KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,591
- 4,604
Kwa kuwa kuna pande mbili zinazotofautiana kwenye uwekezaji wa bandari na pande hizi zimeonesha wazi ni pande za kisiasa. Upande wa wanaopinga uwekezaji wakiongozwa na CHADEMA na upande unaokubaliana na uwekezaji wakiongozwa na CCM. Pande zote mbili zinapenda kusikia lolote kutoka kwako hasa upande unaoongozwa na CHADEMA kwa sababu kwa vyovyote vile lolote utakalosema litakuwa ni upande wa CCM ila inaweza kufanyika vinginevyo kulingana na busara zako zitakavyokuongoza.
Ni ukweli usiopingika suala hili lina matokeo chanya na hasi kwenye siasa hususani za CCM. Matokeo chanya ni pale ambapo uwekezaji utaanza kuonyesha faida zinazosemwa Sasa na matokeo hasi ni pale ambapo wanaopinga Sasa wakawa wapo sahihi kwenye kupinga kwao na faida zisionekane. Matokeo hasi yatakitesa Chama Cha Mapinduzi kwa Muda mrefu hususani katika masuala yanayohusu uwekezaji.
Licha ya kwamba yanayopingwa yanaweza kuwa kweli Kwa sababu hakuna ajuaye ya kesho lakini mtazamo na maoni yangu kwenye suala hili utabaki uleule CCM ISIRUDI NYUMA KWENYE UWEKEZAJI WA BANDARI KWA SABABU KURUDI NYUMA SASA HAKUTAKUWA NA NJIA YA MWENDA MBELE BAADAYE.
Ni wakati wa kuendelea kuziba masikio Mhe.Rais, yanayoongelewa kuhusu DP WORLD jifanye kama hujawahi kuyasikia wala huyasikii maana Kwa Sasa upo kwenye jaribu kubwa:
Kwanza, wanaopinga wanataka ufanye uamuzi wa kusitisha makubaliano hayo ili wapate sababu ya kuongea Zaidi. Ukisitisha Sasa itaonekana ni kweli kulikuwa na nia ovu kwenye makubaliano, taswira ya Chama itakuwa mbaya na itahitajika nguvu kubwa kuisafisha.
Pili, ukisitisha Sasa CCM itabidi Ile matapishi yake. Nguvu iliyotumika kuelimisha umma juu ya umuhimu wa makubaliano na uwekezaji huu itakuwa kazi Bure. Hakuna jambo gumu duniani kama kula matapishi maana itabidi watu wasio na kinyaa wafanye hivyo.
Baada ya kutambua haya napenda kuchukua nafasi hii kukuomba Mhe.Rais:
Kwanza, nakuomba uwe na Imani juu ya dhamira na nia yako Kwa Taifa. Kutaka kuwepo Kwa uwekezaji huu ni dhamira njema uliyonayo ya kuliletea Taifa maendeleo hivyo lolote litakalotokea tutailinda na kuitetea dhamira yako na mapenzi makubwa uliyonayo Kwa Taifa letu.
Pili, nakuomba usiongee lolote juu ya uwekezaji na DP WORLD Kwa Sasa. Wasaidizi wako ndani ya CCM na Serikali watakusaidaia kulisema. Wanataka uongee kitu ili waendelee kusema, mlengwa mkuu mikutano wanayofanya ni wewe, hivyo ninakuomba usiongee lolote.
Tatu, ninakuomba utumie busara zako kupanga safu nzuri ya kuhakikisha uwekezaji unakuwa ni wenye tija na matokeo makubwa ya uwekezaji yanaonekana haraka.
Kwa kufanya hivi Mhe.Rais utakuwa si tu umewajibu wanaopinga uwekezaji bali itakuwa ni pigo Kwa wote wenye lengo la kufanya au kuendeleza kufanya siasa kwenye maendeleo ya nchi.