Ntambaswala
JF-Expert Member
- Dec 7, 2008
- 255
- 78
Kuelekea uchaguzi kwa 2015, habari za kuaminika kutoka vyanzo visivyopenda kujulikana zinadai kuwa hawa jamaa sasa hivi hawaivi chungu kimoja. Ingawa mwaka 2005 walikuwa pamoja, inaaminika kuwa sasa kila mtu yuko kivyake hasa kwa vile Dr. Mwakyembe naye ni malighafi ya urais
Pia inaaminika sasa hivi JK anaelewana vizuri na Profesa Mwandosya kwani aliyekuwa hasa anawatenganisha kabla( ukiacha ugomvi wao wa zamani) ni Edward Lowasa ambaye inasemekana anaelekea kumalizwa nguvu zake ndani ya CCM na serikali.
Kitendo cha Profesa kuwa karibu na JK kinaonyesha kuwa angalau sasa Profesa anaweza kuwa na sapoti fulani toka kwa JK kama ataamua kugombea. Kitendo hicho hakijawafurahisha Sitta na Dr. Mwakyembe ambao wanaona mmoja kati yao ndio anafaa kuwa mgombea urais 2015.
Pia kitendo cha Mpendazoe kuwaumbua Dr Mwakyembe, Sitta na Nape kuwa ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ kimewapunguzia sana umaarufu ndani ya chama, huku Profesa akiwa hajapata msukosuko wowote wa kisiasa.
Hata hivyo tofauti na Profesa, Dr. Mwakyembe anauzika kwa urahisi na hata chama cha wazee wa kuandamana wanamkubali sana Dr. Mwakyembe tofauti na Profesa ambaye hakubaliki kabisa hata na CUF au NCCR Mageuzi.
.