Sooth
JF-Expert Member
- Apr 27, 2009
- 3,922
- 5,617
Ntambaswala,
Kwa maoni yangu, hizi ni siasa za Mbeya tuu, hakuna ubaya kuwa na 'wishfull thinking' hata kama ni empty hopes. Hebu mfikirie JK na umaarufu aliokuwa nao 2005 na jinsi alivyoshinda kwa kishindo kwa over 80%, halafu fikiria kilichompata JK kwenye uchaguzi wa 2010 na ujio wa Dr. Slaa kwenye mbio hizo, JK licha ya kuwa ni sitting president, akigombea kiti alichokikalia with all the support ya presidential institution, halafu CCM ndio chama tawala, ukijumlisha mbinu zote walizotumia, safi na chafu, plus support ya Tume pendeleo ya uchaguzi kuwasaidia, bado ushindi wa JK ulipururuka mpaka 40%!, hivyo mgombea wa CCM wa 2015, lazima awe ni mtu atakayeweza kumkabili Dr. Slaa, kitu ambacho si Prof. Mwandosya, wala Dr. Mwakiembe ana fit, unless otherwise kama CCM kupitia state machinery yake, watafanikiwa kum contain Dr. Slaa before 2015!.
Nashauri wale washabiki wa siasa za Mbeya, kwenye urais, bora msahau, the sooner the better, ili msijeishia kujihuzunikia bure.
Nakumbushia kwa msisitizo, kuna makabila fulani, uraisi ni BIG NO!
Nakubaliana na maoni yako, lakini nadhani hapo mstari wa mwisho ndo umeharibu. Tukianza kutenga makabila fulani, hatutaishia hapo-tutawatenga watu kwa umri (mfano 2015 hatutaki wazee), jinsi, kanda, dini, n.k. Hizi ni criteria ambazo tukizipa kipaumbele, hatutoondoka kwenye lindi la umasikini tulipokwama kwa miaka mingi.