Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

Mahebe

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
319
63
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemalizia kujaza nafasi za uteuzi wa Mawaziri na Naibu Waziri alizobakiza wakati akitangaza baraza la Mawaziri la kwanza katika awamu ya tano yautawala wake


Uteuzi huo ni kama ifuatavyo;

1. Profesa Jumanne Maghembe - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii.

2. Dkt. Philip Mpango - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha na Mipango (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge).

3. Mhandisi Gerson Lwenge - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji.

4. Dkt. Joyce Ndalichako - Ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi.(Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge)

5. Mheshimiwa Hamad Masauni - Ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

6. Prof.Makame Mbarawa - Amehamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiliano

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewatakia heri watanzania wote katika Sikukuu za Maulid, Christmas na Mwaka Mpya na kuwataka washerehekee kwa amani na utulivu.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
23 Desemba, 2015

attachment.php

 

Attachments

  • 20151223094511.jpg
    20151223094511.jpg
    18.6 KB · Views: 28,977
Back
Top Bottom