riltz
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 232
- 83
Mkuu msanii mbona najaribu kuwasiliana nawewe sjupati. Naomba unipm Luna deal tufamze. What's fair trade
Please respond our PMs
Mkuu msanii mbona najaribu kuwasiliana nawewe sjupati. Naomba unipm Luna deal tufamze. What's fair trade
Heshima mbele wana JF,
Nimekuwa nahangaikia kupata habari au msaada wa mawazo kutoka sehemu mbalimbali nafikiri na hapa jamvini lazima kuna msaada mkubwa wa mchango naweza kupata kwani naamini hapa ni kitovu cha taaluma na ujuzi wa mambo.
Kwa muda mrefu sana nimekuwa nikifikiria na kutafuta njia mablimbali za kuweza kufanya sisi kama vijana wa kitanzania katika mambo ya kiuchumi (nikimaanisha kuwa na biashara kubwa) tunazoweza kuanzisha vijana na kutufanya kuondokana na mawazo ya kuajiriwa hasa kwa vijana wenye elimu ya chuo kikuu. Lakini ninasikitika sana kuona watanzania wengi tunagombea nafasi za kuajiriwa tu na serikali yetu haina msaada wowote wa kuwezesha kuleta mafanikio. Serikali yetu inatafafsiri ujasiriamali ni kumwezesha mtu kupata rizki, mi naamini bila viwanda vidogo vya kati huo ujasiriamali hautakuwa na manufaa yoyote, wazalishaji wanatakiwa wajue soko na processing ikifanyika thamani ya mazao yao inaongezeka kwenye masoko ya kimataifa.
Kwa mtazamo wangu nimekuwa nikiamini watu wenye elimu ya chuo kikuu wanatakiwa kuwa na mtazamo wa kuanzisha ajira kwani wao wamepevuka upeo tofauti na waliokosa elimu hiyo.
Kwa wanaJF wanaojua jinsi ya kupata resources jamani ninaomba msaada wa mawazo.
Nimefanya feasibility study kwa miaka kadhaa sasa na hatimaye nimeaandaa business plan ya kufanya processing ya cassava (mihogo) kutengeneza starch. Mali ghafi hakuna asiyejua inapatikana nchi kwetu popote pale unahitaji kuwahakikishia wakulima soko tu na watakufanyia mambo ya kutosha. Hii itainua uchumi wa wakulima wadogo sana na hasa kwenye maeneo ambayo kilimo cha pamba kimeanguka na mikoa kame kama ya kati isiyo na zao la biashara kwani popote inastawi
Soko lipo juu sana na lengo ku export tayari kuna watu wanahitaji sana kuimport kutoka Tanzania nimejaribu kutangaza na kupata response nzuri sana. Kuna soko kubwa sana nchini (yote inaagizwa toka nje esp SA) kuna soko kubwa sana pale TBL na viwanda vingine vinavyotengeneza madawa, nguo, bia, tambi, biscuits, noodles, almost viwanda vyote vinavyotengeneza vyakula (canned na bottled) vinahitaji starch.
Tatizo kubwa nililonalo ni kwamba natafuta source ya funds kuanzisha kamradi haka ambacho profit margin yake ipo juu sana. Nipo tayari kwa mazungumzo specific ya jinsi ya kufanya ili mradi niweze kutimiza hii ndoto. Mradi huu unaweza kuwa expanded katika muda wa miaka 2 au 3 ukawa na plant nyingine ya kuzalisha ethanol kwa kutumia waste materials baada ya kuprocess cassava na tayari nimeanza kudraft plan yake. Nimejaribu kupita Tanzania investment bank na kuongea nao wakawa na interest ya kusaidia ila nikawa sina colateral wala mdhamini mwenye assets nzuri (mimi mtoto wa mkulima tu hata elimu yangu ni ya kuungaunga tu) ninaweza kuraise kidogo tu. Nimepita na NBC ikawa vilevile tu na mradi unakubalika na tatizo siaminiki tu kwa vile sina historia ya kushika pesa kubwa.
Ninaweza kusimamia hii kazi na ikawa juu kiasi cha kuridhisha na kushindana na biashara kubwa tu hata kuanzisha zingine safi zaidi.
Haya wadau naomba reference kwenye source au tujiunege na kuona nini cha kufanya. Nipo kwa wazi nasikiliza mawazo yenu na ushauri! unaweza kuchangia au kuniPM vyovyote utakavyoona
Ahsanteni sana
Mkuu niwie radhi sana kwa kutokufikia kwa wakati.Msanii pliz respond ASAP
Mkuu
watu wa Oxfarm wanatoa funds kwa projects kama yako. wameshafadhili na kuendeleza miradi kadhaa afrika hivyo usisite kuwatafuta.
mimi nina knowledge ya fairtrade ambapo kama ukitaka tuition na contacts usiogope kuwasiliana.
..................hongereni wanaJF kwa ushirikiano mnaounesha kila mara inapohitajika kufanya hivyo. Mungu awabariki
Unapata ujuzi how to participate in Trade Fair.
TANTRADE wangelikuwa moderate wangesaidia exhibitors wengi wanaoshiriki sabasaba. Ila undundundu wetu unatulipa mabua
We are the company dealing with technical issues to support other businesses, achieve their goals.
We prepare and offer the following services to Non Government Organizations (NGOs) and Companies: (1)Concept Paper (2) Project Proposals (3) Business Plans and businesses registration (4) Budgets (5) Annual Work Plan (6) Annual Accounts (7)Annual Report (8) Sourcing Donors / Funders for your Projects. (9) Project Design (10) Project Management (11) Project Monitoring and Evaluation (12) Capacity Building & Training to your organization etc. For no small or big business we can't serve. Please Contact us through, Bizsolutions Co.Ltd, 0688778484. Email:-bizsolutions@mail.com
Mkuu, biashara zilizopo kwenye fairtrade markets zimeorodheshwa kwenye constitution ya Fair Trade Organization. Nakutajia kwa uchache, Kazi za mikono yaani craftworks (kingoni), Mazao kama ndizi, kahawa, chai, Zanzibar Spices.... orodha kamili sinayo hapa ila naamini ukianza kulifuatilia hili soko utajifunza mengi sana.Mkuu....kama hutajali hebu funguka zaidi ni Biashara gani wanazodili nazo hao ndg km hutajali nakuPM mawasiliano yangu...ili nipate hii Elimu vzr
Tuwasiliane mkuu wanguMsanii shida yangu mimi ipo kwenye hizo mambo za proposal write up for NGOs ,nipe maelezo kidogo ya Oxfam
Kiongozi, nimejaribu kukutafuta nakukosa. Naamini kama ukimaanisha kuisaidia sekta ya wazalishaji nchini basi ukipata some hints kutoka kwangu utaweza kwenda beyond levels na kufungua fursa nyingi kwa wabongo...Hi wajasiliamali wenzangu!
We are a company of business and management experts dealing with various consultancies such as project write ups, pcroject evaluations, business plans, company registrations, Taxation, tax returns, business names, business consultancies etc.
Any firm , NGO, company or individuals who need to write a proposals for funding etc, are highly invited to PM the author.
We are committed to finish your work within a given time frame in a professional way you can't imagine. Our price is negotiable. "Kazi Bora kwanza!" is our motto. Mteja wetu huwa analeta kazi nyingine na Wateja wengine, jaribu kutupa kazi hautajuta! PM the author for more details or phone us through our # +255 688 778 484 advance payment siyo lazima kazi kwanza!
Nimejaribu kuanzisha mradi wa kilimo cha ufuta huko Ruangwa,kwa msim huu nimeanza na heka 5,ntawapa mrejesho
mrejesho vipi ulipoishia mkuu
Ni kwamba mavuno hayakua mazur mdau,kama unavyojua hali ya hewa ya mwaka huu iligubikwa na ukame,briefly nimepata hasara,mwaka huu nimeshindwa kulima kwa kua mfuko wangu hauruhusu na pia nilishikwa na harakat za masono,may be msimu wa 2016/2017 ntarud tena shamba,kama nitalima Kusini bas ni Ufuta na Mbaaz,na kama ntalima Songea ni Mahindi na Tangawizi,bado naamini Kilimo kitafikisha somewhere
Pole sna mkuu kwa changamoto zilizokukuta, kikubwa ni kupigania kile unachokiamini hata kama utapita kwenye mazingira magumu.
Hope utafanikiwa msimu ukiwadia nakutakia kila jema kwako.