Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 741
- 479
Uteuzi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amefanya mabadiliko ya Wakurugenzi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kama ifuatavyo;
- Ndugu Othman Omar Othman ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Ualimu. Kabla ya Uteuzi, Ndugu Othman alikuwa Mkuruenzi wa Braza la Mitihani la Zanzibar.
- Dkt. Rashid Abdulazizi Mukki ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani la Zanzibar. Kabla ya Uteuzi Dkt. Rashid alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mafunzo ya Ualimu.
- Ndugu Hafsa Talib Aboud ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Michezo na Utamaduni. Kabla ya Uteuzi Ndugu Hafsa alikuwa Marajis wa Elimu Zanzibar.