Rais Kikwete aagiza flyovers zijengwe Dar haraka sana

JK na mkwara wa flyovers!
Mkuu wa nchi Rais JK,amechimba biti kwa wahusika kuwa sasa umefika wakati wa kuwa na barabara zinazopita juu kwa juu (flyovers) kupunguza misongamano ya magari katika Jiji la Dar es Salaam.

Akichimba biti hilo ndani ya ukumbi wa Karimjee ..huku tukiwa kwenye safari ya kuelekea uchaguzi mkuu...JK alisema ''Hili la flyovers lipewe kipaumbele ili tupunguze msongamano wa magari katika Dar es Salaam...tusipofanya hili jiji hili litakuwa halipitiki katika muda wa miaka mitano, ama hata katika miaka miwili ama mitatu ijayo,''

Rais Kikwete pia ameagiza wataalamu wa mipangomiji kuanza kupunguza maeneo yasiyopimwa katika jiji hilo kwa kuwa ni asilimia 30 ya Jiji la Dar es Salaam ambako watu wamejenga katika maeneo yaliyopimwa.

Amesema, Jiji la Dar es Salaam haliwezi kuendelea kupanuka bila kupangiliwa.

''Hatuwezi kuendelea namna hii na mji unaopanuka namna hii. Hili ni jambo zito, kubwa linalohitaji umakini wa haraka kutatuliwa. Ndio maana kipindupindu hakiishi katika mji huu.'' Amesema.
sorce:darhotwire
 
Kwanza angeanza kwa kutoruhusu ujenzi wa zaidi ya Ghorofa nne maeneo ya Kariakoo, na hiyo CBD, kwani uwezo wa miundo mbinu yetu ni mdogo kuwezesha idadi ya watu na magari kuingia sehemu hizo.
Jingine kwanini jambo hili kaenda liongelea kama Mwenyekiti wa CCm, na asili tole tamko kama Raisi.
 
Nyani-Abiziani,
Town Planners walishatoa mapendekezo tangu mwishoni mwa miaka ya Tisini issue ipo kwenye utekelezaji tu.Jiulize izo flyovers unataka zitoke wapi na ziishie wapi?je tuna feeder roads zakutosha ili kupokea ayo magari yatakokua yanatoka kwenye flyovers?au yatakua yanakaa huko huko juu?

Alles umenichekesha kweli; hivi mnafikiria lengo la flyover ni kuzuia msongamano? no sir. Wanataka mahali ambapo wananchi wanaweza kupigia picha na kuonesha kuwa Tanzania nayo ni kama majuu! Kama ajali zinatokea kwa kuchomekeana humuhumu chini huku juu kwa juu itanyesha miili ya watu!
 
Hapa umetukumbusha daraja la manzese.
 
Alles umenichekesha kweli; hivi mnafikiria lengo la flyover ni kuzuia msongamano? no sir. Wanataka mahali ambapo wananchi wanaweza kupigia picha na kuonesha kuwa Tanzania nayo ni kama majuu! Kama ajali zinatokea kwa kuchomekeana humuhumu chini huku juu kwa juu itanyesha miili ya watu!

The tale of the beautiful of the beggars! Kabla ya Rais Kikwete kutoa kauli siku chache kabla nilitoa kauli kuhusu hoja za SUMARTA na DART kuhusu foleni:

"Nakubaliana na ukweli kwamba foleni katika mkoa wa Dar es salaam ni tatizo lenye athari za kiuchumi ambapo taifa hupoteza takribani bilioni nne kila saa; lakini serikali izingatie kwamba mikakati mipana inapaswa kutekelezwa kukabiliana na hali hii badala ya kufikiri kwamba uwekaji wa makampuni makubwa ya kuendesha mabasi yaendayo kasi ndio suluhisho kuu. Fikra za namna hii za kuongoza kwa dharura ndio ambazo zilitumika kutekeleza mpango wa njia tatu katika baadhi ya maeneo mfumo ambao athari zake zinaendelea kuonekana mpaka sasa. Inashangaza jiji pana lenye takribani milioni nne lenye magari binafsi laki moja tu kuwa na foleni kwa kiwango cha Dar es salaam. Hii ni dalili kwamba tatizo letu la msingi ni udhaifu katika mipango miji. Sasa badala ya kushughulikia matokeo ni muhimu kutekeleza sera zenye kukabiliana na vyanzo vya matatizo.

Hivyo mkazo uwekwe katika kutekeleza sera zenye kupanua jiji kuelekea pembezoni (satellite towns) lakini pia kuheshimu ramani za muda mrefu badala ya kuendelea na mtindo wa ujenzi holela ambao unachochea pia migogoro ya ardhi na kuliingiza taifa katika kubeba mzigo mkubwa wa fidia za mara kwa mara. Pia serikali iwekeze katika barabara za kuchuja magari (filter roads) ili kupunguza msongamano kwenye barabara kuu. Mathalani, hapa jimboni Ubungo haiingii akilini kwamba mtu ambaye yuko Mbezi Loius akitaka kwenda Mbezi Beach upande wa Jimbo la Kawe analazimika kwenda na gari mpaka Ubungo mataa halafu Mwenge ndio anarudi Mbezi. Wakati kama barabara ya kutoka Mbezi Louis kwenda Mbezi Beach moja kwa moja kupitia Goba ingejengwa kwa haraka kiwango cha lami ingepunguza msongamano wa magari. Hivyo hivyo, mwendesha gari kutoka Kibamba kwenda Tegeta analazimika kupita njia hiyo hiyo na kuongeza msongamano wakati angeweza kukatishia Mpiji Magoe au maeneo mengine kama njia hizo zingelindwa dhidi ya uuzaji holela wa viwanja na pia barabara zake zingewekwa lami.

Wakati serikali ya CCM inazungumza kujenga barabara za hewani (flying overs) na mabasi na treni ziendazo kasi (rapid transport), serikali hiyo hiyo inashindwa kuweka mazingira ya huduma za msingi za kijamii kwa wananchi. Hii ni serikali inayojiita masikini inayoendeshwa kwa kuomba omba lakini inataka kuvunja rekodi za kimataifa katika ujenzi na manunuzi kuanzia bungeni, ndege ya rais, rada, majengo pacha ya Benki Kuu, nyumba ya gavana na sasa usafiri katika mkoa wa Dar es salaam.

Hali hii ya kushindwa kutambua vipaumbele kama taifa ndio inafanya kodi za wananchi wa vijijini kutokurejeshwa kuhakikisha maendeleo ya uwiano na hivyo kujenga matabaka yanayosababisha watanzania wengi zaidi kukimbilia Dar es salaam na kusababisha msongamano kuzidi kuongezeka. Kwa hiyo kuleta wawekezaji toka nje, na kuleta mabasi yaendayo kasi havitaweza kuondoa msongamano kama vyanzo vya msingi vya msongamano havitashughulikiwa kisera, kimfumo na kiuongozi.

Mwelekeo mzima wa mradi huu unadhihirisha udhaifu katika mfumo wetu wa utawala ambao serikali kuu na mamlaka zake inahodhi michakato yote ya msingi hata ile ambayo halmashauri zilipaswa kushirikishwa na kuchukua nafasi ya kuwa mstari wa mbele katika kutoa mwelekeo kama suala hili la usafiri katika mkoa wa Dar es salaam na manispaa zake. Lakini ni ishara pia ya uongozi wa muda mrefu wa CCM unaanzisha mipango tofauti tofauti inayoshindwa baada ya muda mfupi. Kwa hali hii badala ya CCM kusherehekea itumie fursa hii kuwaeleza watanzania ni nini kimefilisi kampuni ya Usafirishaji Dar es salaam (UDA) na pia waeleze wazi ilipokwenda michango iliyotolewa na wananchi mkoani Dar es salaam kwa ajili ya mradi wa mabasi ya wanafunzi ambao fedha zake inatuhumiwa kuwa zimeishia mikononi mwa vigogo wa UVCCM wakati walengwa wanaendelea kupata adha ya usafiri.

Katika mazingira haya ni muhimu kuhamasisha mabadiliko ya kweli katika taifa kwa wananchi kuchagua viongozi mbadala. Mwaka 2005 Mkoa wa Dar es salaam uliwaangusha watanzania kwa kuwa pamoja na kuwa na wasomi wengi, wananchi wenye kufikiwa zaidi na vyombo vya habari na pia wananchi ambao wanaelezwa kuwa na elimu ya kuridisha ya uraia ukilinganisha na wa vijijini; lakini mkoa huu wabunge wake wote 7 ni CCM na madiwani wake wote wa kuchaguliwa na wa viti maalumu katika manispaa zote tatu ni CCM. Wananchi wa Dar es salaam wakiwemo wajanja wa Kinondoni wanafurahia hoja za wabunge wa upinzani kama Dr Wilbroad Slaa bungeni ama kazi ya madiwani wa upinzani wanaongoza halmashauri kama kule Karatu lakini hawajui kwamba viongozi hawa mbadala wametokana na wenzao wa vijijini ambao waliamua kuunganisha nguvu katika uchaguzi uliopita kwa kupiga kura kwa wingi lakini pia kushiriki kulinda ushindi wao mpaka hatua ya mwisho. Natarajia mafunzo haya yatawawezesha kuwaunganisha wananchi wa Jimbo la Ubungo kurekebisha kasoro hizo na kusimamia mabadiliko kwani katika miji mingi mikubwa ya Afrika wananchi wanaunga mkono vyama mbadala."

Maneno haya ambayo baadhi yalinukuliwa na vyombo vya habari yamo kwenye hotuba yangu hii: http://mnyika.blogspot.com/2010/01/hotuba-yangu-jimboni-ubungo-nikifungua.html

Nimepata taarifa za ziada kuhusu yanayojiri nyuma ya pazia kuhusu mradi wa mabasi yanaendayo kasi, vikiwemo vikwazo toka juu vinavyoikabili DART, natumaini viongiozi wangu watalitolea kauli wakati muafaka.

Hili la JK fly overs linahitaji kupewa majibu muafaka kwa kumbushia kauli zake 2005, Kauli za Lowassa akiwa PM nk. Tuendelee kujadili

JJ
 
this is just a politician talking to save his skin in the next elections. if he was serious about flyovers, why has he not done since he became president?
 
Then, hao maofisa wa mipango miji wanafanya kazi gani sasa? unaweza kukuta wengine hata wamepanga manzese,na kwa nini hadi wapate amri kutoja juu? Tukija kwenye swala la flyovers ni kwamba linatekelezeka au ni kampeni tu? isije ikawa kama ile ya maisha bora.

Nyani-Abiziani,
Town Planners walishatoa mapendekezo tangu mwishoni mwa miaka ya Tisini issue ipo kwenye utekelezaji tu.Jiulize izo flyovers unataka zitoke wapi na ziishie wapi?je tuna feeder roads zakutosha ili kupokea ayo magari yatakokua yanatoka kwenye flyovers?au yatakua yanakaa huko huko juu?

Dar current inaitaji access(feeder)roads za kutosha, pili zitengenezwe roads mpya za kuunganisha maeneo yanayokua, mfano roads ya kutoka Bunju-mbezi ya Morogoro road to Pugu.Ubungo, kariakoo kupitia kigogo-kupitia club ya Yanga(ii walishaanza kuijenga sijui itaisha lini). Mwisho walishapendekeza since 1980s Dar-CDB ipunguzwe kwa kuanzisha nyingine nje ya Dar na office nyingine zijengwe huko.Matokea yako ni kinyume DAR-CDB kuanzia kariakoo watu wanazidi kutenga vikwangua anga na officeza serikali zinasogezwa kutoka ghorofa moja kwenye lingine na hawahamii nje ya mji kama planners walivyopendekeza, ili kupunguza watu kuelekea Posta kila kukicha.Kufikiria fryover kwa sasa ni ujinga na, kama wameshindwa kujenga simple access roads wataweza fryovers? Kauli ya JK ni too politics.nawaonea huruma mnaomwamini..wahenga hawakukosea waliposema "wajinga ndio waliwao"

Mwisho, Town planner uyu unayemlalamikia mshahara wake ni TSGD=322,000/= na wengine ni TSGE=408,560. Kwa kipato hiki unategemea akapange wapi kama sio Manzese, Msasani bonge la mpunga, Buguruni, viungunguti,Mbagala mgeni nani au akijitaidi kigogo.Nimalizie kwa kusema suala la fryovers alitekelezeki, kwenye ground kuna mambo yanatakiwa kujengwa kabla ya kufukiria fryovers.[/QUOTE]

Natoka nje ya mada.... Pamoja na kutoa mawazo mazuri ningeomba sana tuzingatia kiswahili fasaha na tusiandike kama watu wa elimu ya ngumbaru. Wote tuna jukumu la kukiendeleza kiswahili.....
 
Mkuu Mnyika naona labda wewe ndiye uliyekuwa wa kwanza kuingia mkenge na rai amekufuata. Sina hakika kama kweli nyie wanasiasa mna know how ya kusema wapi, lini na vipi barabara ijengwe. Sina hakika kama kweli rais anajua nini anachosema, na sina uhakika hata wewe mkuu Mnyika kama kweli uko serious na suggestion ya kuondoa msongamano wa magari Dar kwa kujenga barabara toka Mbezi Louis had Mbezi beach.

Kwa layman knowledge yangu ni kuwa msongamano wa magari sababu yake moja ni concetration ya watu Dar, kwa nini lisianze kuangaliwa hilo? Kwanini kinachofuatwa na watu Dar kisiwepo Dodoma Arusha au Morogoro? Tangu mkoloni atuachie city kwa jali ya wakazi laki 5 hatujajenga city yoyote ya maana at least hata ya watu laki mbili. Kila kitu tunaweka Dar, kazi, shule, hospitali kila kitu Dar, Kama tukizingatia kuweka even development matatizo kama haya hayatakuwepo tena.

Otherwise tutajenga flyovers 2, watu wataongezeka zaidi tutataka kuongeza nyingine tena na tena na tena. Tutajenga barabara ya mbezi louis hadi beach, tutakuja kumbuka kuwa tumesahau ya kutoka Rangi 3 hadi Vijibweni.

My point ni kuwa siasa wapige wanasiasa, mipango miji wafanye kazi yao.
 
The tale of the beautiful of the beggars! Kabla ya Rais Kikwete kutoa kauli siku chache kabla nilitoa kauli kuhusu hoja za SUMARTA na DART kuhusu foleni:

"Nakubaliana na ukweli kwamba foleni katika mkoa wa Dar es salaam ni tatizo lenye athari za kiuchumi ambapo taifa hupoteza takribani bilioni nne kila saa; lakini serikali izingatie kwamba mikakati mipana inapaswa kutekelezwa kukabiliana na hali hii badala ya kufikiri kwamba uwekaji wa makampuni makubwa ya kuendesha mabasi yaendayo kasi ndio suluhisho kuu. Fikra za namna hii za kuongoza kwa dharura ndio ambazo zilitumika kutekeleza mpango wa njia tatu katika baadhi ya maeneo mfumo ambao athari zake zinaendelea kuonekana mpaka sasa. Inashangaza jiji pana lenye takribani milioni nne lenye magari binafsi laki moja tu kuwa na foleni kwa kiwango cha Dar es salaam. Hii ni dalili kwamba tatizo letu la msingi ni udhaifu katika mipango miji. Sasa badala ya kushughulikia matokeo ni muhimu kutekeleza sera zenye kukabiliana na vyanzo vya matatizo.

Hivyo mkazo uwekwe katika kutekeleza sera zenye kupanua jiji kuelekea pembezoni (satellite towns) lakini pia kuheshimu ramani za muda mrefu badala ya kuendelea na mtindo wa ujenzi holela ambao unachochea pia migogoro ya ardhi na kuliingiza taifa katika kubeba mzigo mkubwa wa fidia za mara kwa mara. Pia serikali iwekeze katika barabara za kuchuja magari (filter roads) ili kupunguza msongamano kwenye barabara kuu. Mathalani, hapa jimboni Ubungo haiingii akilini kwamba mtu ambaye yuko Mbezi Loius akitaka kwenda Mbezi Beach upande wa Jimbo la Kawe analazimika kwenda na gari mpaka Ubungo mataa halafu Mwenge ndio anarudi Mbezi. Wakati kama barabara ya kutoka Mbezi Louis kwenda Mbezi Beach moja kwa moja kupitia Goba ingejengwa kwa haraka kiwango cha lami ingepunguza msongamano wa magari. Hivyo hivyo, mwendesha gari kutoka Kibamba kwenda Tegeta analazimika kupita njia hiyo hiyo na kuongeza msongamano wakati angeweza kukatishia Mpiji Magoe au maeneo mengine kama njia hizo zingelindwa dhidi ya uuzaji holela wa viwanja na pia barabara zake zingewekwa lami.

Wakati serikali ya CCM inazungumza kujenga barabara za hewani (flying overs) na mabasi na treni ziendazo kasi (rapid transport), serikali hiyo hiyo inashindwa kuweka mazingira ya huduma za msingi za kijamii kwa wananchi. Hii ni serikali inayojiita masikini inayoendeshwa kwa kuomba omba lakini inataka kuvunja rekodi za kimataifa katika ujenzi na manunuzi kuanzia bungeni, ndege ya rais, rada, majengo pacha ya Benki Kuu, nyumba ya gavana na sasa usafiri katika mkoa wa Dar es salaam.

Hali hii ya kushindwa kutambua vipaumbele kama taifa ndio inafanya kodi za wananchi wa vijijini kutokurejeshwa kuhakikisha maendeleo ya uwiano na hivyo kujenga matabaka yanayosababisha watanzania wengi zaidi kukimbilia Dar es salaam na kusababisha msongamano kuzidi kuongezeka. Kwa hiyo kuleta wawekezaji toka nje, na kuleta mabasi yaendayo kasi havitaweza kuondoa msongamano kama vyanzo vya msingi vya msongamano havitashughulikiwa kisera, kimfumo na kiuongozi.

Mwelekeo mzima wa mradi huu unadhihirisha udhaifu katika mfumo wetu wa utawala ambao serikali kuu na mamlaka zake inahodhi michakato yote ya msingi hata ile ambayo halmashauri zilipaswa kushirikishwa na kuchukua nafasi ya kuwa mstari wa mbele katika kutoa mwelekeo kama suala hili la usafiri katika mkoa wa Dar es salaam na manispaa zake. Lakini ni ishara pia ya uongozi wa muda mrefu wa CCM unaanzisha mipango tofauti tofauti inayoshindwa baada ya muda mfupi. Kwa hali hii badala ya CCM kusherehekea itumie fursa hii kuwaeleza watanzania ni nini kimefilisi kampuni ya Usafirishaji Dar es salaam (UDA) na pia waeleze wazi ilipokwenda michango iliyotolewa na wananchi mkoani Dar es salaam kwa ajili ya mradi wa mabasi ya wanafunzi ambao fedha zake inatuhumiwa kuwa zimeishia mikononi mwa vigogo wa UVCCM wakati walengwa wanaendelea kupata adha ya usafiri.

Katika mazingira haya ni muhimu kuhamasisha mabadiliko ya kweli katika taifa kwa wananchi kuchagua viongozi mbadala. Mwaka 2005 Mkoa wa Dar es salaam uliwaangusha watanzania kwa kuwa pamoja na kuwa na wasomi wengi, wananchi wenye kufikiwa zaidi na vyombo vya habari na pia wananchi ambao wanaelezwa kuwa na elimu ya kuridisha ya uraia ukilinganisha na wa vijijini; lakini mkoa huu wabunge wake wote 7 ni CCM na madiwani wake wote wa kuchaguliwa na wa viti maalumu katika manispaa zote tatu ni CCM. Wananchi wa Dar es salaam wakiwemo wajanja wa Kinondoni wanafurahia hoja za wabunge wa upinzani kama Dr Wilbroad Slaa bungeni ama kazi ya madiwani wa upinzani wanaongoza halmashauri kama kule Karatu lakini hawajui kwamba viongozi hawa mbadala wametokana na wenzao wa vijijini ambao waliamua kuunganisha nguvu katika uchaguzi uliopita kwa kupiga kura kwa wingi lakini pia kushiriki kulinda ushindi wao mpaka hatua ya mwisho. Natarajia mafunzo haya yatawawezesha kuwaunganisha wananchi wa Jimbo la Ubungo kurekebisha kasoro hizo na kusimamia mabadiliko kwani katika miji mingi mikubwa ya Afrika wananchi wanaunga mkono vyama mbadala."

Maneno haya ambayo baadhi yalinukuliwa na vyombo vya habari yamo kwenye hotuba yangu hii: http://mnyika.blogspot.com/2010/01/hotuba-yangu-jimboni-ubungo-nikifungua.html

Nimepata taarifa za ziada kuhusu yanayojiri nyuma ya pazia kuhusu mradi wa mabasi yanaendayo kasi, vikiwemo vikwazo toka juu vinavyoikabili DART, natumaini viongiozi wangu watalitolea kauli wakati muafaka.

Hili la JK fly overs linahitaji kupewa majibu muafaka kwa kumbushia kauli zake 2005, Kauli za Lowassa akiwa PM nk. Tuendelee kujadili

JJ

Superb.... Excellent!! Hizi ndio comments za kitaalam... Keep it up
 
Mkuu Mnyika naona labda wewe ndiye uliyekuwa wa kwanza kuingia mkenge na rai amekufuata. Sina hakika kama kweli nyie wanasiasa mna know how ya kusema wapi, lini na vipi barabara ijengwe. Sina hakika kama kweli rais anajua nini anachosema, na sina uhakika hata wewe mkuu Mnyika kama kweli uko serious na suggestion ya kuondoa msongamano wa magari Dar kwa kujenga barabara toka Mbezi Louis had Mbezi beach.

Kwa layman knowledge yangu ni kuwa msongamano wa magari sababu yake moja ni concetration ya watu Dar, kwa nini lisianze kuangaliwa hilo? Kwanini kinachofuatwa na watu Dar kisiwepo Dodoma Arusha au Morogoro? Tangu mkoloni atuachie city kwa jali ya wakazi laki 5 hatujajenga city yoyote ya maana at least hata ya watu laki mbili. Kila kitu tunaweka Dar, kazi, shule, hospitali kila kitu Dar, Kama tukizingatia kuweka even development matatizo kama haya hayatakuwepo tena.

Otherwise tutajenga flyovers 2, watu wataongezeka zaidi tutataka kuongeza nyingine tena na tena na tena. Tutajenga barabara ya mbezi louis hadi beach, tutakuja kumbuka kuwa tumesahau ya kutoka Rangi 3 hadi Vijibweni.

My point ni kuwa siasa wapige wanasiasa, mipango miji wafanye kazi yao.

Naomba usome tena na tena maoni ya Mnyika. Ametoa solution ya hii uliyoiita concetration ya watu. By the way mbona yapo majiji yenye watu wengi kuliko Dar lakini foleni za magari hazitishi?
 
ndiyo tatizo la kuwa na rais mwenye ya ilim ya madrasa tu bila elimu dunia akilini,
anakuwa anaishi ka pepo mchafu tu, hana tofauti na jini, kwa kuwa pepo huwa halina kumbu kumbu, sasa ameshahau kuwa ailiyo ahidi hayajakamilika hata kwa 1/4 ya yote. kazi kwenda USA tu kupiga picha na wana muziki wa Boyz II Men na kuoa tubinti tudogo tudogo tw kipemba huu ni uhuni, Nawaasa Watanzania wenzangu ya kwamba kujikomboa kwetu ni kuwa na uwezo mkubwa wa kusoma alama za nyakati, hapo hakuna uhalisia ni kufungua kinywa cha kampeni mpya
 
sasa mkuu unnashauri tuje na solution gani??
 
And the Lord declared "let there be flyover all over Dar Es Salaam like the ones in New York" and people bow down to the mighty voice and made it happen!
 
ndiyo tatizo la kuwa na rais mwenye ya ilim ya madrasa tu bila elimu dunia akilini,
anakuwa anaishi ka pepo mchafu tu, hana tofauti na jini, kwa kuwa pepo huwa halina kumbu kumbu, sasa ameshahau kuwa ailiyo ahidi hayajakamilika hata kwa 1/4 ya yote. kazi kwenda USA tu kupiga picha na wana muziki wa Boyz II Men na kuoa tubinti tudogo tudogo tw kipemba huu ni uhuni, Nawaasa Watanzania wenzangu ya kwamba kujikomboa kwetu ni kuwa na uwezo mkubwa wa kusoma alama za nyakati, hapo hakuna uhalisia ni kufungua kinywa cha kampeni mpya

Anyisile,

Ndugu yangu mbona mdoni na mbaguzi na mduni wa mawazo kiasi hiki? Jenga hoja inayojengeka na kupimika na si kuongea kama zuzu!

Kama unaidharau Ilmu ya Madrass kuwa ni mbofu mbofu, sasa weye Ilmu yako ya SandeSkuli na Kipaimara na hata Krusedi mbona zinakuvua nguo hadharani na kukufanya uonekane weye wala hufanani na mafundisho ya yule aliyeitwa Masihi?
 
Mkuu Kigogo, huyu jamaa ni msanii na mwaka huu kwa kuwa anataka Watanzania wampe KULA atatoa kauli zake nyingi za kisanii ambazo haziwezi kutekelezeka kabisa. Anadhani hizi zitajiotea kama uyoga au mchicha unavyoota bila hata ya kuwa na planning ya kujenga hizi flyovers na hiyo financing itatoka wapi. Kauli zake kwa kweli zinakatisha tamaa sana maana zinaonyesha tuna kiongozi ambaye hata uwezo wake wa kutafakari mambo ni mdogo sana.
BAK umeniacha hoi hapo kwenye msisitizo. Ila ndiyo hivyo tena rungu tumeshampatia tuangalie kwa macho tu sasa kama atalitumia kujipiga nalo, kutupiga sisi au kumpiga adui yetu (Umasikini, ujinga na maradhi). Ila naona kama limeelekezewa kwetu sasa tuwe macho na actions zake, kabla hajalivugumiza (vuguvugu) kama tunavyoita kule kwetu basi tujue cha kufanya
 
nina kamp[uni ya ku design na kujenga....mnikumbuke kwenye ufalme huu unaokuja.
 
Anyisile,

Ndugu yangu mbona mdoni na mbaguzi na mduni wa mawazo kiasi hiki? Jenga hoja inayojengeka na kupimika na si kuongea kama zuzu!

Kama unaidharau Ilmu ya Madrass kuwa ni mbofu mbofu, sasa weye Ilmu yako ya SandeSkuli na Kipaimara na hata Krusedi mbona zinakuvua nguo hadharani na kukufanya uonekane weye wala hufanani na mafundisho ya yule aliyeitwa Masihi?
mkuu unamaanisha nini hapa!!
 
sina uhakika na uelewa wako ni wa kiwango gani maana naona unaleta mashitaka jambo la mhimu weye kama umeguswa na hoja polisi si wapo? lakini sababu ya kuanza kulumbana hapa hoja ni maagizo rais mwenye ilimu ya madrasa maana hata wa kuwadanganya hawaoni kutokana kuwa na upeo wake kuwa mdogo, harafu tambua kuwa kuna tofauti kubwa sande skuli na madrasa
Sandeskuli = unafundishwa na kuulizwa maswali juu ya kile ulichofundishwa
hatukaririshwi kwa lengo kuhifanyi juzuu nna ayaze, tunafundi
shwa ili uelewe kama hujaelewa unauliza maswali
Madrasa = unakaririshwa na hakuna kuuliza maswali fuata vile
unavyo karirishwa na maana unatakiwa kumuanzisha mtoto
asiyejua kusoma wala kuandika, kwa sababu sedhemu kubwa ya
ilimu ni kukariri
 
Back
Top Bottom