Mambo 10 yaliyotekelezwa kwa ufanisi tangu yalipowasilishwa na watumishi mbele ya Rais Samia

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
cbfcdad2-e4a9-40c7-92e5-59adad5eeec9.jpg
Na Mwl Udadis, Morogoro

Uweledi wa kiongozi hupimwa kwa hatua na matokeo. Leo tukisherehekea siku ya wafanyakazi #MeiMosi hatuna budi kuangalia hatua alizochukua Rais Samia tangu alipoingia madarakani akilenga kustawisha maisha ya watumishi wote;

1. Mikataba ya hali bora ya kazi kwa Taasisi za umma na uidhinishwaji wa miundo ya Taasisi na miundo mbalimbali katika sehemu za kazi.

2. Uundwaji wa mabaraza ya Taasisi 40 za umma ambazo hazikuwa na mabaraza ya wafanyakazi. Hii ni zaidi ya upendo kwetu watumishi kwa kuwa itaimarisha ufanisi wa kazi.

3. Kulipwa kwa mafao kwa wakati kwa watumishi wanaostaafu. Kuwapa mafao kwa wakati wastaafu ni haki yao na heshima kubwa kwa kuwa ni uthibitisho kuwa Rais Samia anatambua thamani ya wafanyakazi wakiwa kazini na hata baada ya kustaafu.

4. Kulipwa mafao watumishi waliokuwa wameondolewa kazini kutokana na dosari katika vyeti vyao. Hii ni uhakika kwa kuwa sote ni mashuhuda watumishi takribani 9771 waliokuwa wanadai bilioni 22.22 kutoka PSSSF walishaanza kupokea fedha zao.

5. Kupunguzwa kwa kiwango cha kodi ya mapato ya PAYEE kutoka 9% hadi 8% na kuweka nyongeza ya mshahara.

6. Kuondoa tozo katika miamala ya kibenki na kulipa madai ya watumishi. Tangu alipoingia madarakani Rais Samia, watumishi wapatao 116,792 wamelipwa madai na stahiki zao mbalimbali na kazi inaendelea kwa wote wenye sifa za kulipwa.

7. Kuongeza umri wa watoto(wategemezi) wa wanachama wa NHIF. Hii iko wazi tayari umri umeongezwa mpka kufikia mika 21 kwa watoto wategemezi kwa wanachama wa NHIF.

8. Kutoa ajira mpya kwa watumishi wa umma. Mpaka sasa ni zaidi ya vibali vya ajira 55,000 tayari vimeshatolewa na Rais Samia tangu alipoingia madarakani na kila siku tunaona matangazo mapya ya ajira. Hii ni kubwa sana.

9. Kupandisha madarajawatumishi. Kwa Takwimu zilizopo ni karibu watumishi 264,491 wamepandishwa madaraja tangu Rais Samia aingie madarakani. Kwa ahadi ya leo tutarajie makubwa zaidi katika mwaka mpya wa fedha.

10. Kuondolewa tozo ya kulinda thamani ya fedha (VRF) kiasi cha 6% kwa mwaka kwa wanufaika wa Bodi ya Mikopo (HESLB) ambao wengi wao ni watumishi. Hii ni relief kubwa kwetu watumishi.

Haya ni baadhi tu ya mambo mengi yanayofanywa na Rais wetu mpendwa, jukumu limebaki kwetu watumishi wote kuhakikisha tunamuunga mkono Rais Samia kwa kutatua changamoto mbalimbali za wananchi ili wananchi waendelee kumuunga mkono kiongozi huyu anayejali watu wake.
 
Back
Top Bottom