MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,644
- 33,455
Hii ni spinning ya kizamani kumu implicate JPM kwenye hii issue. Ilikuwa case ya kijinga na imezaa aibu na rekodi mbaya!Kwa kukubali viongozi wa dini kumvaa na kwa uhakika ni kwa ushawishi wa askofu shoo rais samia ameonyesha udhaifu mkubwa.
Gharama kiasi gani zimepotea kuendesha kesi dhidi ya Mbowe? Kwanini asisubiri ahukumiwe.
Magufulists hakika tumeudhika sana kuona huyo gaidi aliyekua ameanza kampeni mbaya kumdemonise Magufuli serikali ya Samia imemuachia.
Na ngoja samia ndio atawajua Chadema. Watasema wameshinda kesi ya uonezi na huyohuyo Mbowe ndio ataanza mashambulizi dhidi ya serikali ya CCM akikejeli na kutukana.
Uhakika Mbowe angekutwa na makosa na kuhukumiwa aende jela lakini askofu wa Chadema shoo bila shaka ameweza kuwashawi viongozi wa dini kumuomba rais kesi ifutwe kwenye hatua ya kujitetea mtuhumiwa.
Ili kuleta furaha kwa wote basi Mama Samia atoe msamaha na kufuta kesi zinazomkabili Sabaya. Tunajua Chadema kwa akili yao wanafikiri Mbowe hawezi kua gaidi na kwamba sabaya ni jambazi.
Sisi Magufulists tunaamini Mbowe angekutwa na hatia ya ugaidi na Sabaya amekua framed na wafuasi wa Mbowe. Kwahivyo Sabaya naye aachiwe vinginevyo hakuna kuelewana.
Kama Mbowe kesho asubuhi akianzisha tena vuguvugu la katiba mpya bila ukomo watakosa la kumfanya na pending na Chadema ilivyojiandaa wanaweza kutwaa dola uchaguzi ujao.