Rais Samia hawezi kushinda urais 2025 kirahisi kama Wakurugenzi na Tume ya Uchaguzi watadhibitiwa

ndugu tupo mitaani kwani nazungumza kutoka wapi? yaani kila mtu yupo busy na mambo yake ya kutafuta hela wewe unaonekana huna cha kufanya na huna chakufanya kwasababu ni mvivu unasubiri uletewe hakuna hela rahisi ndugu hata ukiangalia utawala wote uliopita hakuna aiyekuwa anagawa hela
Kwamba unakataa mtaani hali sio ngumu?
 
Wananchi wa kawaida labda umaanishe hawa wanaoshinda JF wakiandika maoni yao, lakini hao wa huko chini watampigia kura tena nyingi sana.

Bajeti ya wizara ya kilimo imeongezwa zaidi ya asilimia sabini, kilimo kimeguswa moja kwa moja kwa maana ya pembejeo na ufufuaji wa mazao yaliyokuwa yakipuuzwa miaka ya nyuma. Hao wote ni wapiga kura na ni wengi sana kulinganisha na wapambe wanaoshinda humu jukwaani.

Kwa bahati mbaya sioni wapiga kura kujitokeza kwa wingi tena kwani box la kura limepuuzwa rasmi. Mnaweza kuzungumzia kushinda, ila sio kwa idadi ya wapiga kura kama wapiga kura. Nina hakika wapiga kura watakuwa wachache kuliko kipindi chochote ndani ya nchi hii. Wengi wa watakaojitokeza kupiga kura ni wenye uelewa mdogo.
 
Kwamba wanufaika Hawa wote wanamchukia na hawatampigia kura sio? Kuwa serious basi 👇

Screenshot_20220520-100034.png

Screenshot_20220520-094607.png

Screenshot_20220520-094242.png

Screenshot_20220520-083255.png

Screenshot_20220520-083032.png

Screenshot_20220520-082848.png

Screenshot_20220520-082359.png

Screenshot_20220520-081529.png
 
Kwa bahati mbaya sioni wapiga kura kujitokeza kwa wingi tena kwani box la kura limepuuzwa rasmi. Mnaweza kuzungumzia kushinda, ila sio kwa idadi ya wapiga kura kama wapiga kura. Nina hakika wapiga kura watakuwa wachache kuliko kipindi chochote ndani ya nchi hii. Wengi wa watakaojitokeza kupiga kura ni wenye uelewa mdogo.
Wenye uelewa mdogo ni wachache, wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaofaidika moja kwa moja na mapinduzi ya kilimo yanakwenda kufanyika nchini.

Wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaojishughulisha na maisha halisi huko mtaani. Mimi na wewe wa mitandaoni huwa hatuoni maana ya kupiga kura, tunaishia kulalamika huku tukizeeka na malalamiko yetu.
 
Ngoja chodomo waendeleee kujiaminisha kwenye mitandao 😄😄

Sio tuu Kilimo bali wamama kwa maelfu watampigia kura kwa sababu anawapa ile mikopo isiyo na riba kupita Halmashauri na Banks,amewatua ndoo kichwani na kuwajengea vituo vya afya .
 
Kina Tindo wanakariri maisha hawajui kuwa kuna mabadiliko makubwa ya kimtazamo yanayoendelea ndani ya CCM hivyo nchi nzima.

Huyu ni rais mwanamama, anayo huruma ya asili, hana kiburi wala hana ule ujinga wa kutaka kuwakomoa baadhi ya watu wanaokupigia kura.
 
Mama akimaliza miradi ya Mwendazake atashinda kirahisi maana maisha yatakuwa mazuri ila miradi ikimshinda wapinzani ndani na nje ya chama chake watatumia kigezo cha kudai "tumechoka kuongozwa na mwanamke"

Hii ni nchi ya mfumo dume na wanaume wengi wametii katiba tu ila mioyo yao inaungua na kwasasa maji yametuama walafi wa urais wanahesabu miaka tu amalize waanze kumnanga na kumparura!!

Mama needs to go extra miles!!
 
Sio kila mwaka ni 2020. CCM ikidhibitiwa wizi wake inashindwa.

Wizi unafanywa kwa kutumia vyombo vya dola na usalama, utadhibiti vipi? Tungekuwa na vyombo vya dola vinavyofuata sheria hapo sawa, lakini hivi vyombo vya dola vinavyomtii rais labda kutokee machafuko.
 
Kina Tindo wanakariri maisha hawajui kuwa kuna mabadiliko makubwa ya kimtazamo yanayoendelea ndani ya CCM hivyo nchi nzima.

Huyu ni rais mwanamama, anayo huruma ya asili, hana kiburi wala hana ule ujinga wa kutaka kuwakomoa baadhi ya watu wanaokupigia kura.

Hayo mabadiliko ya kimtazamo ni kwakuwa vyama vya upinzani hasa CDM hawafanyi ushawishi wake kwa umma. Lakini sasa hivi CDM wakianza uhamasishaji na watu wakajaa, utaona yale yale. Inshort CCM sio chama cha kizazi hiki, na kwa bahati mbaya hakikubaliani na ukweli huo, ndio maana kinatumia vyombo vya dola kukaa madarakani kwa shuruti.
 
Pamoja na kuwa mpaka sasa hakuna mpinzani makini na uhakika walio makini wamejificha na wanasubiri 2025 ikaribie na watajitokeza.

Lakini wakurugenzi wadhibitiwe kuchakachua matokeo na tum ya uchaguzi idhibitiwe kuchakachua matokeo. Rais Samia hatashinda.

CCM imegawanyika na wanaCCM wengu ndio watamnyima kura. Changanya na raia wa kawaida ambao tangu arithi urais kwao ni tabu tu maana hata wauza karanga wanamchukia kwa magumu wanayopata.

Sasa hapo ndio ashinde Urais?
Hao raia wa kawaida/wauza karanga wana uwakilishi wa nguvu ndani ya kamati kuu ya CCM? Huko ndiko Rais wa Tanzania anateuliwa na kusimikwa. Kule kwa Mahera ni bra bra tu na ulaji vinafanyika.
 
Wenye uelewa mdogo ni wachache, wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaofaidika moja kwa moja na mapinduzi ya kilimo yanakwenda kufanyika nchini.

Wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaojishughulisha na maisha halisi huko mtaani. Mimi na wewe wa mitandaoni huwa hatuoni maana ya kupiga kura, tunaishia kulalamika huku tukizeeka na malalamiko yetu.

Sibahatishi ninachoongea, nimeona ni kwa kiwango gani watu hawajitokezi kupiga kura, na ule uhayawani uliofanyika 2019 uchaguzi SM, na 2020 uchaguzi mkuu ule ndio rasmi ulikata rasmi hamu ya wananchi kupiga kura. Chungu za chaguzi zote za marudio zilivyokuwa na wapiga kura wachache, na chaguzi nyingine za marudio zitakavyokuwa na wapiga kura wachache.

Kwa huku bara wangalau CDM wakiamua kushiriki uchaguzi unaweza kuongeza idadi ya wapiga kura, lakini wasiposhiriki ndio utaona idadi ya wapiga kura halisi ambao ndio huwa wanaipa kura CCM, na hawa kimsingi huwa ni wachache kisha wanajazia na za wizi.
 
Uwadhibiti WAKURUGENZI walioteuliwa na Mama ili wamdhibiti Mama Mwenyewe??? 🤣 🤣

Ndo maana tunataka SERIKALI ya Majimbo yaani hawa Wakurugenzi wawe wanaajiriwa na Jimbo husika yaani ukiharibu Serikali ya Jimbo ndo ikushtaki na hakuna tena ishu ya UHAMISHO kama hii ya CCM kufunikiana madhambi.
 
Sibahatishi ninachoongea, nimeona ni kwa kiwango gani watu hawajitokezi kupiga kura, na ule uhayawani uliofanyika 2019 uchaguzi SM, na 2020 uchaguzi mkuu ule ndio rasmi ulikata rasmi hamu ya wananchi kupiga kura. Chungu za chaguzi zote za marudio zilivyokuwa na wapiga kura wachache, na chaguzi nyingine za marudio zitakavyokuwa na wapiga kura wachache.

Kwa huku bara wangalau CDM wakiamua kushiriki uchaguzi unaweza kuongeza idadi ya wapiga kura, lakini wasiposhiriki ndio utaona idadi ya wapiga kura halisi ambao ndio huwa wanaipa kura CCM, na hawa kimsingi huwa ni wachache kisha wanajazia na za wizi.
Zipo sababu nyingi zenye kuchangia upungufu wa wapiga kura, sio ajabu uchaguzi ujao idadi ya wapiga kura ikaongezeka kulinganisha na miaka iliyopita.

Bajeti ya kilimo kutoka bilioni 200 mpaka bilioni 700 ni ongezeko kubwa sana, linakwenda kugusa sekta nyeti sana, inayogusa maisha ya watanzania wengi.
 
Hayo mabadiliko ya kimtazamo ni kwakuwa vyama vya upinzani hasa CDM hawafanyi ushawishi wake kwa umma. Lakini sasa hivi CDM wakianza uhamasishaji na watu wakajaa, utaona yale yale. Inshort CCM sio chama cha kizazi hiki, na kwa bahati mbaya hakikubaliani na ukweli huo, ndio maana kinatumia vyombo vya dola kukaa madarakani kwa shuruti.
Hata CDM sio wa kizazi cha sasa wanapitwa na wakati kila kukicha. Mbinu zao hazibadiliki bora hata CCM wanao uzoefu wa kushughulika na watu wakiwa na jukumu la kuongoza nchi, kulinganisha na CDM.

Uongozi wa CDM tangu 2004 ni ule ule, miaka 18 sasa endeleeni kujidanganya kwamba nyinyi ni chaguo la kizazi kipya wakati huo CCM wanafanya mapinduzi ya kimtazamo.
 
Back
Top Bottom