Rais Samia asaini miswada ya Sheria za Uchaguzi

Taarifa zilizosambazwa kwa vyombo vya Habari Nchini Tanzania zinaeleza kwamba Rais wa Nchi hiyo amesaini ile Miswada mibovu inayopingwa na kila mwenye akili timamu

Bila Shaka kwa kitendo hiki inamaanisha kwamba Rais Samia AMEWAPUUZA KABISA WALE WOTE WANAOPINGA MISWADA HIYO MIBOVU YA SHERIA ZA UCHAGUZI .

---

Rais Samia Suluhu Hassan amesaini miswada minne ya sheria iliyopitishwa na bunge kuwa sheria. Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ametaja sheria hizo kuwa ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani; Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Taifa; Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.

Soma: Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024

Samia ana uchu mkubwa wa madaraka, anajua demokrasia ili kujua mkondo wake hawezi kupenya na waarabu wanamtaka abaki ili aendelee kuwauzia Tanganyika yetu
 
Kususa kuna kuwa na maana kwa kiongozi mwenye akili na hekima, kwa sababu anatazama athari zake mbeleni. Ambaye hana, ukisusa yeye atashangilia.

Hapa inatakiwa kutangaza maandamano yasiyo na mwisho, na kumtangaza yeye binafsi kama adui wa demokradia na ustawi wa nchi.
Screenshot_2024-03-08-20-57-04-1.png
 
Inasikitisha sana mkuu, chakufanya hapo ni Chadema kususia uchaguzi tuu ili kutuma ujumbe kwenye mataifa kuwa Tanzania sio sehemu salama
Mawazo kama haya etu tuwape Nchi.

Ubasusia kula huku unanjaa!
Mwanaume anajipambania sio kudeka kwa wanaume wenzio!
 
The right option ni status quo.

CHADEMA washiriki uchaguzi kama utakavyokuwa kama hapo awali.

Manufaa ya CDM kushiriki:

1. CCM, serikali na vyombo vya dola watasota kuiba uchaguzi, kukimbizana na masanduku ya kura, kupiga wananchi virungu, na kukesha kufuatilia nyendo za wagombea, viongozi, na wafuasi wa CDM. Watashuhudiwa na umma wa Watanzania na wadau duniani.
2. CCM wataendelea kuipata saikolojia ya kuzidiwa kura na CDM kwa kushuhudia kura halisi vs matokeo ya mchongo wanayotangaza. Wao ndio huwa wanaoiona hesabu halisi ya kura.
3. CDM pamoja na kudhulumiwa, nafasi yao katika siasa na upinzani wa kulazimishwa itakuwa juu tu: watapata wabunge wengi, madiwani, etc. Hii ni pamoja na kufaidika kiuchumi kwa chama na wanaoshinda uchaguzi (individuals). Uhai wa chama ni muhimu.

Hasara za CDM kushiriki:

1. Wananchi kuibiwa uchaguzi wao (hata bila ya ushiriki wa CDM). 2. Vipigo, Majeruhi na hata vifo kuongezeka kutokana na jazba ya CCM na vyombo vya dola kukamia kuzuia umaarufu na ushindi wa CDM. 3. Matumizi ya kutisha ya pesa za umma kununua wagombea na viongozi wa CHADEMA kutafuta kupunguza au kuondoa ushindani; kuhonga wapiga kura pesa, nguo, chakula, pombe, usafiri, n.k.; ufisadi mkubwa kwa wanaoshika hizo pesa.

CHADEMA wameshafanya kazi kubwa kuwapigania Watanzania haki zao. Kama wananchi hawaamki na kuunga mkono mapambano basi wao CDM waendelee kuithibitisha nafasi yao katika jamii na kujikusanyia chao toka kwenye keki ya taifa ili wasife. Kila mtu ajijue kivyake hadi siku watu watakaporejewa na fahamu kuwa nchi inaelekea kuzimu.

CDM wasiposhiriki kwa jinsi nchi hii ilivyo watapotea kabisa! Na ndio lengo kuu la CCM. CCM inafanya mapambano ya attrition (kuwakatisha tamaa na kuwachosha wapinzani wa kweli hadi waachane na mapambano). Rejea kilichomtokea Halima Mdee na Covid 19, Nasari, etc. Wamelegezwa bila kutaka! Sad!

CCM wamefanikiwa kuwachosha Watanzania hadi political apathy imetamalaki. Sasa hivi nguvu zote zinaelekezwa CHADEMA. Ndilo changamoto kuu lililobakia. Na inaaminika Mbowe ndio tatizo kubwa kuliko hata Lissu katika kuvunja will ya CDM. Fuatilia kelele za JF.
 
Hivi upinzani nchi hii umekufa kiasi hiki?? Zama hizi za uwazi na watu wameamka bado tu mnakuwa na hofu na woga?? Sukari bei, umeme haueleweki, maji, ajira hakuna n.k Bado kwenye uchaguzi mnapigwa tu kama watoto wadogo mnaishia kususa tu bila kuchukua hatua? Nchi zote za Afrika yameshafanya mabadiliko vyama tawala vimeangushwa isipokuwa Tanzania! Si kwamba CCM inafanya vizuri, hapana bali ni udhaifu wa upinzani, Shida iko wapi?
 
Mbona Kama unayumba na hujui unachosimamia? Post yako no. 11 umeandika nini na hii umeandika vitu gani! Acha kuvuta Cha Arusha Kama ulivyoshauriwa na waziri mkuu!
Nmesema Chadema wasusie uchaguzi, sasa nmeyumba wap
 
Back
Top Bottom