Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimedai kuwa Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amekuwa akiandaa njama za kudhoofisha maandamano ya chama hicho yaliyopangwa kufanyika jijini Mbeya Jumanne, Februari 20.2024
Akizungumza na wanahabari kwenye Ofisi za CHADEMA Kanda ya Nyassa zilizopo Kadege Mbeya leo, Jumapili Februari 18.2024 Mkurugenzi wa Itifaki, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya nje wa chama hicho Taifa John Mrema ameeleza kuwa Homera kwa kushirikiana na baadhi ya wazee wa mkoa huo wamekusudia kuitisha kikao cha wanahabari ili wautangazie umma kuwa Jumanne, Februari 20.2024 wanakusudia kufanya ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya kimkakati jambo ambalo CHADEMA imetafsiri kuwa ni njama iliyoandaliwa ili wananchi wasitoke kwenye maeneo yao kushiriki maandamano
Mrema amesisitiza kuwa jambo hilo halijawastua kwa kuwa njama kama hiyo ilijitokeza walipoandaa maandamano ya kwanza Dar es Salaam ambapo Mkuu wa mkoa huo Albert Chalamila alitangaza siku iliyopangwa kufanyika maandamano ya CHADEMA kuwa siku ya usafi lakini mpango huo haukufanikiwa
Ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani kwa Machifu na wazee wa Mbeya kwa ushiriki wao katika kuhakikisha maandamano hayo yanafanikiwa sambamba na kufafanua kuwa chama hicho kinaratibu maandamano hayo kwa ajili ya umma.
Credit - JamboTv