Rai: Waziri aliyetuma SMS kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo awajibishwe!

Labda utuambie waziri kosa lake ni lipi ambalo linafanya astaili kufukuzwa? Je, hilo la meseji tu au kuna lingine? Kama ni meseji....Basi sio kosa la kumfukuzisha mtu kazi.
Waziri Mhongo yupo kwenye Wizara ya Nishati siku nyingi. Sio Waziri mgeni yule kama kina Mpango na Nape. Anaijua situation vizuri. Kitendo chake cha kutuma meseji hata kama sio text msg, iwe hata barua formal au aina yoyote ya ujumbe, ni kudhoofisha dhana ya collective responsibility kwenye cabinet. Kama alijua kuna huo uozo (na kwa nafasi yake kama Waziri wa Nishati wa Kikwete lazima alijua) kwa nini hakurekebisha tangu day 1 alipoteuliwa hadi asubiri Majaliwa apange kwenda kutembelea ndipo aamue 'kumtonya' yule mkuu wa WMA? Utasemaje hakukua na nia ovu nyuma ya ule 'mtonyo'?
 
huyu mama hawezi kufukuzwa. Atapewa kazi nyingine. ulishajiuliza kwa mamlaka gani anao uwezo wa kutotumia system za nchi na kukosesha nchi mapato yeye kama yeye?
Hii issue ni syndicate.Cancer ni ccm na sio watendaji wa serikali. Wastafu na misingi mibovu ya maadili ya viongozi ndio imetufikisha hapa na viongozi wastaafu wa nchi hii.

Sijui kwanini commissioner wa maadilii asijiuthuru tu. sijui kaiz yake ni ipi hasa .
 
Utalalamika sana lakini ukweli unabaki palepale kuwa CCM INA WENYEWE...

Kwani umesikia kuna mfanyabiashara anachunguzwa kwa ukwepaji kodi kwenye hayo mafuta? Oilcom si ni ya Al Hooshom yule anachangia sana CCM, Lake Oil si ni ya wale vijana wa Home Shopping Center na wachangiaji wakubwa wa CCM. Hao ndio wenyewe huko ccm na so far utumbuaji majipu aliosema rais wangu Dr JPM ni kwa watumishi wa serikali pekee, wafanyabiashara hawaguswi. Huyo mama Chuwa wa WMA ni mtumishi wa serikali, ndio majipu rahisi kutumbuliwa raisi wetu hataki presha ya kutumbua majipu ya ukweli. Kumbuka usemi wa Pinda "Mafisadi wakikamatwa NCHI ITAYUMBA"
 
SIJUI WENZANGU NIMESOMA STORY ZA MAFUTA NA MABARUA YALE NIMEGUNDUA N ,MCHEZO MREFU SANA SANAA NA WASIKU NYINGI...SI HAPO OMBI LANGU KWA MH WAZIRI MKUU TUMEMSIMAMISHA HUYU JIPU ALIIEFUNGA HIZI MITA MBONA AMJALITUMBUA JIPU ALIEMWAMBIA ATAFUTE MAFUNDI HARAKA

HIVI AMWONI DHAMBI...HUYU ALIETUMA MSG WAZIRI ALIKUWA ANATAKA KUFICHA NINI

MH RAIS EMBU KAENI MSIPEPESE MACHO VUENI JIPU HILO LITAWATUMBUKIA KABLA AMJAAZAA NALO MUULIZENI MSTAAFU

USIKUMWEMA

Sasa kafukuzwa au kasimamishwa kazi kupisha uchunguzi?
 
Kwa taarifa yenu bado TPA wanaangaika nazo mwisho wameamua nao kuendelea na by pass.
Eventually, zitapona tu mkuu. Si wameanza kazi wiki iliyopita tu! Cha msingi JPM atusaidie kudai kodi yetu iliyokwepwa kwa miaka mitano. Hatutaki mambo mengi
 
Ndg. Rais nafikiri wahenga walisema kikulacho ki nguoni mwako. sasa huyo waziri ndio mmoja kati ya wanaokuzunguka lakini kumbe wanacheki myenendo yako na ya waziri mkuu waone kama itawafikia kwenye maslahi yao.
Mheshimiwa Rais timua huyu waziri haraka sana maana ameonesha usaliti na usipomtimua tunategemea kuvuja siri nyingi za kazi, baraza la mawaziri na hata siri zako binafsi.
 
Huwezi kumfukuza kazi waziri kwa ushahidi wa SMS, hizo fikra za kijinga sana. UKAWA mnapiga sana vita waziri Muhongo, mkishirikiana na yule mzee mwenye vituo vya habari. Hakuna mtu asiyefanya makosa. Lowassa alifanya makosa ndio maana akaambiwa ajiuzulu, lakini Lowassa huyo huyo amepata kura milioni 6, ameiwezesha CHADEMA kupata wabunge wengi. Kama binadamu hasamehewi makosa yake, Lowassa asingepata hata kura laki moja. Kama Lowassa amesamehewa na kutazamwa upande wake mzuri kwanini Muhongo asisamehewe na elimu yake ikatoa mchango kwa taifa?.

Tubadilike watanzania, hizi akili za kumtazama mtu, eti mwaka fulani alifanya kitu fulani kwa hiyo hafai kupewa cheo fulani, ni akili za kipuuzi sana.
 
Mtazamo kama wako,ndiyo ulioifikisha hii nchi yetu hapa,Muhongo ana elimu kubwa na utaalamu wake unajulikana ulimwenguni kote,lakini nathubutu kusema,MUHONGO NI KIBARAKA WA KUTUNYONYA WATANZANIA,na ni aina ya kiongozi aliyesemwa na DONALD TRUMPH,ANASHIRIKI KUIIBIA SERIKALI YETU,HATUFAI HATUFAI HATUFAI!!!!
 
Ukisema kuwa kiongozi anayeshiriki kutuibia rasilimali zetu hatufai, basi unamaanisha kwamba Afrika haina kiongozi hata mmoja. Zaidi ya asilimia 90 ya viongozi tulionao wanao uhusiano kibiashara na makampuni ya kizungu. CCM inao viongozi wengi wa aina hiyo, CHADEMA inao wengi wa aina hiyo. Mwalimu Nyerere - "Nchi haziongozwi na malaika zinaongozwa na binadamu, Mungu ametaka sisi wenyewe tuziongoze nchi hizi".
 
Ukisema kuwa hakuna wakati kweny % umeacha 10%, maana yake wapo, unatuchanganya
 
Ukisema kuwa hakuna wakati kweny % umeacha 10%, maana yake wapo, unatuchanganya
Zaidi ya asilimia 90, maana yake wachache wapo lakini kwa bahati mbaya ukumbuke kuwa karibu nchi zote za Afrika haziruhusu wagombea binafsi wa urais. Mwalimu Nyerere alipigania mgombea binafsi aruhusiwe lakini ikashindikana. Hivyo hiyo asimilia chache ya wasafi, na yenyewe inao mtihani wa kupambana na urasimu wa siasa za vyama.
 
Sawa, kumbe wapo wachache
 
Back
Top Bottom