Rai ya Jenerali: Waziri mkuu asiye waziri mkuu, serikali iliyobinafsishwa - hatuendi kokote

Congratulation Jr. Ulimwengu!! Hivyo ndivyo nchi ilivyo kwa sasa.
Hilo liwe somo tosha kwa watumiao sanduku la kura katika mtazamo hafifu. MUNGU BARIKI TANZANIA!!
 
ujue kuna zile nchi kama Thailand, indonesia, malaysia, Korea, nk wale siyo kwamba dili za hapa na pale hamna au ufisadi hamna, upo, ila wenzetu wanachofanya wana ufisadi ulio na nidhamu. nitafafanua kidogo hili

nchi zote zisizo za kimagharibi zina kitu kinaitwa patron-clients networks (yaani kiongozi anaweka watu anaowaona yuko salama nao ili waendeshe serikali bila ya kua na mikwaruzo wala uoga wa kukosolewa au hata kuondolewa kwenye uongozi na hawa wenzake-mfano spika makinda ni client na Jk ni patron wake kutokana na ufinyu wa demokrasia hii inabidi iwepo)..sasa hii patron-client network ili iwe na ufanisi inabidi iwe imehodhiwa na nguvu kubwa ya serikali kuu na wakuu wake (centralized and top-down approach) hapa ufisadi utakua una mpango, utakua unafanywa na wachache sana kwa sababu lazima upate ruksa ya wakuu wako na hapa kutakua na hali ya kuridhisha katika uongozi na maendeleo kiujumla mfano wa hawa niliowataja wa malaysia, thailand vietnam nk

Hapa tanzania na nchi nyingine kama hizi tuna patron-client network isiyohodhiwa kati ,(yetu ni decentralized) ambayo ni loose, bottom-up approach ikiwa bila ya nidhamu-hapa sasa kila wizara, kila ofisa wa serikali, kila mkuu wa wilaya, kata anaweza kutafuna hela ya nchi au kutumia madaraka yake vibaya kupata hiki au kile bila ya wenzake kujua, au hata wakijua atawashirikisha wakubwa zake kwa sababu kila mfanyakzi wa serikali anaruhusiwa kuiba katika ngazi zote, hamna mamlaka kuu ya kati inayohamua nani, nini, wapi, na ngapi ziibiwe hapa ni iba unavyoweza, washirikishe wenzako kidogo na hii inaleta hasara kubwa, na maendeleo finyu.

fedha za umma zinapotea kushoto, kulia, chini, juu, ndani, nje, usiku, mchana, yaani vurugu tupu
 
'Waziri mkuu asiye waziri mkuu...'

'Kiongozi wa nchi mtoro'

Asante sana G. Ulimwengu.
 
jenerali.jpg


Jenerali Ulimwengu



Ndiyo maana hawezi kuwaambia mawaziri wanaotoa kauli za kijinga "Shut up!," hawezi kumwambia bosi wake awaondoe, na imedhihirika kwamba huko maofisini mwao wanafanya wanavyotaka. Waziri anaweza akasema hadharani kwamba naibu wake anafanya mambo bila kumwambia, anakwenda kutafuta wakandarasi wake bila kumpa taarifa, na kadhalika, hali inayodhihirisha ubinafsishaji wa ofisi za serikali yetu.

Ivunjwe serikali,iundewe serikali ya mpito,kuelekea katiba mpya.Kwani wametema kabisa sifa za uongozi na hakuna njia ya mkato kuinusuru serikali mahututi.Tusitegemee miujiza miaka mitatu ni mingi muno kwa serikali ilio ICU Muhimbili.Hongera Ulimwengu lakini watakutafutia visa safari hii usije ukajikuta uhamishoni.
 
Nimekuwa nikifuatilia article za huyu mkuu kwa takribani miaka kumi na mbili sasa.
Vile vile,nimehudhuria public talks nyingi ambazo huyu bwana huwa mmoja wa wasemaji wakuu ama wachangiaji.
Mara zote amekuwa anatema cheche..lakini sioni mabadiliko yoyote kwa upande wa watawala.
Hata kama hawataki kuchukua hatua, makala ama hata matamko ya huyu Nguli yamekuwa na yanaendelea kutengeneza kizazi cha 'waasi' dhidi ya watawala.Mathalani, tabia ya 'uasi' inayoonyeshwa mara kwa mara na wanafunzi wa UDSM ni mmoja ya matokeo ya kazi zake maana huyu jamaa huwa haipiti muda bila kwenda kupandikiza sumu pale.Ni kweli watawala hawataki kuchukua hatua,lakini tayari wanakumbana na athari za kazi zake kila iitwapo leo na muda si mrefu watatambua kosa walilolifanya kwa upuuzi wa kupuuza mawazo yake.
 
nimewahi kumuona mara kadhaa waziri mkubwa akibubujikwa na machozi tena bungeni. Ndo maana mawaziri wake wanafanya yaliyo zaidi ya hayo
 
Mzee wangu jenerali naomba nikupe pongezi zangu kwa kutumia kalamu yako ipasavyo. Nchi hii tungekuwa na waandishi wa aina ya mzee Ulimwengu hakika watawala nchii hii wangekuwa welevu, wasikivu, wawajibikaji, wabunifu nk. Sina la zaidi la kusema mzee wangu ila naomba uendele kutumia kalamu vizuri kuwakumbusha wa mabwanyenye pale magogoni... ni hatari sana kuwa na mkuu mtoro, waziri mkuu kibogoyo tena kivuli. Ahsante.
 
Very correct Generali. Haileti maana kuwa na nafasi zisizo kuwa na nafasi ( Power). Ni sawa na kuwa na "teethless bull of dog" ukiwa na malengo yaleyale ya kufuga mbwa kuimarisha ulinzi. It's shame to our rich poor country.
 
jeneral hakika utakumbukwa na jamii ya watanzania wote vizaz na vizaz vijavyo kwa nasaha zako za waz na zilizojaa hekima, busara na maonyo meng. nakuheshim sana mzee wetu.
 
Namuaminia mzee huyu nimemsoma sana makala zake wakati ule RAI enzi ya Mzee Mkapa.Kama ni kupiga kelele Mzee huyu jamani amepiga kelele siku nyingi sana,alikuwa anatuhabarisha enzi hizo za KILA MTU NA KAMUHOGO KAKE leo hii nimeshamiliza chuo miaka mitatu iliyopita kale kamuhogo kake kameshakuwa KILA MTU NA LIMUHOGO LAKE HUKO SERIKALINI.

Ila ili la Waziri Mkuu mimi naona kama anavyosema ni Someone's attitude or behaviour can be described as schizophrenic when they seem to have very different opinions or purposes at different times.

Hivyo kwa cheo hicho hicho cha waziri Mkuu Edward Moring Sokoine alitenda tofauti na wenzie.Hivyo tufike sehemu tujue pamoja na mapungufu ya katiba yetu lakini tuna tatizo la watu wanaoteuliwa kuwa mawairi wakuu [Ebu jaribuni iyo post apewe Mtu wa kabila la Mmasai, mkurya au mnyaturu. Kwa kuwa makabira haya yana kitu cha ziada nacho ni aggressiveness ya uthubutu!!!
 
Duuh... kumbe Nyerere alitunga tu cheo cha Waziri Mkuu halafu badae ndio kikachomekwa kwenye Katiba?

Kwa kweli hatuna haja ya kuwa na Waziri Mkuu, tayari tuna Marais watano, Billal, Hamad, Kikwete, Shein, Iddi.

Waziri Mkuu wa nini?
 
I can only add my thanks to Ulimwengu's majestic article. Bravo!
Wow,well said Jenerali .The article is well balanced and the guy is very articulate and open minded about this particular issue,we need more people like Jenerali who have guts to say as what has just been analysed and said by Ulimwengu
Big up J.U
 
GENERALI, mimi sina cha kuongeza kwenye busara zako kwamba '... [(1)]Taratibu, wananchi wameanza kutambua kwamba ufukara wao katika mazingira ya nchi tajiri sana unahusiana moja kwa moja na utajiri mkubwa wa watawala wao ambao wamekuwa wakitumia ofisi zao kujikusanyia mali haramu. Ofisi za serikali sasa zinajulikana kuwa ni mali binafsi za wale waliowekwa mle eti kuwatumikia wananchi. Kila anayepata nafasi hiyo ameiona kama ‘kihamba’ chake binafsi bila kujali maslahi ya nchi.... [na (2) mwanzo nafasi ya waziri mkuu haikuwepo, lakini] Baadaye ikaandikwa kwenye Katiba kwamba tutakuwa na waziri mkuu atakayekuwa kiongozi mkuu wa “shughuli za serikali bungeni” lakini tunashuhudia ukweli kwamba tunaye waziri mkuu asiye waziri mkuu....'

Mimi siyo gwiji kama wewe, ila nimeandika mara kadhaa kuhusiana na mambo hayo mawili. (a) PM wetu si WAZIRI MKUU. PM kapewa kazi za kufanya KIKATIBA (IBARA 52: (1) kusimamia shughuli za serikali, (2) kiongozi wa shughuli za serikali bungeni na (3) kufanya kazi atakazo pewa na RAIS). HIZO NI KAZI, sasa mamlaka ya kuzitekeleza yako wapi, HANA. PM hana mamlaka. (b) Wananchi wameanza kutambua kuwa sababu ya chakula kidogo kuja mezani kwa ajili ya wote ni WAPISHI (VIONGOZI) wanaolia jikoni. BABA YETU aliye MBINGUNI amenunua nyama kilo mbili, hizi ndizo raslimali za taifa, akawapatia wapishi, viongozi wetu, wapike tule wote. LAKINI wapishi wanalia jikoni kilo moja na nusu, nusu kilo iliyosalia ndo wanatuletea wote mezani: ni wazi chakula hakitatutosha. JIBU, ILI TUSHIBE, WOTE TUINGIE JIKONI kupika, au siyo?
jenerali.jpg


Jenerali Ulimwengu


236
25 Apr 2012

NCHI inapitia kipindi tete, kipindi ambacho kinashuhudia maswali mengi yakiruka kutoka kila upande huku kukiwa hakuna majibu yanayoeleweka. Halitakuwa kosa kuieleza hali hii kama hali ya mkanganyiko wa kitaifa.


Hivi majuzi niliandika makala katika mlolongo wa safu hii iliyosema kwamba “kupotea tulikopotea ni kupotea kukubwa.” Hali tuliyo nayo leo hainipi sababu ya kudhani kwamba hali yetu ya upotevu imebadilika sana, isipokuwa tu kwamba watu wengi zaidi wametambua kupotea kwetu ama wameamua kukupigia ukunga, kusema kwamba hata wao wameuona upotevu huo.


Hivi majuzi Rais Jakaya Kiwete ameiapisha tume yake aliyoiteua kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Napenda kuwapa pole wote walioteuliwa kwa kubebeshwa mzigo usiobebeka, kwa sababu ambazo nitazieleza leo na katika makala nyingine zijazo.


Kimsingi, ninachokiona mimi ( na wala siko peke yangu katika hili) ni kwamba tuko katika hali ya wananchi kufurukuta wakitaka mabadiliko makubwa yafanyike na yaonekane yakifanyika, lakini wakikabiliana na utawala uliokufa ganzi na kuduwaa, usijue la kufanya. Wananchi wanaumia, wanahenya, wanalalama, wanatafuta majibu, lakini wanakutana na maswali zaidi.


Kila mtu anajua kwamba hali ya maisha kiuchumi imekuwa ngumu sana, hususan katika maisha ya watu wa kawaida ambao wanaathirika vibaya kutokana na gharama za maisha kuzidi kupanda kutokana na bei za mafuta na chakula kupanda kila uchao. Hawaoni jitihada zo zote za serikali yao kupambana na hali hiyo, na badala yake wanashuhudia wakubwa ndani ya serikali wakizidi kujijengea ukwasi usiokuwa na maelezo.


Taratibu, wananchi wameanza kutambua kwamba ufukara wao katika mazingira ya nchi tajiri sana unahusiana moja kwa moja na utajiri mkubwa wa watawala wao ambao wamekuwa wakitumia ofisi zao kujikusanyia mali haramu. Ofisi za serikali sasa zinajulikana kuwa ni mali binafsi za wale waliowekwa mle eti kuwatumikia wananchi. Kila anayepata nafasi hiyo ameiona kama ‘kihamba’ chake binafsi bila kujali maslahi ya nchi.

Jambo moja linajidhihirisha kila mwaka, nalo ni kwamba kila siku uozo wa watawala wetu unazidi kujidhihirisha kwa kiasi kile kile ambacho tunadhihirisha udhaifu wa jamii yetu kukabiliana nao.


Kwa mfano, ofisi ya CAG ina maana gani kama kila mwaka inatoa taarifa inayoonyesha ubadhirifu katika idara za serikali lakini hakuna hatua yo yote inayochukuliwa kutokana na taarifa hizo?


Hakuna shaka kwamba ofisi ya CAG inaendeshwa kwa gharama kubwa na ziara za uchunguzi zinazofanywa na ofisi hiyo ndani na nje ya nchi ni mzigo mkubwa kwa bajeti ya nchi, na gharama hizi hatimaye zinabebwa na mlipa kodi. Kama tunajua kwamba taarifa za CAG hazina umuhimu kwa sababu hakuna dhamira ya kuzifanyia kazi, ni kwa nini ofisi hiyo isifungwe ili, angalau, tupunguze matumizi katika eneo hilo finyu?


Ofisi ya CAG ni kielelezo cha undumilakuwili wa utawala wetu. Sipati neon toshelezi la kuielezea hali hii, hivyo nalazimika kutumia neno la Kiingereza ‘schizophrenia,’ kwa maana ya kuwa na hulka mbili kwa wakati mmoja.


Kwa upande mmoja, tumerithi kutoka kwa wakoloni vyombo vya udhibiti ambavyo kazi yake ni kuhakikisha kwamba fedha za serikali hazitumiki hovyo, na kwamba pale zinapothibitika kutumika hovyo, wahusika wanachukuliwa hatua.


Lakini kwa upuuzi wetu hatuna dhamira ya kuchukua hatua pale inapobidi kwa sababu, kimsingi, ni kama tumekubaliana kwamba kila mtu atajinufaisha na ofisi yake, na kwa hiyo hakuna wa kumsema mwenzie.


Kwa maana hiyo, ingekuwa hatua ya mantiki kuifutilia mbali ofisi ya CAG, lakini hiyo ingetusababishia matatizo na wafadhili ambao wangetusuta kwa kufuta ofisi muhimu kama hiyo.


Hivyo, basi, tunayo ofisi ya CAG ambayo inatoa taarifa za kila mwaka ambazo hazifanyiwi kazi lakini hatuifuti kwa sababu wafadhili watatusuta. Watu wa ajabu!


Kuna jambo ambalo inawezekana watawala wetu wamekosa kuliona kutokana na ulafi wao na uwezo mdogo wa kufikiri unaotokana na ulafi huo. Kuruhusu ofisi ya CAG kutoa taarifa hizi kila mwaka zikionyesha wizi mkubwa wa fedha za wananchi bila kuzichukulia hatua ni njia mojawapo ya kujenga chuki ya wananchi dhidi ya serikali. Serikali inayofikiri ingechagua moja: ama kuzifanyia kazi taarifa hizo, ama kuzipiga marufuku kabisa na kuifuta ofisi ya CAG. Kwa sasa serikali yetu ni ‘schizophrenic.’


Kwangu mimi ni dhahiri kwamba siku wananchi watakapochukua hatua ya kuwaadabisha watawala wao, hoja mojawapo itakayowasukuma itakuwa ni taarifa za CAG zisizofanyiwa kazi.


Wiki iliyopita, bungeni, tumepata ushahidi mwingine kwamba watawala wetu wameshindwa kufanya kazi wanayotakiwa kuifanya. Baadhi yao wamebanwa na wabunge ambao bila shaka wamesukumwa na hasira za wananchi dhidi ya utawala wa ubadhirifu, wizi, kutokujali, na upuuzi. Katika sakata tulilolishuhudia bungeni, mojawapo ya sababu za malumbano yale ni taarifa za ubadhirifu serikalini (kutoka kwa CAG na kwingineko) ambazo serikali inaonekana kutokuwa na uwezo wa kuzishughulikia.


Kusema kweli, sura iliyojitokeza wiki hii iliyopita ni kwamba hatuna serikali inayofanya kazi kama serikali, bali tuna mkusanyiko wa maofisa waliokabidhiwa ofisi mbalimbali ambazo wanazitumia kadri wanavyojua wao na wala hawana udhibiti wa kati (central control).


Kila mmoja anasema anavyotaka, na katika kusema huko tunagundua kwamba katika ofisi yake anatenda anavyotaka pia, na hana ofisa mwandamizi wa kumwelekeza.


Walichotuonyesha watawala wetu wiki iliyopita ni taswira ya mkanganyiko mkubwa na wa kutia wasiwasi kwa ye yote anayethubutu kufikiri kidogo. Nchi hii haijakabiliwa na janga kubwa la ghafla katika miaka ya karibuni. Hatujakabiliwa na vita, mafuriko makubwa wala milipuko mikubwa ya magonjwa ya kutisha. Tuthubutu kujiuliza, je, iwapo tungekabiliwa na mojawapo ya majanga kama hayo, wale tuliowaona na kuwasikia bungeni Dodoma ndio tungewaamini kwamba wangetuongoza kuishinda dharura hiyo? Wale?


Nasema hapana. Tulichokishuhudia ni msamabaratiko ambao haujawahi kutokea katika historia ya nchi hii, serikali iliyoparaganyika, mawaziri wenye kauli za kitoto, wakuu wa serikali wasiokuwa na maamuzi, waziri mkuu kivuli asiyekuwa waziri mkuu, na mkuu wa nchi mtoro.


Hapo juu nimewapa pole wale walioteuliwa katika tume ya kuratibu maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hii ni kwa sababu namheshimu sana Joseph Warioba, kama ninavyowaheshimu baadhi ya wajumbe wa tume yake. Ningependa Warioba, ambaye tunajua sote ni mtu makini, afanikiwe nasi tupate manufaa.


Katika wiki zijazo nitaieleza ‘pole’ yangu, lakini nianze tu kwa kusema kwamba, katika kazi ambazo zinaweza kufanywa na tume hiyo katika muda mfupi iliyopewa ni kuangalia nafasi ya waziri mkuu asiye waziri mkuu, anayefanya kazi chini ya mkuu wa nchi asiyekuwapo, na anayewasimamia mawaziri asiowasimamia na wanaofanya shughuli zao binafsi.


Hivi tunaelezaje kwamba inafikia hatua ya wabunge (bila kujali vyama) wanachukua uamuzi wa kufanya jambo ambalo halijawahi kufanyika katika historia yetu, kama kusukuma hoja ya kutokuwa na imani na serikali kwa sababu mawaziri wachache wanaoonekana wameboronga hawataki kuondoka hata pale wanapotakiwa kufanya hivyo na chama chao bungeni, halafu waziri mkuu hana kauli na bosi wake yuko ughaibuni?


Kama nilivyosema kuhusu ofisi ya CAG asiye CAG, hivi kuna haja gani ya kuwa na waziri mkuu asiye waziri mkuu? Niliwahi kuijadili mada hii katika safu hii yapata miaka miwili iliyopita, nikieleza ‘schizophrenia’ ya ofisi hii.


Nilieleza kwamba katika mojawapo ya mazoezi ya kuunda serikali katika miaka ya sabini, Mwalimu Nyerere alimteua Edward Sokoine kuwa waziri mkuu, na akaulizwa na waandishi wa habari kwa nini anamteua waziri mkuu wakati Katiba haitaji ofisi hiyo.


Jibu la Mwalimu lilikuwa ni kwamba, kweli, Katiba haikusema kwamba kutakuwa na waziri mkuu, lakini pia Katiba haikutamka kwamba hakutakuwa na waziri mkuu, na kwamba waziri mkuu ni waziri kama mawaziri wengine isipokuwa yeye yuko kidogo juu ya wenziwe. ‘Schizophrenia.’


Baadaye ikaandikwa kwenye Katiba kwamba tutakuwa na waziri mkuu atakayekuwa kiongozi mkuu wa “shughuli za serikali bungeni” lakini tunashuhudia ukweli kwamba tunaye waziri mkuu asiye waziri mkuu.
Ndiyo maana hawezi kuwaambia mawaziri wanaotoa kauli za kijinga “Shut up!,” hawezi kumwambia bosi wake awaondoe, na imedhihirika kwamba huko maofisini mwao wanafanya wanavyotaka. Waziri anaweza akasema hadharani kwamba naibu wake anafanya mambo bila kumwambia, anakwenda kutafuta wakandarasi wake bila kumpa taarifa, na kadhalika, hali inayodhihirisha ubinafsishaji wa ofisi za serikali yetu.










 
Kabla ya bunge kujua kazi yake, ilikua naunga mkono hoja. Gazeti la rai kabla ya kununuliwa na fisadi lilikuwa linafanya hii kazi aliyoifanya cag zito na akina mwakyembe. Kwa kweli jenerali siku zote amefanya kazi yake. Endelea na mungu akupe nguvu. Sio kwamba hawajui mchango wako. Hila ujeuri na ufedhuli wao unaendelea kuua dhamila zao. Ni sisi wa kuwashughulikia.
 
Watawala wetu wamezama katika tope la utajiri na wanashindwa kunyanyua vichwa vyao ili waone kinachoendelea. Rai wanalalama kwa mateso wao hawasikii. Matope yameziba masikio yao. Wanaunda jeshi la kuwaua wao wenyewe bila kujijua. Wananyang'anya hata kile kidogo tulichonancho ili tuzidi kuichukia serikali yao. Wanakula nyama ya miili yao. Wanakunywa damu yao wenyewe. Wanachimba nyumba yao isiyo na madirisha

Tazama kashifa za mawaziri hwaw: Malima na SMG, Nundu na bandari, Ngeleja na umeme, Chami na TBS, wengine kama akina Mathayo, Nyalandu ....taja wengine. Mawziri hawa katika Serikali yo yote makini wagekuwa wamefukuzwa na kufikishwa mahakamani. Kwetu sisi wanaendelea kutanua na kufanya vituko.

Tujiulize. Hivi ni serikali gani ambayo mawaziri wanatajana jinsi wanavyoliibia taifa halafu Mkuu wa Kaya anaendelea kula na kunywa nao? Hivi hii ndiyo serikali makini na sikivu?" Hivi tutarajie katika utendaji huu wa serikali nchi yetu isonge mbele? Wananchi wanakata tamaa. Taifa la wananchi waliokata tamaa haliwezi kusitawi wala kuendelea kuwepo. Wananchi waliokata tamaa wanaweza kufanya cho chote kile. Hawna cha kupoteza zaidi ya minyororo ilifunga miguu yao.

Rais wetu fanya mabaliko sasa. Usingoje kesho. Kesho sisi na wewe tutakuwa tumechelewa. Siamini kama umeandaa mahali tofauti na Tanzania utakapoishi baada ya kumaliza kipindi chako cha urais. Hawa unaowaacha sasa wafanye madudu ndio watakuwa wa kwanza kupiga kelele usulubiwe. Hawa si watu wema kwako na kwetu. Ni wauaji.
Naona niishia hapa ......Lakini lazima Mawaziri hawa wafukuzwe siyo kubadilishwa kazi. Hawa si miungu. Hawa wanafitinisha serikali na wananchi.
 
"Nasema hapana. Tulichokishuhudia ni msamabaratiko ambao haujawahi kutokea katika historia ya nchi hii, serikali iliyoparaganyika, mawaziri wenye kauli za kitoto, wakuu wa serikali wasiokuwa na maamuzi, waziri mkuu kivuli asiyekuwa waziri mkuu, na mkuu wa nchi mtoro"

na kwamba waziri mkuu ni waziri kama mawaziri wengine isipokuwa yeye yuko kidogo juu ya wenziwe.

Baadaye ikaandikwa kwenye Katiba kwamba tutakuwa na waziri mkuu atakayekuwa kiongozi mkuu wa "shughuli za serikali bungeni" lakini tunashuhudia ukweli kwamba tunaye waziri mkuu asiye waziri mkuu.

Ndiyo maana hawezi kuwaambia mawaziri wanaotoa kauli za kijinga "Shut up!," hawezi kumwambia bosi wake awaondoe, na imedhihirika kwamba huko maofisini mwao wanafanya wanavyotaka. Waziri anaweza akasema hadharani kwamba naibu wake anafanya mambo bila kumwambia, anakwenda kutafuta wakandarasi wake bila kumpa taarifa, na kadhalika, hali inayodhihirisha ubinafsishaji wa ofisi za serikali yetu.

Pure Genius,
Legendary
JENERALI
:A S 41:
 
enough said mzee ulimwengu taifa la wachuuzi(merchants) hata viongozi wetu nao wachuuzi kila mtu mchuuzi mkuu wa kaya nae mtoro fujo kila mahali
 
Schizophrenia is a complex mental disorder that makes it difficult to:
  • Tell the difference between real and unreal experiences
  • Think logically
  • Have normal emotional responses,
  • Behave normally in social situations

    "I love JF"
 
Back
Top Bottom