hopaje
JF-Expert Member
- Jan 11, 2013
- 1,726
- 1,218
Kwa maoni yangu, mimi siamini hata kidogo kwamba mheshimiwa rais Magufuli hatawakumbuka watumishi wa umma. Hiki ni kipindi kifupi tu cha mpito, siku zote kipindi cha mpito huwa ni kigumu japo siyo sana. Imani yangu ni kwamba, MAGUFULI atakuwa ni rais pekee ambaye ataleta mabadiliko chanya makubwa katika nchi yetu. Huyu ni rais ambaye ataleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kimfumo katika nchi yetu. Naomba tumpe muda, tuwe wavumilivu kidogo katika kipindi hiki kama watanzania wenzetu walivyovumilia wakati na baada ya vita vya Tanzania na Uganda.
Unaota???