Rais Magufuli, bila kuwajali Watumishi wa Umma utakutana na Magumu zaidi ya Kikwete

Watumishi wa umma wanaongoza kwa uchelewaji ofisini kuwahi kutoka ofisini, kufanya shughuli zao za pembeni muda wa kazi halafu wanataka waongezwe mishahara nyie watu badilikeni kwanza....
Nani aliyeyasababisha yote haya kama siyo ubovu wa viongozi wa kisiasa hawa hawa?
 
Hebu fikiria watu wamekopa wamejenga nyumba haijaisha madeni hayakipiki unaambiwa twende dodoma ! Hafikirii maisha ya watu na familia zao. Sasa kweli tutakuombea Mungu kivipi?
Katika jambo1ambalo mheshimiwa anafurahisha uma ila anaudhi nguvu kazi yake ni hili la Dodoma.
 
Wapo kibao, wanafuatilia na kisha kuwakilisha. Utashangaa tu, Simu hiyo(kwa namba isiyojulikana). Wewe Fulani, pumbavu kabisha hizo taarifa umezitoa wapi. Futa kabla hatujakupiga ''Drilling'' Shauri lako.
Mimi Mjumbe tu Mkuu, na Mjumbe hauwawi sijawakejeri wala kuwatukana. Zaidi ya yote ni kuwasaidia wao badala ya kutumia nguvu watumie akili.
 
Ungekuwa Mejor General Kamzora huenda ange kusikiliza ila asie MHANDISI wala Askari ume ULA wa chuya
 
Watumishi wa umma wanaongoza kwa uchelewaji ofisini kuwahi kutoka ofisini, kufanya shughuli zao za pembeni muda wa kazi halafu wanataka waongezwe mishahara nyie watu badilikeni kwanza....
sometimes i wonder if people do real think before they write down
 
Ukiona Mshahara mdogo kavaa nyumban au kuwa Mkulima, Nchi sio ya Wafanyakazi wa Umma peke yao.
Kama una Majukumu makubwa na Mshahara hautoshi achia wengine wafanye.
 
Ukiona Mshahara mdogo kavaa nyumban au kuwa Mkulima, Nchi sio ya Wafanyakazi wa Umma peke yao.
Kama una Majukumu makubwa na Mshahara hautoshi achia wengine wafanye.
Umeelewa kilichoandikwa au umechangia tu ili uonekane nawewe umo? Acha mihemko hiyo.
 
Watumishi wa umma wanaongoza kwa uchelewaji ofisini kuwahi kutoka ofisini, kufanya shughuli zao za pembeni muda wa kazi halafu wanataka waongezwe mishahara nyie watu badilikeni kwanza....

Mkuu
Hivi hilo unaloandika ni kweli?
Hebu fanya kautafiti kadogo uone jinsi hoja yako inavyo tofautianana huo utafiti.
Sasa hivi mambo yamebadilika sana mkuu.
 
Uhanga wako wa kukosa ajira isiwe kero kwa wengine. Ni vema ukakaa kimya usiku haya yatakusaidia nawewe kula yako hapo ulipo kwa ndugu yako.
Wahanga wako wengi humu hatari wananjaa atafisi ananafuu watumishi kiukweli sasaivi wanaishi kwavitisho hofu utathani unafanya kazi dukani kwa muhindi maana huna pakuomba msaada ukiongea tu kakufukuza dah! Izishida sjuizitaisha lini
 
Mkuu
Hivi hilo unaloandika ni kweli?
Hebu fanya kautafiti kadogo uone jinsi hoja yako inavyo tofautianana huo utafiti.
Sasa hivi mambo yamebadilika sana mkuu.
Wanajiropokea tu kwavile hawajahi kuwa watumishi na ni wahanga wa kukosa ajira hivyo wanadhani ndiyo nafasi yao ya kukandia waliyoopo ili wapate wao.
 
Kwani kuhusu watumishi rais kasema hana mpango nao? ama unahisi nchi no sawa na familia yakp
 
Hata kama watumishi wana mapungufu nchi imesonga mbele kupitia haohao watumishi. Zaidi ya kuwa ofisini wanachangia kwa kushiriki shughuli nyingi za kiuchumi tena kitaalamu. Mfano kiliimo, ufugaji na biashara. Haifai kuwabembeleza japo pia haifai kuwapuunza. Ni kama vile watumishi wanaonekana wezi, wavivu na mafisadi mbele ya jamii. Hii inafanya wasio watumishi kushangilia kuona namna wanavyosemwa na kutumbuiwa. Ni wanafamilia tu wanaowanea huruma ndugu zao.
 
Nakumbuka namna ambavyo familia yetu ililazimika kuwa shabiki wa Simba mpaka Leo nina familia yangu bado niko Simba.

Alichokua anafanya baba ni kutuandalia wali nyama na soda kila mara Simba ikicheza na ikashinda. Isiposhinda hakuna wali.

Masikini sisi kipindi kile hata mpira wenyewe hatuujui, tukawa tunaombea Simba ishinde tule wali. Familia nzima inashangilia mpaka tunatetemeka, eti Simba ishinde baba anunue wali.

Sasa nafananisha Ujumbe huu na namna ambayo Mimi nilipata kuwa mwanasimba. Magufuli akiwabeza watumishi, watumishi wanaweza sababisha wananchi wote kumchukia na akafeli kweli.
Mawazo ya kitoto haya! Mzazi wako wakati huo alikuwa muadilifu sana kazini kwake ndio maana aliweza kuwanunulia nyama nk. Ninaamini alinunua akiwa na moyo mweupeee kabisa.
 
Kwa maoni yangu, mimi siamini hata kidogo kwamba mheshimiwa rais Magufuli hatawakumbuka watumishi wa umma. Hiki ni kipindi kifupi tu cha mpito, siku zote kipindi cha mpito huwa ni kigumu japo siyo sana. Imani yangu ni kwamba, MAGUFULI atakuwa ni rais pekee ambaye ataleta mabadiliko chanya makubwa katika nchi yetu. Huyu ni rais ambaye ataleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi na kimfumo katika nchi yetu. Naomba tumpe muda, tuwe wavumilivu kidogo katika kipindi hiki kama watanzania wenzetu walivyovumilia wakati na baada ya vita vya Tanzania na Uganda.
 
Hata kama watumishi wana mapungufu nchi imesonga mbele kupitia haohao watumishi. Zaidi ya kuwa ofisini wanachangia kwa kushiriki shughuli nyingi za kiuchumi tena kitaalamu. Mfano kiliimo, ufugaji na biashara. Haifai kuwabembeleza japo pia haifai kuwapuunza. Ni kama vile watumishi wanaonekana wezi, wavivu na mafisadi mbele ya jamii. Hii inafanya wasio watumishi kushangilia kuona namna wanavyosemwa na kutumbuiwa. Ni wanafamilia tu wanaowanea huruma ndugu zao.
Ni lini Rais Magufuli alisema anawanyima mishahara watumishi wa umma? Wanaoshughulikiwa ni wezi, wavivu, na wazembe. Iweje wanaofanya kazi kwa uadilifu wanung'unike? Hivi wooote mnaolalamikia hatua zinazochukuliwa mmewahi kukumbwa na uzembe wa watumishi wa umma waliojisahau kwamba wao ni watumishi umma na sio vinginevyo!
 
Back
Top Bottom