Rais Samia tunaomba uingilie kati suala la kulipwa posho intern doctors waliopo hospitali za Dar

Bhahebhu

Member
Dec 3, 2021
33
33
Mhe. Rais wa JMT, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, leo ni takribani unaelekea mwezi wa pili kuisha bila kulipwa posho yao ya mwezi kama mikataba yao inavyoonesha hawa madaktari watarajali(intern drs), hasa katika hospitali za Dar es Salaam.

Mfano; Temeke, Mwananyamala nk. Ikumbukwe kuwa hawa ndio wanafanya kazi nyingi sana wawapo hospitalini na pia wanafanya masaa mengi zaidi kuliko mtumishi aliyeajiriwa, hivyo kuchelewesha malipo yao bila sababu za msingi ni kutowatendea haki kabisa, intern dr anaitwa PUNDA wa hospitali hilo ndio jina maarufu kwa hawa madaktari watarajali.

Sababu zimekuwa ni nyingi za kwanini posho imechelewa mara mfumo sjui mpya, mara fedha imeshaingia mahospitalini ila mfumo mpya unasumbua, sababu hizi hazijitoshelezi kwani hakuna kiongozi yeyote si wakurugenzi, si MCT, waliotoa taarifa rasmi kuhusu hilo jambo, hivyo kuleta sintofahamu kubwa miongoni wa madaktari hawa.

Hivyo basi kwa unyenyekevu mkubwa Mhe Rais wa JMT Mama yetu Samia tunakuomba sana uingilie kati suala hili ili mamia ya vijana hawa waweze kulipwa posho zao za mwezi wa kumi, pia kupiga marufuku ucheleweshaji wa malipo kwa miezi inayoendelea.🙏🙏🙏
 
Mhe.Rais wa JMT, kama kichwa cha habari kinavyojieleza, leo ni takribani unaelekea mwezi wa pili kuisha bila kulipwa posho yao ya mwezi kama mikataba yao inavyoonesha hawa madaktari watarajali(intern drs), hasa katika hospitali za dar es salaam, mfano; temeke,mwananyamala nk.Ikumbukwe kuwa hawa ndio wanafanya kazi nyingi sana wawapo hospitalini na pia wanafanya masaa mengi zaidi kuliko mtumishi aliyeajiriwa,hivyo kuchelewesha malipo yao bila sababu za msingi ni kutowatendea haki kabisa, intern dr anaitwa PUNDA wa hospitali hilo ndio jina maarufu kwa hawa madakyari watarajali. Sababu zimekuwa ni nyingi za kwanini posho imechelewa mara mfumo sjui mpya, mara fedha imeshaingia mahospitalini ila mfumo mpya unasumbua,sababu hizi hazijitosherezi kwani hakuna kiongozi yeyote si wakurugenzi,si MCT, waliotoa taarifa rasmi kuhusu hilo jambo,hivyo kuleta sintofahamu kubwa miongoni wa madaktari hawa. Hivyo basi kwa unyenyekevu mkubwa Mhe Rais wa JMT Mama yetu Samia tunakuomba sana uingilie kati suala hili ili mamia ya vijana hawa waweze kulipwa posho zao za mwezi wa kumi, pia kupiga marufuku ucheleweshaji wa malipo kwa miezi inayoendelea.🙏🙏🙏
No
 
Hivi nyie wakubwa, kwani Hawa vijana wanalipwa sh ngapi na ninyi mnaiba sh ngapi?
Acheni hizo.
Hapa Dar, kila mkuu wa hosp ya serikali ana hosp yake binafsi (Ila Janabi Sina uhakika, na Nina uhakika Muhimbili ya upanga ma intern wanalipwa stahiki zao)
Mnadhulumu hao hao wanaofanya kazi zenu nyie mkiwa bar?
 
Back
Top Bottom