Sn2139
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 834
- 250
Magufuri haiwezi nafasi ya maamzi kama ya rais yeye ni mtendaji , mtu wa kupewa kazi na kuifanya kwa uaminifu na siyo siasa za maji taka za urais
You are very wrong! Najiuliza kuwa unapokuwa unatoa jibu kama hilo unatumia vigezo gani wewe? Unataka kumaanisha Kikwete anafaa kuliko Migufuri? Usitake kutoa judgement ya mtu kwasababu za kutoka mfukoni kwako. Tukiruhusu judgements hizo, mimi nitazitumia kukuhukumu wewe pia kwa kutumia jina lako la Oba, kuwa wewe una-push ganja ... ha ha ha ha!
Tuache utani, nafasi ya rais sasa hivi ni nyeti kwasababu kuu zifuatazo:
(1) Nyerere aliongoza nchi hii vizuri sana na kuweka precedence ambayo waliomfuata wameshindwa kuifikia
(2) Watu wamepoteza maana ya rais kama kiongozi wa watu, sasa wanaanza kuona kama ni zamu ya ama kabila, au dini, au ukanda kutumbua keki ya taifa
(3) Mali asili imeporwa na viongozi baada ya Nyerere, Ardhi imeuzwa na haohao, Viwanja vinanunuliwa na wageni na wananchi wazawa wanaanza kuwa marginalised
(4) Influx ya foreigners ni kubwa kuliko wakati wowote, na wanakuja na capital power. Tuna wachina, wasomali, waarabu, wahindi, wakenya, wanigeria, pakstan, nk.. wanakuja kuishi, kunua ardhi, kufanya biashara...wana uwezo mkubwa wa (1) mawazo ya biashara (2) capital (3) information (4) Exposure, (5) business networks nk
Wa-Tz wamekuwa timed wakingali bado wanaamini kuwa rais anawalinda, analinda nchi na mali zao, anawapenda na kuwafundisha na kuwatayarisha kujilinda. Wakati wakiwa katika hali kama hiyo, kumbe wanayemwamini alishabadilika kutoka binadamu hadi nunda mla watu. Very sad
Sasa, kila upande tuangalie, yaani Ruling part na Opposition parties:
CCM | CDM | |
1 | Kina performance record mbili nzuri (Nyerere) na mbaya (Non-Nyerere) | Bado hakijashika dola |
2 | Sera zao ni nzuri | Sera zao ni nzuri |
3 | Record yake ni ya mtu mmoja tu (Nyerere) | Record yao ni ya mtu mmoja tu (Dr W. Slaa) |
4 | Kina watu wazuri na wabaya | kina watu wazuri na wabaya |
5 | Kujisafisha ni vigumu, labda yafanyike mapinduzi ya mtutu kuua mafisadi wote | Hakijachafuka, lakini kina potential ya kuchafuka pia |
6 | Kina watu wengi wenye uwezo wa kuongoza kama vile: Magufuri, Mwandosya, Lowasa, Mwakyembe, Membe, Mwinyi, na wengine... | Kina watu wenye uwezo wa kuongoza kama: Dr W. Slaa, Mh Tundu, Mh Zito, Mh Mbowe. |
Pia kuna vyama vingine kama CUF kule kuna Prof Haruna Ibrahim Lipumba, ana uwezo, kuna NCCR na TLP. Kwa mawazo yangu mimi ni kuwa, CCM iondoke ikae pembeni mwaka 2015 ili kuimarisha democrasy, kisha miaka ijayo vyama vya upinzani vibaki 2 au 3 na kuimarisha mfumo huo. Lakini ukweli hakuna chama hata kimoja ambacho ni kizuri 100% au kina watu wazuri 100% tusidanganyike, hakuna, na siyo Tz peke yake, bali hata UK, USA na Israel. Kote huko kuna binadamu tu kama mimi na wewe. Samahani sina mpangilio lakini naomba upate hoja yangu katika mvurugano wa mawazo ktk hoja yangu.