Tanzania Njema Yaja
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 3,042
- 2,414
Mkuu mawasiliano ya sms si mapya. Kutuma sms si dhambi ya kumfukuza mtu, hata kama uko nje ya mawasiliano rasmi. Siku hizi ofisi zina Whatsapp Group ambazo wanatumiana matangazo na taarifa mbalimbali, sio rasmi lakini taarifa zinafika haraka.
Hili jambo nalifananisha na kiranja wa shule kumtaarifu kiranja wa darasa kwamba kesho mwalimu mkuu anakuja kufanya ukaguzi fulani. Ni hiari yako kufanya au kutofanya. Kesho mwalimu mkuu ukija, ukionekana na makosa usioneshe ulikuwa na mawasiliano na kiranja wa shule, maana alikufanyia favour, lakini hujabebeka.
Kama mtu alitaka ufanye jambo jema akakutumia sms, si mbaya ukamsitiri. Je, unadhani sms isingetumwa nani angeonekana hawezi kazi? Muhongo au huyo Mama? Bila shaka Muhongo haguswi hata chembe.
Mkuu hujui serikali yetu inafanya vipi kazi.... utakuwa uko UN au umejiajiri.... waziri akutumie msg uache kutekeleza? Hujipendi..... na pale yule mama asingesema kwamba alipewa maelekezo hayo yeye alikuwa ni jipu moja kwa moja na yawezekana hata asingepewa muda wa kuandika hiyo barua.... angefukuzwa palepale..... ni uungwana wa waziri mkuu kutaka kujua undani zaidi na mdo uziri wa kumpa mtu nafasi ya kujieleza....