Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

Kuna mtu alianzishaga uzi humu ndani kama wk mbili zilozopita akiomba Dr Ndaluchako ateuliwe kuwa Wazir wa elimu nahisi dua yake imekubaliwa, humu ndani kuna watu wanaona mbali sana.... Long Live JF!
 
hivi mtu kama alikosa na akajiuzulu hafai kabisa kuteuliwa tena?

nadhan suala hili inabidi tuliangalie kwa mapana yake. sioni tatizo kama mtu alijiuzulu apewe tena nafasi hasa kama alishinikizwa kujiuzulu kwasababu za mizengwe.
 
Watu wa Kaskazini wanajitapa ni wabunifu na wana akili mingi, ukizingatia huyu ni profetha; ngoja tusubiri tuone watu wa Kaskazini wakipiga mzigo.

Queen Esther

Nadhani maneno maneno ya humu kuhusu kuwaacha watu wa kaskazini ndo yamepelekea Maghembe kuteuliwa, tatizo huyu Prof simuelewagi kabisa utendaji wake. Sidhani kama atamudu hiyo wizara
 
Maghembe kawekwa kwa sababu za siasa kwani ni mbunge mmoja to wakuchaguliwa wa CCM kutoka Kilimanjaro. Ili CCM ionekane bado iko kwenye ramani mkoa huo na kwamba mkoa umetoa waziri. Au siyo alikuwa mtu wa kupigwa chini.

Hapo basi kasigina ile kauli yake kuwa ataunda baraza dogo la wachapa kazi
 
tunawatakia kazi njema fanyeni kwa manufaa ya wananchi wenu na c kwa ajili ya waliowapa izo nyadhifa za uwaziri
 
kwanza niwaombe mods msinichanganyie huu uzi na nyingine maana nataka kutoa yaliyo moyoni
mimi ni mtanzania, ingawa nakiri sipendi sana siasa lakini katika uteuzi wa mheshimiwa magufuli nimefurahishwa na mambo kadhaa
1. mh.Ridhiwani kikwete hajapata wizara yoyote
2.mwigulu na makamba wamekosa wizara nyeti
3.dr ndalichako kuwa waziri wa elimu
nawatakia sikukuu njema
 
Sio wewe tu wapo weng wameliona kwa maslah mapana,hao wizara nyet hawawez,helcopter zote ziko poa,kumbe deo kafa! lakn
 
Kwa hilo la kwanza nadhani ni feelings za watanzania wote wanaoitakia mema nchi hii.
 
MI NIMEPENDA KUKURUPUKA KATKA KUTUMBUA MAJIPU mfano mazao/mahindi heka 400, yafyekwa kwa madai wameinglia ENEO LA SERIKALI . . . . . . . . wakiotesha walikuwa wapi? mpaka yanakaribia kukomaa ndo unafyekelea mbali
 
Back
Top Bottom