Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,919
- 2,798
kama hizo barabara za hewani zitashuka toka mbinguni its ok. kama ni mpango mkakati ita ok!
Kwanza mradi wa mabasi ya kwenda kasi umeishia wapi , tuambiwe kwanza kuhusu mradi huo
Kwanza mradi wa mabasi ya kwenda kasi umeishia wapi , tuambiwe kwanza kuhusu mradi huo
hizo pesa atazitoa wapi? na je mradi utakamilika lini?
Kamuagiza nani!?
Hivi anaelewa hata 'feasibility study' ya hii kazi inachukua muda gani?
Majuzi hapa wamesema wapo njiani kuleta train ziendazo kasi ya ajabu (kupitia kwenye reli ile ile ya mjerumani!!?)
Hivi uchaguzi mkuu ni mwezi wa ngapi vile!!?
Nadhani imefika muda sasa tusiwe na president mwanasiasa
Hapo ndo tujue siasa zilivyo kiboko...
Hii ya treni ilizinduliwa kabisa...japo mpango ulikuwa ipite kwenye hizo reli za mjerumani.lakini walizindua na ikaenda safari moja,sasa ni mwaka wa tatu hakuna kilichoendelea,....
......... Then, hao maofisa wa mipango miji wanafanya kazi gani sasa? unaweza kukuta wengine hata wamepanga manzese,na kwa nini hadi wapate amri kutoja juu? Tukija kwenye swala la flyovers ni kwamba linatekelezeka au ni kampeni tu? isije ikawa kama ile ya maisha bora.
Kuna mambo mengi ambayo Mh! anaagiza yafanywe na hayafanyiki. Mradi wa mabasi ya kasi umeyeyuka na hatuambiwi kinachoendelea. Lakini je flyovers ndio suluhisho pekee la trafic jam Dar Es Salaam? Hayo magari yatakuwa yanapita kwenye hizo flyovers kwenda kupaki wapi? Magari kutoka pande zote za Dar na miji jirani yote yanaingia katikati ya mji. Mheshimiwa angefikiria vile vile akisha jenga hizo flyover na magari yakapita bila foleni ndefu kuingia mjini yataenda kupaki wapi?
Kwa mawazo yangu mepesi lingetafutwa suluhisho la muda mrefu kwa "kuwalazimisha kwa kupenda" wenye magari kutoingia na magari katikati ya jiji. Hii inaweza kufanyika kwa kuweka usafiri wa uhakika kutoka nje ya mji na kuweka parking salama za magari nje ya mji ambako usafiri huo wa uhakika utakuwa unaanzia. Kwa mfano, stendi ya mabasi ya ubungo inaweza kuacha iwe parking ya magari na kuwe na train ya kwenda kasi kutoka Ubungo kuingia mjini. Watu wanapaki magari pale na kuingia kwenye treni. Akimaliza kazi anapanda treni mpaka ubungo na kuchukua gari lake huyo kuelekea kibaha, mbezi, mwenge, n.k. Kunaweza kuwa na vituo vy treni kadhaa hapo mjini. Kwa njia hii watu hawataona haja ya kuingia na magari mjini kwani hii mbali ya kusaidia kupunguza matumizi ya mafuta, itasaidia kuokoa muda ambao mtu angetumia kwenye trafic jam.
Ni mawazo yangu ambayo yako open for criticism.
Tiba
Anataka kuanza kujenga hoja ya kampeni asiyowezakuitekeleza!.
Tiba, mawazo mazuri. Nadhani pia ingesaidia kama jiji lingeweka congestion charge kwa magari madogo kuingia sehemu fulani za mji kiasi kwamba yale magari ya ulazima tu ndio yaruhusiwe e.g utility vans, taxis. Congestion charge iwe juu kidogo.
Pia misafara ya mawaziri isisimamishe magari mengine, kwani wao nani?