Lidafo
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 551
- 747
Habari wanajamvi!
Kwa anayefuatilia siasa za Tanzania atakubaliana na mimi kuwa kwa sasa Mh. Paul Makonda Katibu mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndiye anayetamba katika anga za Kisiasa hapa nchini, Ujio wake umekuwa wa kishindo sana na hii ni karata muhimu kwa Rais Samia kuelekea mbio za uchaguzi wa 2025 nitaelezea kwa ufupi kwanini makonda ni karata ya muhimu kwa Rais Samia.
Tufahamu kuwa kipindi cha Hayati Dr. Magufuli alianzisha siasa zilizojulikana kama siasa za kutetea wanyonge na kupitia mbinu hii alifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90% kuteka nyoyo na akili za watanzania hasa wa tabaka la chini ambao walikuwa wakifurahishwa na jinsi Dr. Magulfuli alivyokuwa akiwawajibisha viongozi.
Baada ya Rais Samia kupokea kijiti cha Urais aina ya siasa za Hayati Magufuli zilionekana kupotea na kundi kubwa la watu wa tabaka la chini halikupenda viongoizi wanapokosea kutowajibishwa na hii ilipelekea taratibu Rais Samia kuanza kupoteza mvuto hasa kwa raia wa hili tabaka la chini.
Inaonekana Samia alipewa ushauri wa kumrudisha Makonda kuwa active kwenye siasa tena ndani ya chama na akaukubali kwani Makonda anaziweza siasa za Hayati Dr. Magufuli na hivyo lile kundi kubwa la watu lililopoteza imani na serikali ya Dr. Samia taratibu litaanza kurudisha imani kwa serikali na hili linajidhihirishakupitia mikutano ya Mh. Makonda inayoendelea Tanzania. Hapa ni kusema kuwa ujio wa Mh. Makonda ni wa kimkakati Zaidi.
Niseme tu kama Mh. Samia kaamua kutumia karata hii ya makonda ni wazi kuwa timu Magufuli bado walikuwa na nguvu ndani ya chama na hivyo haikuwa sahihi kuwaapuuza lakini hii ni ishara huenda kufikia 2025 wengi katika wanasiasa wenye mrengo wa Hayati Dr. Magufuli wakarudishwa kundini ili kumsaidia Rais Samia katika kampeni za 2025, Ingawaje inaonekana mchuano utakuwa mkali sana ndani ya chama kwani kuna loophole nyingi sana zinazoweza kutumika kumuweka mgombea mwingine tofauti na Samia.