Kwanza niseme mimi siyo wa kwanza kuwalalamikia hawa Bodi ya Mkopo Elimu ya Juu (HESLB). Ukiingia ATM uka-command kutoa pesa, ukapewa risti na pesa isitoke. Ukiingia ndani au ukapiga simu pesa yako inarudishwa muda huo huo.
Lakini hawa HESLB wanakata wanufaika wa mikopo Elimu ya juu kwa miaka kadhaa. Mara nyingi marejesho yakikamilika wanatabia ya kuendelea kukata mwezi mmoja, miwli, mitatu hadi minne kutegemea na mkatwaji atakavyo wahi kufuatilia kwenda kulalamika HESLB.
Ukirnda kulalamika wanakupa fomu ya kujaza Ili kusitisha makato na barua ya kumpelekea mwajiri asitishe na kukueleza kiasi unachotakiwa kurejeshewa baada ya kukata zaidi ya kiasi wanachokudai.
Badala ya kukuandikia hundi upewe pesa yako papo hapo, wanakwambia uende ukajaze taarifa zako kwenye mfumo wa ki electronic ( loan refund) na unatakiwa usubiri siku 90.
Zikiisha ukiwafuata utaambiwa endelea kusubiri, ukimaliza miezi kadhaa tena ukienda wanakwambia uendelee kusubiri huku ukipitia kuona Akaunti yako ya loan refund.
Dr. Samia kama unasoma hili embu tueleze tatizo ni nini wakati pesa wanazo kwani Kila mwezi wanakata wanufaika.
Tuondolee huu utaratibu na ikikupendeza zaidi ondoa yule mtendaji Mkuu wa HESLB au Prof. Mkenda kabisa. Hatutachoka kuwalalamikia hawa jamaa mpaka tutakapolipwa pesa yetu na kubadilisha huu utaratibu wa kuingia kwenye mfumo wa ku-claim badala ya kuandikiwa hundi.