenye red kuna exemption kwa kesi hii ya kifo cha Mhe Regia au ni kwa wote...............what a double standard
Kwanini tunakimbia vivuli vyetu kwa kisingizio cha majonzi, Misiba imejadili mingapi humu kwa style hii? Tusiendeshwe na hisia binafsi zaidi kuliko uhalisia

Labda nikupe maelezo ya wenye mamlaka ya kutoa matamko kuhusu ajali hii


Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Saleh Mbaga alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ilitokana na hatua ya Mbunge huyo kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla likatokea roli la mafuta na
alipotaka kurejea upande wake gari hilo lilimshinda na kubiringita mara saba.

Alisema hata hivyo ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya Mbunge huyo kuwa na ulemavu wa mguu na hivyo kuwa na mguu mmoja tu wa kushoto ambao alisema inadhaniwa ulimpa tabu katika kufanya uamuzi baada ya kutokea kwa lori hilo la mafuta mbele
yake.

“Kama mnavyojua pedeli za gari zipo upande wa kulia lakini yeye alikuwa anatumia mguu wa kushoto kwa hiyo inawezekana kutokana na mshituko wa kutokea gari mbele, alibabaika katika kuutumia mguu huo wa kushoto kufanya uamuzi na hivyo kusababisha gari kumshinda na kupinduka,” alisema Mbaga.

Chanzo HabariLeo | Mbunge Chadema afa ajalini Ruvu

Pamoja na maelezo haya yaliyo wazi kabisa naamini bado hawatakuelewa. Ila ukisema ajali hiyo ina mkono wa CCM na serikali yake. Watakuunga mkono na miguu pia, aisee hawa ni watu wa ajabu kabisa. Suala hili liko wazi kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji magari.
 
Kwa mfano mimi leo ndo najua kuwa hilo eneo la ajali ni baya sana,ina maana bila huu mjadala nisingefahamu.So ndugu tuna majonzi lakini yale ya msingi tuyajadili tu ili tuendelee kujiokoa wenyewe maana tukiwategemea wenye mamlaka bado wako likizo ya x mas na mwaka mpya.

Eneo lile ki ukweli kufanya ovateki halifai hata kama kukiwa hakuna gari linalokuja mbele yako. Kwanza kuhama tu kutoka kushoto kwenda kuliwa ishu kutokana na kubonyea barabara na kuacha gema katikati. Aisee! Wahusika wanatakiwa kuweka alama katika eneo lile.
 
Ni hoja ya msingi sana, na huu ndiyo wakati wake. Kwa desturi, watu wakishatoka kuzika husahau/kupuuza kila kitu. Ajali zimeendelea kutokea kwa sababu tunakosa tafiti za kutosha na kuweka sheria ndogo ndogo. Mara nyingi ajali zinapotokea tunaishia kusema ni kazi ya Mungu, wakati mwingine tunamsingizia Mungu. Ajali za barabarani zaweza kusababishwa na Makosa ya Ki-binadamu (dereva au watembea kwa miguu), miundo mbinu (barabara, daraja n.k) na makosa/hitilafu ya gari (wakati mwingine ni makosa katika uundwaji wa gari lenyewe). Hivyo basi ajali inapotokea utafiti wa kina inabidi ufanyike ili ajali ya namna hiyo isiweze kutokea tena.

Kwa ajali hili; taarifa ya polisi inaonyesha kama tayari wameshahitimisha chanzo cha ajali, jambo ambalo siyo sahihi. Swali la msingi ni kwanini mheshimiwa alishindwa ku-control gari baada ya kutaka kurudi upande wake. Je ni kutokana na hitilafu ya barabara (kama wengine wanavyo-comment), hitilafu katika gari au makosa ya dereva? (kivipi).

Vilevile, dereva wa mheshimiwa anstahili kufunguliwa mashitaka kwa kusababisha kifo cha mheshimiwa. Hii itakuwa fundisho kwa madereva wengine kutokukubali kuwaachia mabosi wao kuendesha safari ndefu huku wakijua kuwa uwezo wao ni mdogo.
 
Ninamfahamu dereva mmoja mlemavu kijijini kwetu anaendesha Land Rover ya kubeba abiria ambayo ni Manual huku akiwa hana mkono wa kushoto na gari ni RHD.Nimemfahamu for more than 20 years na hana rekodi ya accident.Wacheni ku-generalize vitu hapa.
 
Mimi namjua mlemavu mwingine anatembelea magongo lakini ni dereva pia, self drive. Ni mfanyakazi pale Tanesco. Suala la ulemavu na ajali nadhani halina mshiko kwa sasa hasa kipindi chenyewe cha majonzi. Pia nijuavyo wakati anapata leseni ya udereva alikuwa ni mlemavu tayari....sasa unataka kusema kuwa waliompa hiyo leseni hawakujua ni mlemavu na kujua jinsi gani anaweza kuendesha gari? Pia tujiulize,,,ni jalingapi zimetokea zikihusisha walemavu wa miguu ukilinganisha na wale ambao hawana ulemavu wowowte?
Umepitwa na wakti ww, nenda pale nssf akiba ulizia mlemavu anaendesha gari,
Tena gari yenywe mbenz!!!
Utaonyeshwa kijana niliyesoma nae, tukiwa shule alikuwa akitamba kwa magongo hadi leo hii.

Cha ajabu nini hapo?
 
Kwa wale ambao tumetumia barabara hiyo tutakubaliana kuwa barabara haifai. Ni ya rami kweli, LAKINI IMEUMUKA KAMA MKATA! Tena maeneo just before daraja kama unatokea Mlandizi au eneo lile karibu na daraja la reli inapopita juu, kawaida kuhama kutoka eneo moja la barabara kwenda jingine inapaswa kujihami kwanza maana ina mgongo ile barabara utadhani ni mpaka unaotenganisha nchi moja na nyingine.

Kwa ajali hili; taarifa ya polisi inaonyesha kama tayari wameshahitimisha chanzo cha ajali, jambo ambalo siyo sahihi. Swali la msingi ni kwanini mheshimiwa alishindwa ku-control gari baada ya kutaka kurudi upande wake. Je ni kutokana na hitilafu ya barabara (kama wengine wanavyo-comment), hitilafu katika gari au makosa ya dereva? (kivipi).
 
Niswali la msingi na wala siladhiaka kama Brugita ulivyodhani yakupasa kuwa nasubira japo yawezekana unahusika mojakwamoja na msiba huo nakama alikuwa anaendesha gari ambayo haikuwa nanyenzo za walemavu basi serikali has Bunge la JMT wanatakiwa kushitakiwa!
 
Uungwana ni pamoja na kuukubali ukweli japo waweza kuwa mchungu kwa upande mmoja au mwingine. Nikiri kwamba tuliowengi tumeguswa na tumeshtushwa na kifo cha mpendwa wetu Mhe. Regia na hasa mazingira ya kifo chake.
Lakini katika kipindi hiki ambapo serikali, asasi, wanaharakati na makundi kadhaa ya kijamii wakiwa kwenye kampeni kubwa ya kupunguza kama si kumaliza kabisa ajali za barabarani hatuna budi kujiuliza maswali kadhaa juu ya mazingira ya ajali ambayo imepelekea umauti kwa mpendwa wetu dada Regia.
Bila shaka hilo swali hapo juu ni la msingi sana, pamoja na mambo mengine majibu mazuri yatakayotokana na tafiti juu ya chanzo cha ajali hiyo, yatatusaidia kupambana na kuepuka ajali za barabarani. Si swala la kupuuza ni busara tuukaubali ukweli ili tuweze kuepuka mazingira na tabia hatarishi juu ya ajali za barabarani kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye.

R.I.P Hon Regia Mtema. May The Almighty God rest your Soul in Eternal Peace. Amen
 
Ingawa ajari haina kinga kwa maoni yangu mtu mwenye hadhi ya ubunge, uwaziri, ujaji, kiongozi wa ngazi ya juu wa chama etc haileti picha nzuri kuendesha mwenyewe, hata kama hauko kikazi. Sina maana kwamba ukiwa na dreva hautapata ajari lakini inaleta mantiki sana kwa hadhi yako kuwa na dreva.
 
Niswali la msingi na wala siladhiaka kama Brugita ulivyodhani yakupasa kuwa nasubira japo yawezekana unahusika mojakwamoja na msiba huo nakama alikuwa anaendesha gari ambayo haikuwa nanyenzo za walemavu basi serikali has Bunge la JMT wanatakiwa kushitakiwa!

kweli?? Are you serious?
 
mdau ameuliza swali la msingi,hawa makamanda lazima wawe makini,hasa ktk ulimwengu wa siasa uchwara.niliwahi kumwona mhe halima mdee anaendeshe mwenyewe toka dom or dar mpaka mwanza ni hatari,wanatakiwa kuwa makini ata kama kifo ni mpango wa mungu
 
Kuna issue pia ya kuwa na abiria saba lkn watu hawaliongelei, uzito pia unawezekana ulichangia yy kushindwa kulitawala gari
Kwa ajali hili; taarifa ya polisi inaonyesha kama tayari wameshahitimisha chanzo cha ajali, jambo ambalo siyo sahihi. Swali la msingi ni kwanini mheshimiwa alishindwa ku-control gari baada ya kutaka kurudi upande wake. Je ni kutokana na hitilafu ya barabara (kama wengine wanavyo-comment), hitilafu katika gari au makosa ya dereva? (kivipi).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom