Bongo Trust
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 252
- 241
Kwa katiba hii Samia ataenda hadi twenty thirty bisha at your own risk
Mmeharibu nchi kiukweli so hakuna kupewa nchi.
Kwamba unakataa mtaani hali sio ngumu?ndugu tupo mitaani kwani nazungumza kutoka wapi? yaani kila mtu yupo busy na mambo yake ya kutafuta hela wewe unaonekana huna cha kufanya na huna chakufanya kwasababu ni mvivu unasubiri uletewe hakuna hela rahisi ndugu hata ukiangalia utawala wote uliopita hakuna aiyekuwa anagawa hela
Ukiwaona hapa jukwani utadhani wao mambo yako poa sana.🤣🤣Jamaa jinga sana
Wananchi wa kawaida labda umaanishe hawa wanaoshinda JF wakiandika maoni yao, lakini hao wa huko chini watampigia kura tena nyingi sana.
Bajeti ya wizara ya kilimo imeongezwa zaidi ya asilimia sabini, kilimo kimeguswa moja kwa moja kwa maana ya pembejeo na ufufuaji wa mazao yaliyokuwa yakipuuzwa miaka ya nyuma. Hao wote ni wapiga kura na ni wengi sana kulinganisha na wapambe wanaoshinda humu jukwaani.
Wenye uelewa mdogo ni wachache, wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaofaidika moja kwa moja na mapinduzi ya kilimo yanakwenda kufanyika nchini.Kwa bahati mbaya sioni wapiga kura kujitokeza kwa wingi tena kwani box la kura limepuuzwa rasmi. Mnaweza kuzungumzia kushinda, ila sio kwa idadi ya wapiga kura kama wapiga kura. Nina hakika wapiga kura watakuwa wachache kuliko kipindi chochote ndani ya nchi hii. Wengi wa watakaojitokeza kupiga kura ni wenye uelewa mdogo.
Ngoja chodomo waendeleee kujiaminisha kwenye mitandao 😄😄Wenye uelewa mdogo ni wachache, wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaofaidika moja kwa moja na mapinduzi ya kilimo yanakwenda kufanyika nchini.
Wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaojishughulisha na maisha halisi huko mtaani. Mimi na wewe wa mitandaoni huwa hatuoni maana ya kupiga kura, tunaishia kulalamika huku tukizeeka na malalamiko yetu.
Kina Tindo wanakariri maisha hawajui kuwa kuna mabadiliko makubwa ya kimtazamo yanayoendelea ndani ya CCM hivyo nchi nzima.Ngoja chodomo waendeleee kujiaminisha kwenye mitandao 😄😄
Sio tuu Kilimo bali wamama kwa maelfu watampigia kura kwa sababu anawapa ile mikopo isiyo na riba kupita Halmashauri na Banks,amewatua ndoo kichwani na kuwajengea vituo vya afya .
Sio kila mwaka ni 2020. CCM ikidhibitiwa wizi wake inashindwa.
Kina Tindo wanakariri maisha hawajui kuwa kuna mabadiliko makubwa ya kimtazamo yanayoendelea ndani ya CCM hivyo nchi nzima.
Huyu ni rais mwanamama, anayo huruma ya asili, hana kiburi wala hana ule ujinga wa kutaka kuwakomoa baadhi ya watu wanaokupigia kura.
JangaTujikumbushe kidogo 😁😁😁
View attachment 2231225
Hao raia wa kawaida/wauza karanga wana uwakilishi wa nguvu ndani ya kamati kuu ya CCM? Huko ndiko Rais wa Tanzania anateuliwa na kusimikwa. Kule kwa Mahera ni bra bra tu na ulaji vinafanyika.Pamoja na kuwa mpaka sasa hakuna mpinzani makini na uhakika walio makini wamejificha na wanasubiri 2025 ikaribie na watajitokeza.
Lakini wakurugenzi wadhibitiwe kuchakachua matokeo na tum ya uchaguzi idhibitiwe kuchakachua matokeo. Rais Samia hatashinda.
CCM imegawanyika na wanaCCM wengu ndio watamnyima kura. Changanya na raia wa kawaida ambao tangu arithi urais kwao ni tabu tu maana hata wauza karanga wanamchukia kwa magumu wanayopata.
Sasa hapo ndio ashinde Urais?
Wenye uelewa mdogo ni wachache, wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaofaidika moja kwa moja na mapinduzi ya kilimo yanakwenda kufanyika nchini.
Wengi wa watakaopiga kura ni wale wanaojishughulisha na maisha halisi huko mtaani. Mimi na wewe wa mitandaoni huwa hatuoni maana ya kupiga kura, tunaishia kulalamika huku tukizeeka na malalamiko yetu.
Hujui nguvu ya umma. Ipo siku itanyanyuaka hata hao wanausalama watakubali.
Zipo sababu nyingi zenye kuchangia upungufu wa wapiga kura, sio ajabu uchaguzi ujao idadi ya wapiga kura ikaongezeka kulinganisha na miaka iliyopita.Sibahatishi ninachoongea, nimeona ni kwa kiwango gani watu hawajitokezi kupiga kura, na ule uhayawani uliofanyika 2019 uchaguzi SM, na 2020 uchaguzi mkuu ule ndio rasmi ulikata rasmi hamu ya wananchi kupiga kura. Chungu za chaguzi zote za marudio zilivyokuwa na wapiga kura wachache, na chaguzi nyingine za marudio zitakavyokuwa na wapiga kura wachache.
Kwa huku bara wangalau CDM wakiamua kushiriki uchaguzi unaweza kuongeza idadi ya wapiga kura, lakini wasiposhiriki ndio utaona idadi ya wapiga kura halisi ambao ndio huwa wanaipa kura CCM, na hawa kimsingi huwa ni wachache kisha wanajazia na za wizi.
Hata CDM sio wa kizazi cha sasa wanapitwa na wakati kila kukicha. Mbinu zao hazibadiliki bora hata CCM wanao uzoefu wa kushughulika na watu wakiwa na jukumu la kuongoza nchi, kulinganisha na CDM.Hayo mabadiliko ya kimtazamo ni kwakuwa vyama vya upinzani hasa CDM hawafanyi ushawishi wake kwa umma. Lakini sasa hivi CDM wakianza uhamasishaji na watu wakajaa, utaona yale yale. Inshort CCM sio chama cha kizazi hiki, na kwa bahati mbaya hakikubaliani na ukweli huo, ndio maana kinatumia vyombo vya dola kukaa madarakani kwa shuruti.