Rais Magufuli: Pesa za Uhuru zijenge barabara ya Mwenge-Morocco Dar es Salaam

Hii speed ya magufuli itakuja kupunguzwa na wale walevi wetu wa bungeni, ngoja waje na akili zao za viroba kujifanya wanajua sana kujifanya wazalendo sana kumbe wapo kwa maslahi yao tu,
Hawa ndio wameturudisha nyuma sana, roho inauma sana kuwa mawaziri watatoka miongoni mwao,
 
Ni bora ata katiba ije ibadirishwe ili Magufuli aongoze miaka 20 bila kufanyika uchaguzi mkuu tu sasa maana hakuna namna.

Kweli kabisa mkuu ukizingatia uchaguzi ni ma bn mengi sana na tunaowachagua huwa wanaishia kutuzingua, ni heri aendelee ili kila kitu kikae sawa kwanza. Kama Putin vile.
 
Last edited by a moderator:
Makatibu wakuu wanatosha sana sema tu katiba inatambua mawaziri.
Huyu jamaaaaaaa ni shee3eeeeeeeda 4x
 
Asilimia kati ya 75-80mya pato la Taifa inatoka Dar. Tukiimarisha Dar na kupunguza foleni tutaongeza ufanisi wa kazi na kukusanya kodi nyingi zaidi ambayo itatumika kujengea barabara zingine nchini. Ningependa kama ingewezekana bajeti nzima ya mwaka ya barabara iwekweze Dar baadae kungine si kwakuwa naishi Dar ila kwa sababu za Kiuchumi.

Japo sina uhakika na chanzo chako cha habari, tunaomba kuuliza, hivi nchi hii kila kitu ni Dar peke yake, ama Dar ndio kuna walipa kodi peke yao?
 
Tanganyika tu matajir sana hata shetani anatushangaa tunaishi kutegemea misaada, hii sio haki hata kidogo
 
Ni hatua nzuri sana lakini mbona pesa zote zinaelekezwa mkoa wa Dar?
Ina maana sie wa Bukoba hatupaswi kuneemeshwa na hizi pesa za zuio la Magufuli!
Ina maana Dar wao peke yao ndio wanalipa kodi?

Magufuli acha ubaguzi, hizo pesa zilenge kusaidia watanzania wote nchini na sio kwa wakazi wa Dar peke yao.

Mbona kijijini kwako Chato uliweka taa za kuongozea magari wakati hakukuwa na umuhimu kivile maana magari huko ni moja moja.

Nafikiri logic ilikuwa ni kwamba sherehe zilikuwa zifanyike kitaifa Dar, Singida nafikiri labda wataambulia zile za sherehe za ukimwi duniani.
Kiukweli, ili nyie muwe poa huko, lazima Dar pawe sawa kwanza.
 
Ni bora ata katiba ije ibadirishwe ili Magufuli aongoze miaka 20 bila kufanyika uchaguzi mkuu tu sasa maana hakuna namna.

Duh DAKA MTUMBA tayari mhemuko imeanza kuharibu hata uwezo wa kufikiri!!! Tumuombee Mh. Rais maana vita aliyoianza ni ngumu sana!! Mafisi hayafurahi na ni magumu kukata tamaa unaweza kukuta yameshaanza mipango ya kujibu mapigo...
 
Last edited by a moderator:
Hii speed ya magufuli itakuja kupunguzwa na wale walevi wetu wa bungeni, ngoja waje na akili zao za viroba kujifanya wanajua sana kujifanya wazalendo sana kumbe wapo kwa maslahi yao tu,
Hawa ndio wameturudisha nyuma sana, roho inauma sana kuwa mawaziri watatoka miongoni mwao,

Kama umesoma article kuhusu mtazamo wa act kuhusu uchaguzi ilivyosemwa na zitto kabwe, kama Magufuli ataendelea na spidi hii kuna uwezekano wabunge watakaokuwa wanaenda kinyume na Magufuli wakaadhibiwa na wananchi majimboni kwao! Hivyo nadhani wabunge watakuwa waangalifu sana kulinda matumbo yao kwa kutowaudhi waajiri wao ambao ni wananchi.
 
Ndio mana leo nime lipa kodi kwa roho nyeupee japo nilikuwa na nafasi ya kufanya bla bla bla, Ninaimani sasa na rais DR. MAGUFILI, inauma sana yani mtu unalipakodi iliizunguke nakurudi kwa wanyonge huku mitaani, alafu mijitu inagawana tu huko juu. Ndio maana watu sazingine wanavunjika moyo na kutafuta mwanya wa kukwepa. Naapa kwa dhamira hii ya magufuli sitajaribu kukwepa kodi kamwe.

MUNGU atupenini jamani huyu mahufuli ndio mtu unaweza ukasema ni chaguo la MUNGU. Piga kazi rais wetu tupo nyumayako tutakupasaport ya kutosha.
MUNGU akubariki sana kila laheri.
 
The guy's something ekse. Japo ningefurahi kama angemaliza kiporo cha afya, akasambaza vifaa tiba throughout. Hasa vile ambavyo ni muhimu, nadhani hizo 4...bn zingefanya makubwa tu katika sekta ya afya.
Anyway, good move Dr. President.
 
Public Procurement Act 2011 inasemaje? Hakuna mchakato ni kuagiza tuu hata bila hata Budget Revision?
 
Back
Top Bottom