Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,333
- 24,218
Rais Samia Suluhu Hassan
Nikiwa mmoja wa members wa JF nilyepinga sana mkataba wa awali kati ya nchi yetu na DP World, nachukua nafasi hii kumpongeza Mama Samia.
Pongezi zangu zinazingatia vipengele kadhaa:
- Watanzania wengi tunapenda uwekezaji na nchi iweze kuvutia mitaji toka kote duniani
- Mchakato wa kwanza jinsi ya kumpata muwekezaji DP World uligubikwa na usiri
- Mchakato huo wa awali haukuzingatia maslahi ya wazi kabisa kitaifa
- Taratibu za manunuzi ya umma kwa kuzingatia uhusika na uhalali vyombo husika kwa mkataba na DPW haukuwepo wazi.
Mama Samia ameonyesha usikivu na uelewa kwa athari zilizoanza kujitokeza.
Kwamba mama alikaa kimya kumbe chini ya carpet anayafanyia kazi madudu yote yaliyo jitokeza.
Ingawaje kuna wakati mama Samia alionyesha kukerwa na lawama nyingi, lakini cha msingi na cha kuigwa na viongozi wajao ni kushughulikia matatizo kwa mafanikio na maslahi ya nchi.
Sasa kina Mwabukusi na Slaa inabidi watafute soo jingine, waliyoonyesha yameshughulikiwa.
Kitu cha msingi sasa hivi ni kujitathmini: how did Ikulu get it so wrong mwanzoni?
Waliotoa na kuratibu ushauri hasi watawajibika vipi?
Otherwise kwa sasa:
Hongera mama Samia maana hongera hizo unastahili, kwa kondoa wingu lililokuwa limetanda.
Siyo siri Rais Samia alianza vizuri, sasa analikoroga
Kaa kimya kama huna hoja za kujadili, nchi hii ni yetu sote! Haya tumia hiyo haki yako vibaya. Muda sio mrefu utaelewa wazoefu wa ku deal na polisi, kama viongozi wa vyama vya siasa wanaojua mipaka yao kwanini hizo lugha za mapinduzi wanawaachia wenyewe na kwanini Lissu hataki hayo majukwaa...
www.jamiiforums.com
CCM, kwa mtaji wa ukakasi wa suala la Bandari, kaeni mguu sawa kung'olewa!
Suala la Bandari linajadiliwa kwa marefu na mapana kila kona ya nchi. Maandamano ya vyama vya upinzani yameshaanza mikoani kupinga suala zima la ubinafsishaji/uuzwaji/ukodishaji, au hata kuigawa bure Bandari yetu na nyingine Tanzania. Tukubali tusikubali, serikali ya CCM imeingia mkenge mkubwa...
www.jamiiforums.com
CCM sasa tunaelewana, Chongolo amekubali mkataba DP World ulikuwa na makosa! Sasa tusonge mbele!
Baada ya kuonywa mara nyingi na wadau, sasa CCM imeanza kuelewa. Na mimi kada nilionya huko nyuma, CCM ikiendelea kushupaza shingo, itavuna mabua 2025. https://www.jamiiforums.com/threads/ccm-kwa-mtaji-wa-ukakasi-wa-suala-la-bandari-kaeni-mguu-sawa-kungolewa.2113301/page-2#post-46992236 Suala...
www.jamiiforums.com