Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,902
- 944
WAZIRI MHAGAMA: HATUPENDEZWI KUTUITA MAWAZIRI NI WANAFIKI
"Ninaamini kabisa hakuna Waziri yeyote ambaye amesimama hapa akajipiga kifua mbele akatetea ubadhirifu wa fedha hizo ambazo zimekuwa zikifanywa na watumishi wa Serikali. Ziko hatua zilizochukuliwa" - Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
"Mafanikio ya kazi nzuri ya Serikali inatokana na kazi nzuri iliyofanywa pia na Mawaziri katika udhibiti kama mnavyotuagiza waheshimiwa wabunge." - Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
"Lugha kwamba Mawaziri ni wanafiki, hatukai hapa na hatujakaa hapa tukiwa wanafiki katika kuisaidia Serikali" - Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)
“Mafanikio ya kazi nzuri ya Serikali hii yanatokana na kazi nzuri illiyofanywa pia na mawaziri katika udhibiti kama mnavyotuagiza [...] Lugha ya kwamba mawaziri ni wanafiki si kweli, hatujakaa hapa [bungeni] tukiwa wanafiki katika kuisaidia hii serikali yetu.” – Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama