Waziri Mchengerwa aagiza Fedha za Kujikimu za Ajira Mpya zilipwe kabla 30 Oktoba, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed O. Mchengerwa (Mb) amewaelekeza Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanalipa fedha za kujikimu kwa Watumishi wa ajira mpya za Ualimu na Afya walioripoti kwenye vituo vya kazi kuanzia mwezi Julai, 2023.

Amesema Serikali tayari imeshapeleka fedha kwenye kila Halmashauri kwa ajili ya kulipa stahiki za watumishi hao lakini mpaka leo kuna watumishi wa ajira mpya ambao hawajalipwa fedha za kujikimu, hii sio sawa watumishi wote walipwe fedha za zao kabla ya Oktoba 30, 2023.

"Fedha za kujikimu ni haki ya kila mwajiriwa mpya sasa, kwanini usilipe na fedha unayo kama kuna changamoto yeyote iwasilishwe ila sio kukaa na fedha na kuacha hawa watumishi wakihangaika, walipwe mara moja." amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

Kwa mwaka wa fedha 2022/23, Serikali iliajiri watumishi wapya wa kada ya Ualimu na Afya ambapo kwa Kada ya Ualimu ni watumishi 13,130 na Afya ni watumishi 7,192 na wote wamekwisharipoti kwenye vituo vyao vya kazi.

Tamisemi.jpeg

Pia Soma
=> Malalamiko kuhusu pesa za kujikimu kwa waajiriwa wapya Halmashauri ya wilaya ileje

=> Madaktari Watarajali Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro tunadhalilika mitaani kwa kucheleweshewa posho za kujikimu
 
Kama Serikali imepeleka hela muda mrefu hiyo October 30 ni ya nini? Kulipa hela ambazo unadai zipo na tena zilishatengwa kwa idadi yake siku 27 unazotoa ni kwa kitu gani kinachozuia ndani ya masaa 24 hela iliyopo isiwakute wahusika?
Na kama kuna watu wameamua kutolipa ni hatua gani kama Wazir amechukua dhidi ya uonevu huu?
Mchengerwa na wenzake ni wanafiki wakubwa hawa wanastahili kulaaniwa kwa dhihaka hizi, huwezi kusimama kama Wazir eti unajifanya kuwa na huruma huko unatoa tena siku 27 mbele.
CCM wamechezea hela za umma kujilipa na kunufaishana wakiwasahau watumishi wanaowasadia kuiba kura.
Na nyinyi watumishi ifike hatua mkubali kutotumika kama daraja la kuwaweka mafisadi mamlakani, inukeni nyinyi watu kuondoa uovu.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed O. Mchengerwa (Mb) amewaelekeza Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanalipa fedha za kujikimu kwa Watumishi wa ajira mpya za Ualimu na Afya walioripoti kwenye vituo vya kazi kuanzia mwezi Julai, 2023.

Amesema Serikali tayari imeshapeleka fedha kwenye kila Halmashauri kwa ajili ya kulipa stahiki za watumishi hao lakini mpaka leo kuna watumishi wa ajira mpya ambao hawajalipwa fedha za kujikimu, hii sio sawa watumishi wote walipwe fedha za zao kabla ya Oktoba 30, 2023.

"Fedha za kujikimu ni haki ya kila mwajiriwa mpya sasa, kwanini usilipe na fedha unayo kama kuna changamoto yeyote iwasilishwe ila sio kukaa na fedha na kuacha hawa watumishi wakihangaika, walipwe mara moja." amesisitiza Mhe. Mchengerwa.

Kwa mwaka wa fedha 2022/23, Serikali iliajiri watumishi wapya wa kada ya Ualimu na Afya ambapo kwa Kada ya Ualimu ni watumishi 13,130 na Afya ni watumishi 7,192 na wote wamekwisharipoti kwenye vituo vyao vya kazi.

Pia Soma
= Malalamiko kuhusu pesa za kujikimu kwa waajiriwa wapya Halmashauri ya wilaya ileje

= Madaktari Watarajali Hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro tunadhalilika mitaani kwa kucheleweshewa posho za kujikimu
Haya ndiyo mambo wananchi wanayahitaji

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kama Serikali imepeleka hela muda mrefu hiyo October 30 ni ya nini? Kulipa hela ambazo unadai zipo na tena zilishatengwa kwa idadi yake siku 27 unazotoa ni kwa kitu gani kinachozuia ndani ya masaa 24 hela iliyopo isiwakute wahusika?
Na kama kuna watu wameamua kutolipa ni hatua gani kama Wazir amechukua dhidi ya uonevu huu?
Mchengerwa na wenzake ni wanafiki wakubwa hawa wanastahili kulaaniwa kwa dhihaka hizi, huwezi kusimama kama Wazir eti unajifanya kuwa na huruma huko unatoa tena siku 27 mbele.
CCM wamechezea hela za umma kujilipa na kunufaishana wakiwasahau watumishi wanaowasadia kuiba kura.
Na nyinyi watumishi ifike hatua mkubali kutotumika kama daraja la kuwaweka mafisadi mamlakani, inukeni nyinyi watu kuondoa uovu.
Yaani yeye analalamikia wakurugenzi wake, sisi tunamshngaa Kwa kutoa siku 27 kulipa mtu anayedai huku mdaiwa akiwa na fedha mkononi ya kulipa!!

This is very ridiculous kiasi cha mtu kufikiri kuwa labda na yeye anapiga siasa zilezile za udanganyifu wa ki - CCM..!
 
Hili jambo nilisha lizungumzia apa toka mwez wa saba leo limeibuka ngoja tuone lakini kiukweli kuna maovu meng sana kwenye ma halmashauri
 
Yaani yeye analalamikia wakurugenzi wake, sisi tunamshngaa Kwa kutoa siku 27 kulipa mtu anayedai huku mdaiwa akiwa na fedha mkononi ya kulipa!!

This is very ridiculous kiasi cha mtu kufikiri kuwa labda na yeye anapiga siasa zilezile za udanganyifu wa ki - CCM..!
Hawa ni wanafiki wakubwa, jioni wanakutana kupongezana kwa kuzima jambo lao kinafiki, kwa wasiwajua ndio hao wanasema eti huyu ni mtetezi.
Hawa watu wanajua hao walioenda kwenye hizo ajira sio watoto wao ila ni makapuku fulani hayawezi kugomea hizo kazi kwani hawana pa kwenda, kwahiyo unawapiga fix wanakenua siku imeisha na umejizolea sifa.
Kwa akili ya kawaida tu, tangu July hiyo Wizara haikuwa na viongozi? Je leo nani kampa taarifa kama sio unafiki tu.
 
Halmashauri ya ILEJE,SONGWE lipeni fedha za kujikimu....kila siku majibu yamekuwa Yale Yale, alpokuja ummy Mwalimu majuzi alitoa maelekezo fedha hizo zilipwe,mkurugenzi,DMO na katibu wake wakatafuta kisingizio kuwa BOT mtandao wa kuruhusu malipo unasumbua.
Yapata mwezi Sasa bado eti mtandao wa BOT unasumbua. Halmashauri zingine mkoani songwe wamepewa fedha za kujikimu kwa ILEJE ukiuliza majibu yanakuwa ya vitisho na kejeli.
 
Au wali stake high kanj akapita nazo so wanaskilizia next games.
 
Back
Top Bottom