Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

Kigoma vichwa..hapa nadhani ndugu yetu xito hatatumika kutumia bunge kuwanyanyasa hawa mawaziri kama alivyofanya kwenye escrow
 
Pumbavu! toa ukanda/ukabila hapa. Hao watu wameteuliwa kwa sifa zao wala hawajaenda kuwakilisha waha/kigoma. Watz wote tunawaunga mkono wala hatuhitaji kujua walikozaliwa. Watu wa aina yenu ni majipu mnapaswa kutumbuliwa.
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Pumbavu! toa ukanda/ukabila hapa. Hao watu wameteuliwa kwa sifa zao wala hawajaenda kuwakilisha waha/kigoma. Watz wote tunawaunga mkono wala hatuhitaji kujua walikozaliwa. Watu wa aina yenu ni majipu mnapaswa kutumbuliwa.

Ujidanganye, asili ya mtu inabaki pale pale hivyo hawa watabaki kuwa wazaliwa wa Kigoma; Hata siyo siri wachagga wanalalamika kwa mara ya kwanza wameshindwa kutoa mjumbe katika baraza la mawaziri tangia nchi ipate uhuru:: Wanaisoma namba kikamilifu!!!
 
Awali ya yote tunatuma pongezi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli kutokana na uteuzi mzuri wa mawaziri katika wizara nyeti (Fedha na Mipango, na Elimu) wateule wote wakiwa ni wenyeji wa mkoa wa Kigoma. Pasipo kupepesa macho, wanakigoma tumeupokea uteuzi huu kwa mikono miwili, tutazidi kukipa kura za kutosha CCM.

vp na mikoa waliotoa ma rais wameijenga hiyo mikoa kushinda dar wanapokimbilia hao viongozi????
 
Mkuu MAFILILI, naona unataka mkatambike. Karne hii bado hii kitu iko kichwani!!
 
Awali ya yote tunatuma pongezi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli kutokana na uteuzi mzuri wa mawaziri katika wizara nyeti (Fedha na Mipango, na Elimu) wateule wote wakiwa ni wenyeji wa mkoa wa Kigoma. Pasipo kupepesa macho, wanakigoma tumeupokea uteuzi huu kwa mikono miwili, tutazidi kukipa kura za kutosha CCM.

Acha ukabila wewe. Mlikuja na wanamuziki Eka tudigite hamna aliyewaunga mkono kwa kuwa wa TZ watutaki ukabila. Ndio maana nyie mnaambiwa niakina Nkurunzinza hamtaki! Bado mna chembechembe za ukabila.
 
mleta mada ni mzembe ajabu. haya sasa, dr ndalichako et al wanatoka mkoa wako wa kugoma, umenufaika na kipi haswa? nyambavu mkubwa ww.
 
Idumu jf, pia hongera mama Ndalichako, katibu mkuu mtendaji wa enzi zile ukiwa NECTA mwenye weledi wa hali ya juu, sasa waziri.

Sina mashaka na utendaji wako ila jihadhari sana na wimbi la mfumo wa kisiasa ktk utekelezaji wa majukumu yako. Weka misimamo thabiti kama ulivyoweka misimamo wakati ule ukiwa NECTA.

Kazi njema na kila laheri.
 
Kumbe mama yuko vizuri kama kosa lenyewe lililomwondoa ni hilo kwa maelezo aliyotoa hakupasws kuondolewa kwenye nafasi hiyo nadhani majungu masufuria yaliikwa hapo.

yeye aliondoka pale katk utawala wa Jk baada ya serikali kuamua kutanua goli na kuamua kuwa wanafuz wa fom two ata wakifeli waendee ndio akaamua kuachia nyoya akenda zake kenya..naona magufuli kaona umuhimi wake
 
tkitu kilichomuondoa Joyce Ndalichako ni kuwa hakuwatendea haki vijana wa kiislamu katka somo la Islamic knowledge.

tujikumbushe

BARAZA la Waislamu Tanzania (Bakwata)
limemtaka Katibu Mtendaji wa Baraza la
Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako
kujiuzulu wadhifa huo akimtuhumu
kuwafelisha mitihani ya dini ya Kiislamu
wanafunzi wa kidato cha sita wa dini hiyo.
Kauli hiyo ya Bakwata imetolewa na Mufti
wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban
Simba katika mkutano wake na waandishi
wa habari jijini Tanga jana kuelezea
msimamo wa Waislamu nchini kuhusu
matokeo ya kidato cha sita, hujuma
inayoandaliwa kufanyika katika zoezi la
sensa pamoja na vurugu zilizotokea
Zanzibar.
Kuhusu hujuma ya mtihani, Mufti Simba
alisema kuwa matokeo ya mtihani ya dini
hiyo ya Kidato cha Sita yaliyotangazwa Mei
Mosi 2012, yaliwashtua wanafunzi Waislamu
waliofanya mtihani wa elimu ya dini ya
kiislamu (Islamic Knowledge), ambayo
yalionyesha kuwa asilimia 70 walifeli kwa
kupata daraja F.
Alisema matokeo hayo yalionyesha kuwa ni
asilimia 30 ndiyo waliofaulu kwa kupata
daraja D, ambapo waliopata alama za juu
kabisa nchi nzima ni wanafunzi saba
pekee.?Matokeo haya yaliwashtua wanafunzi
na wazazi, taasisi mbalimbali za kiislamu
zilimua kukata rufaa kuonyesha
kutokubaliana na matokeo hayo, hatimaye
baraza hilo
likabaini kuwa lilikosea na likaidhinisha
kutolewa matokeo
mapya,? alisema Mufti Simba.
Tayari Ndalichako ametoa ufafanuzi kuwa
kosa lililotokea akisema si hujuma bali ni la
kiufundi lililotokana na kubadili utaratibu wa
kufanya mitihani mitatu ya somo hilo kuwa
miwili, lakini mfumo wa ujumlishaji maksi
ulisahaulika kubadilishwa.
Ndalichako alilieleza gazeti dada la
Mwananchi, The Citizen, kuwa awali
matokeo ya mitihani mitatu yalikuwa
yanajumlishwa na kugawanywa kwa tatu
kwa kutumia mfumo wa kompyuta, ili kupata
alama rasmi za mtahiniwa, lakini safari hii
zilipojumlishwa alama za mitihani miwili ya
somo hilo ziliendelea kugawanywa kwa tatu
badala ya mbili kimakosa.

magufuli naona unafanya mambo bila tahadhari ya. kuamsha hisia zilizolala

argue don't shout
Hapo sioni chuki kwa Waislamu mkuu. Ni somo walikosea kusahihisha na tatizo wakali-fix. Iyo ni chuki au mistake?
 
Prof Maghembe alikuwa Waziri Mzigo na si mtu ambaye ni results oriented. Na anapenda mshiko..
Mtazamo wangu hakufaa kabisa kuwa waziri wa awamu hii
 
Back
Top Bottom