Ridhiwani Kikwete: Watumishi tatueni kero za wananchi haraka kabla ya kufika kwa Viongozi wa Kitaifa

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewataka watumishi kutoka taasisi zote za serikali za umma kutatua malalamiko na changamoto za wananchi kwa wakati ili kuondoa msongamano wa wananchi katika ofisi za juu zaidi.

Ameyasema hayo jana wakati wa kufunga kikao kazi cha taasisi simamizi za madili katika Umutendaji, kitaaluma na watumishi wa umma kutoka wizara na taasisi za umma katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa PSSSF Jijini Dodoma.

Kikwete ameeleza kwamba ni matarajio ya serikali kila mtumishi wa umma akiwajibika ipasavyo katika majukumu yake atasaidia wananchi wengi kupata huduma kwa wakati na itaondoa lawama kwa viongozi kila siku kulalamikiwa.

"Nimatarajio yangu kuwa ninyi kama wawakilishi wa watumishi katika taasisi zenu, mtakuwa chachu kwa wengine katika uzingatiaji wa maadili, hakikisheni mnatatua malalamiko ya wananchi ili kuwapunguzia viongozi wa kitaifa kutatua malalamiko ambayo yangeweza kutatuliwa katika sehemu zenu za kazi." alisema Kikwete.

"Maadili mema ni msingi mkubwa katika utoaji haki, hivyo watumishi wa umma zingatieni maadili ili haki itendeke wakati wote wa utoji huduma kwa wanachi wetu pasipo upendeo au ushawishi wa jambo fulani". aliongeza Kikwete.

Aidha Naibu Waziti Kikwete aliwakumbusha washiriki hao kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi katika sehemu zao za kazi na zaidi kuwa kiungo kizuri kati ya serikali na wananchi katika utoaji huduma bora.

20230927_084048.jpg
20230927_084045.jpg
20230927_084043.jpg
 
Huyu kazi anayoiweza ni kulipa media wamwandike akitoa matamko empty.

Ukienda kwenye Twitter page ya utumishi zimejaa habari zake akitoa matamko ya ajabu ajabu yasiyo na mpingo wala mikakati yoyote.

Hana tofauti na wale wengine wa mbeleko, akina Januari na Nape.
 
Hakuna kitu rahisi sana kwa wanasiasa kama kutoa matamko...😂
 
Atoke ofisini aende akawasikilize wananchi akifuatana na watumishi, kisha awape deadline
 
Kero yangu ni mtoto wa kigogo mmoja aliyekamatwa China na madawa ya kulevya, lini atarudi China kwenda kunyongwa ili turudishiwe gas yetu iliyowekwa kama dhamana?
 
Back
Top Bottom