Profesa Mwandosya na Dr. Mwakyembe hawapikiki

You've spoken well ndugu, hii nchi imekuwa na watu ambao ni obsessed na uongozi. Hata mwaka haujaisha tangu uchaguzi uliopita, sisi tunawaza rais ajae.

Mambo ya kuandaa wagombea mwezi mmoja kabla ya uchaguzi ndio yanatuharibu watz. Waulize CHADEMA kuhusu Shibuda, unadhani wangeandaa mgombea wao mapema yangewakuta haya ya leo?

Rais mpya anaanza kuandaliwa siku ile tu rais mteule anaapishwa.......................
 
Rais wa 2015 atakuwa ni Mheshimiwa Gwamahala Gwaijolo Gwamaka Gwanaloli...!!! Kupitia mgombea binafsi.
 
Kama ilivyo kwa Rais wa sasa na Bagamoyo, Prof Mwandosya anaweza kuwa na vision ya Mbeya lakini hana vision ya Tanzania nzima. All road will lead to Mbeya under him. Tukumbuke chini ya huyu Mwandosya ndio TTCL iliongeza kasi ya kuelekea kaburini, alisimamia mkataba mbovu kati ya TTCL na MSI (mzazi wa Celtel).

Tafuteni research za Russell Southwood, editor for Balancing Act's News Update au Kitabu chake 'Less Walk more talk - How Celtel and the Mobile Phone changed Africa. Ukisoma documents za MSI/Celtel, inaonekana kama wataalam wetu hawakuelewa ni kitu gani walikuwa wana-sign! Sijui Prof Mwandosya kama aliona makosa yaliyokuwa yanafanyika wakati wa mkataba au la? Na kama shirika moja tu linamshinda Prof Mwandosya itakuwaje akikabidhiwa nchi? Pia akiwa kama waziri wa maji, ni nafuu gani watanzania wamepata kuhusu maji? Unaweza kulinganisha utendaji wake na wa mtu kama Magufuli?

Narudia, Prof. Mwandosya anaweza kuwa na vision ya Mbeya lakini hana ubavu wa Tanzania. And after what this country has been through hatutaki usanii wa kuuza sura! Tunataka watu wenye proven track record katika utendaji kazi.
 
CCM wamchukue naibu meya wa Arusha, mr Mallah..............

Ohhh, Mwandosya akiwa Waziri alikuja Tabora Airport na kuiba mapipa ya lami na kibaya ni kuwa Mbeya hayajatumika na Tbr kiwanja ni vumbi.
 
CCM wamchukue naibu meya wa Arusha, mr Mallah..............

Ohhh, Mwandosya akiwa Waziri alikuja Tabora Airport na kuiba mapipa ya lami na kibaya ni kuwa Mbeya hayajatumika na Tbr kiwanja ni vumbi.

Nashukuru kama umejua kuwa jamaa ni bogasi kabisa
 
Sikonge,
Nasikia anaungana na Sambwee Shitambala aka Abdulrahman. Unajua tumepiga mkwala mzito sana ndani ya Magamba, hakuna kumpa cheo chochote au madaraka mtu aliyetoka upinzani hasa CDM labda Tundu Lissu na Slaa. Maaana huyu Shita alishaanza hata kujigamba kuwa anakwaa posti ndani ya wiki mbili. Hakujua Makamba ndo anaondoka hivi. Nakwambia jamaa ana mawazo ila mbaya maana amekuwa kama Musalia Mudavadi wakati ule
 
.......... Tukumbuke chini ya huyu Mwandosya ndio TTCL iliongeza kasi ya kuelekea kaburini, alisimamia mkataba mbovu kati ya TTCL na MSI (mzazi wa Celtel).....................................

Umesema weel ndugu huyu mpaka gazeti la rai kipindi ile lilitoa issue nzima ya rushwa na jinsi mwanae Mwandosywa ( Au mmoja wa ndugu zake) alivyogharimikiwa Chuo na hoteli za kifahari huko South africa. Kampuni iliyoingia gharama hizi ilikuwa moja ya kampuni tanzu iliyonunua TTCL kwa bei chee........

Huyo ndio prof Mwandosya na CCM........
 
Kingine huyu jamaa ni mkabila bora kusikia, tuombe Mungu ujue nchi itagawanyika, itakuwa kila mahali akina Mwanafyale tu. Huyu jamaa muda wake umepita hawezi kusimama na Mkulungu mbegu ya dume Samweli Sita kwenye majadala wowote wa hali ya siasa ya nchi yetu, ujue atamchana chana vibaya mno.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
mwandosya hafai hata kwa bure,msitishwe na yeye kuwa prof...a prof is a person who knows much about a very little thing...kama anajua juu ya jicho basi hajui juu ya sikio..........huyu hafai kabisa kwanza mgonjwa

nije kwa mwakyembe: hakuna mtu ndumila kuwili kama hyu jamaaa....hana tofauti na sita...ni mtu wa majigambo sana.......hana lolote na hawezi sana sana atazika nchi......mpaka sasa kama naibu waziri anabebwa na pombe...
 
Pasco,
Umepigilia msumari hasa, uliyosema ni kweli kabisa. Na mimi naona kweli hizo ni wishful thinking kwa watu wa Mbeya kutaka kutoa rais. Ila mke wangu hajapendezwa kabisa na post yako maana anaamini kaka yake (shemeji yangu) -Dr Mwakyembe ndo atakuwa mgombea wa urais 2015, iwe kupitia magwanda au magamba
Ntambaswala, mpe pole shemeji, mwambie Mwaki na mwenzake Six, wamepewa pipi bazoka (bigijii) baada ya kuiasisio CCJ, ingekuwa ni hatari sana kuwaacha mbali, kwa ule utaratibu, keep your friends close, but your enemies closer, lakini kama ilivyo bazoka, ikishakwisha utamu, hutemwa. Hiki ndicho pekee kinachowasubiri.

Eneo la hatari kuliko eneo lolote nchini Tanzania kisiasa ni Kanda ya Ziwa. Ni kura za Kanda ya Ziwa ndizo determinant factor nani anakuwa rais wa Tanzania. Kwa kuzingatia kilichomkumba Masha na Diallo, ili kurudisha kanda hiyo CCM, 2015, CCM, itamsimamisha John Pombe Magufuli, japo CCM hawampendi kwa vile yuko too genuine, nao wamezoea kufanya madudu, huyu ni no-nonsense-man, lakini itabidi wamsimamishe yeye tuu kama the one and only that CCM has, anaweza kumkabili Dr. Silaa na kubadili direction ya 'the wind of change which is sweeping accross Tanzania'.
 
mwandosya hafai hata kwa bure,msitishwe na yeye kuwa prof...a prof is a person who knows much about a very little thing...kama anajua juu ya jicho basi hajui juu ya sikio..........huyu hafai kabisa kwanza mgonjwa

nije kwa mwakyembe: hakuna mtu ndumila kuwili kama hyu jamaaa....hana tofauti na sita...ni mtu wa majigambo sana.......hana lolote na hawezi sana sana atazika nchi......mpaka sasa kama naibu waziri anabebwa na pombe...

Profesa kuumwa mbona jambo la kawaida..........kuna mtu asiyeugua jamani. Huo ugonjwa unaomsumbua sio ugonjwa wa kufisha
 
Mpaka sasa hivi tunafahamu kuwa:

1. Sitta aliiba sana CDA enzi zake. Pia matumizi mabaya ya pesa akiwa Spika wa bunge na moja wapo ni kujenga ofice ya Spika Urambo na sasa imekaa tu wakati yeye ni Waziri kwa sasa. Nina wasiwasi akichaguliwa basi Ikulu itajengwa Urambo. I wish ingelikuwa Sikonge, ila ndiyo hivyo tena kwa sisi wa Sikonge tulie tu.

2. Mwakyembe miezi kadhaa nyuma kafukuzwa jimboni kwake Mkuku na karudi na akina Sitta wampe nguvu ya kuingilia. Ni heri Mwakalinga angelikuwa mbunge huko maana walau kungelikuwa na nafuu. Aliwaahidi watu kujenga kipande kidogo cha barabara na kimemshinda. Zamani alikuwa akitumia visingizio vya Mwakipesile anafanyia majungu, Mwakalinga anamchonganisha na UK, Lowassa na Rostam wanataka kummaliza. Ila sasa hao ndiyo hawana nguvu kabisa na yeye ni Naibu waziri wa Ujenzi, sasa shida iko wapi?
Huyu mkimchagua, MTAMKUMBUKA HATA KIKWETE maana visasi vyake, wengi watakimbia Tanzania.

3. Mwandosya tumeshajua jinsi alivyoifilisi TTCL. Nina imani hajaanzia hapo au kuishia hapo. Pia nimeandika juu kuwa aliiba mapipa ya Lami ili kwenda kujenga uwanja wa ndege Mbeya ambao umemshinda. Kibaya zaidi ni kuwa, pembeni mwa uwanja wa ndege wa Mwandosya hapo Mbeya, kuna kiwanda cha Cement ambayo ni nzuri zaidi ya Lami kwenye kujenga Landing Lanes na majengo kwa ujumla.

4. Magufuli na kama Lowassa. Ni wachapa kazi na wanaweza kufanya maamuzi magumu. Ila wote wakichaguliwa, nusu ya mali ya Tanzania watajiuzia wao. Wilaya zao itakuwa ni kama Yamoussoukrou huko Ivory Coast enzi za Félix Houphouët-Boigny ambapo alijenga kanisa kubwaa kuzidi la Vatican (St Peter) na mji kwa ujumla ambao hadi leo majengo yako wazi mengine.
 
Ntambaswala, mpe pole shemeji, mwambie Mwaki na mwenzake Six, wamepewa pipi bazoka (bigijii) baada ya kuiasisio CCJ, ingekuwa ni hatari sana kuwaacha mbali, kwa ule utaratibu, keep your friends close, but your enemies closer, lakini kama ilivyo bazoka, ikishakwisha utamu, hutemwa. Hiki ndicho pekee kinachowasubiri.

Eneo la hatari kuliko eneo lolote nchini Tanzania kisiasa ni Kanda ya Ziwa. Ni kura za Kanda ya Ziwa ndizo determinant factor nani anakuwa rais wa Tanzania. Kwa kuzingatia kilichomkumba Masha na Diallo, ili kurudisha kanda hiyo CCM, 2015, CCM, itamsimamisha John Pombe Magufuli, japo CCM hawampendi kwa vile yuko too genuine, nao wamezoea kufanya madudu, huyu ni no-nonsense-man, lakini itabidi wamsimamishe yeye tuu kama the one and only that CCM has, anaweza kumkabili Dr. Silaa na kubadili direction ya 'the wind of change which is sweeping accross Tanzania'.

Pasco umeongea mambo mazito. Pamoja na kuwa mimi ni mmoja wa wafuasi wa 'kuchukia kujadili urais wa 2015', kwasababu naamini ni kati ya mambo yanayotufanya tujisahau na kuendelea kusota na kero zilizopo.Nakubaliana na hoja kuwa ni vizuri tuanze kufikiri na kujiandaa nani atatufaa mapema sasa. Lakini kwa style ya nchi yetu, twaweza piga kelele weee kuwa nani anafaa na nani hafai lakini isisaidie chochote!Ila kama usemavyo, hawa jamaa wote hata sio, huyo Mwakyembe ni kweli ndumilakuwili na majigambo kama nini!Mwandosya ndio balaa kubwa,waulize hapo Wizara ya Maji watakwambia jinsi alivyojaa na mshipa wa nepotism, hata miradi kibao ya maji anaipeleka kwao-sijui ndio mtaji wa Urais!(Hapishani na Ngeleja anayetuhumiwa kwa tabia hii pia).
Yote kwa yote, pamoja na kujadili nani Rais 2015, hebu tusijisahau kuwa matatizo tuliyonayo kama nchi ni makubwa na mengi mno, hata 2015 ni kama mbali mno,nchi inateketea!
 
Hakuna hata jina moja ulilotaja laweza kupitishwa. Nasikia Naodha au mwanamama wa UN anaweza kuwa mgombea wa chama cha magamba

Sasa hivi kuna rungu zuri sana la kupondeana ndani ya chama. nalo ni kutangaza kuwa sasa hivi ni zamu ya mwanamke. ukitaka kujuwa utamu wa kauri hii muulize sita kilichotokea kwenye uspika.
 
Umesema weel ndugu huyu mpaka gazeti la rai kipindi ile lilitoa issue nzima ya rushwa na jinsi mwanae Mwandosywa ( Au mmoja wa ndugu zake) alivyogharimikiwa Chuo na hoteli za kifahari huko South africa. Kampuni iliyoingia gharama hizi ilikuwa moja ya kampuni tanzu iliyonunua TTCL kwa bei chee........

Huyo ndio prof Mwandosya na CCM........

Alikua ni binti yake kipenzi aitwae sekela mkuu,alilala protea hotel south africa kwa gharama za kampuni ulioitaja ndio kina kikwete na genge lake likiongozwa na rostam na lowassa walipogundua na kumpunch kwenye rai kipindi hicho wakimtumia salva rweyemamu....ambae yuko ikulu sasa kama asante ya kazi nzuri
 
Pasco umeongea mambo mazito. Pamoja na kuwa mimi ni mmoja wa wafuasi wa 'kuchukia kujadili urais wa 2015', kwasababu naamini ni kati ya mambo yanayotufanya tujisahau na kuendelea kusota na kero zilizopo.Nakubaliana na hoja kuwa ni vizuri tuanze kufikiri na kujiandaa nani atatufaa mapema sasa. Lakini kwa style ya nchi yetu, twaweza piga kelele weee kuwa nani anafaa na nani hafai lakini isisaidie chochote!Ila kama usemavyo, hawa jamaa wote hata sio, huyo Mwakyembe ni kweli ndumilakuwili na majigambo kama nini!Mwandosya ndio balaa kubwa,waulize hapo Wizara ya Maji watakwambia jinsi alivyojaa na mshipa wa nepotism, hata miradi kibao ya maji anaipeleka kwao-sijui ndio mtaji wa Urais!(Hapishani na Ngeleja anayetuhumiwa kwa tabia hii pia).
Yote kwa yote, pamoja na kujadili nani Rais 2015, hebu tusijisahau kuwa matatizo tuliyonayo kama nchi ni makubwa na mengi mno, hata 2015 ni kama mbali mno,nchi inateketea!

mimi ni miongoni mwa watu wengi wanao mpenda magufuli awe kiongozi kama uwaziri mkuu lakini sipendi awe rais. kwangu ni bola lowasa kuliko magufuli kwa urais.
tukiacha ushabiki wa watu lowasa anamaamuzi siyo kulialia tu, mala tusitumie magari ya galama kubwa lakini anaidhinisha yakanunuliwa!.
 
CCM wanaweza wakaendelea kuongoza dola kama watampendekeza Sitta kugombea urais 2015,ila wakiteua mwingine yeyote CDM njia nyeupe pee.
Samwel Sitta yupi unaemzungumzia wewe? ni huyu huyu anaejiita spika mstaafu wakati tunajuwa alipigwa chini kwenye uchaguzi? jitu limeng'ang'ania nyumba ya Spika mpaka leo hutadhani hana nyumba nyingine pale Oysterbay halafu unataka kutufanya sisi mazuzu tuwe na Rais mlafi kama huyu mnafki Sitta? huyu akipewa urais tujiandae kujenga ikulu mpya maana hata akishindwa uchaguzi ujao ataifanya ikulu ya magogoni kuwa ni makazi yake kama Rais mstaafu.
 
Back
Top Bottom