Profesa Muhongo: Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati

Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja moja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.
Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.

Huyu ni Muhongo bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.

Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.
Huyu ni Professor Msomi ana hakika na anachokisema. Enzi hizo hakuweza au aliweza akatupwa kwenye Recycle Bin.
 
Tundu Lissu, Muhongo, Lema na Chadema kwa ujumla mkitaka kuuwa legacy ya hayati rais Magufuli kwa watanzania itabidi ufanye yafuatayo.

Unapokula kichwa mradi wa umeme kutoka bwawa la Nyerere ambao umefikia 50% itabidi watuambie umeme tutatoa wapi?.

Unapokula kichwa serikali kuhamia Dodoma na kusema ni hasara itabidi wajieleze.

Unapokula kichwa reli ya kisasa ambayo inakaribia Makutupora itabidi wajieleze kwa watanzania hiyo Tanzania ya viwanda itawexekana vipi.

Unapokula kichwa ujenzi wa meli mpya kwenye maziwa makuu itabidi watueleze watatusafirisha na nini?

Wanapokula kichwa ndege zetu itabidi tuwawekee video za kina Heche ,Lema,Lisu wakitukana serikali iliyoshindwa kununua ndege

Watakaposema wachimbaji wadogo, bodaboda na mama ntilie wafukuzwe itabidi watueleze wanafanya haya kwa faida ya nani?

Watakapoamua zahanati na hospitali zote zilizojengwa na Magufuli zifungwe ,itabidi watueleze tutaenda kutibiwa wapi?

Watakaposema wamefuta elimu bure itabidi watueleze kodi zetu zinafanya kazi gani?

Watakaposema lazima watanzania millioni 60 wachanjwe, itabidi watueleze wao mpaka sasa
hawajachanjwa
Nyungu hawajapiga,
Hawajajifungia ndani wanaenda kazini kila siku
Mbona hawajafa na corona sasa?

Watakaohoji haya maelezo siyo Magufuli wala watoto wa Magufuli ni watanzania.

Anayedhani itakuwa rahisi kuuwa legacy ya Magufuli atakutana na nguvu ya uma.

Muda utaongea .
Hii ni miradi inaitwa WHITE ELEPHANTS. Unaweza ukaimaliza lakini isikupe Desired Return on Investment.

Kwa mfano SGR hata ikimalizika kwenda huko Rusumo sijui ambako tuna target mzigo wa Rwanda, bado haina faida kwa vile throughout ya Rwanda ni less than 800k metric tons per annum.

Mzigo wa ndani ni very insignificant kwa vile Magufuli hakuwa na vision. Anajenga reli huku anaua sekta binafsi. Amefirisi akina Yusuf Manji, amewatisha kina Mo Dewji kwa kuwateka, amesababisha vifo vya akina Mufuruki na Shamte kwa chuki zake, Je anategemea local traders gani wasafirishe mzigo kwenye SGR?

Hiyo Stiglers Gorge ni upotevu wa Matrilioni ya hela tu kwa kuwa mabadiliko ya tabia nchi ndiyo adui mkubwa wa hydro electricity. Kamwe hawezi kupata hizo megawatt 2100 kama alivyotamba kwenye maradio na matv.

Ameshia kuharibu baioanuai ya selous tu na kuteremsha hadhi ya pori tengefu
 
Huyu mzee naye wakati mwingine sijui anafikiria nini.

Dunia inaelekea kwenye renewables yeye anasema twende kwenye fossil fuel. Sijui ni dunia gani anaiongelea. Umeme wa maji ndio wa bei rahisi zaidi duniani, na wala hatukatazwi kuwa na vyanzo vingine mbadala. By the way, Stiglers ndio ishakuwa mimba, tusubiri kuzaa tu.
 
Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja moja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.
Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.

Huyu ni Muhongo bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.

Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.
muda wa kuchukua chako mapema
 
Akichangia katika mpango wa maendeleo wa Serikali bungeni amesema anashangaa watu wanavyohangaika na umeme wa maji na huku dunia ya sasa ni umeme wa gesi

Uchumi wa sasa duniani ni umeme wa gesi, umeme wa maji umepitwa na wakati.

Mbunge wa Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema uchumi wa gesi pekee ndiyo utakaoifikisha Tanzania kwenye uchumi thabiti.

Profesa Muhongo ametoa kauli hiyo wakati akichangia kwenye mpango wa Serikali leo Aprili 9,2021 bungeni Jijini Dodoma

Waziri huyo wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini amesema Tanzania kuendelea kuwaza kuhusu madini yaliyopo ni kuchelewa huku akikosoa mawazo ya kutegemea uzalishaji wa umeme mkubwa kwa kutumia maji.

Amesema Tanzania inatakiwa ijikite katika matumizi ya umeme mchanganyiko badala ya kutegemea mabwawa ya Maji ambayo wakati wowote yanaweza kukauka.

"Kuwekeza katika umeme wa maji halafu unasema utaleta fedha, huko ni kujidanganya kwani umeme wa maji huchukua muda mrefu kuanza kutoa faida, huko wenzetu wamepita wanafanya mambo kisasa” amesema Profesa Muhongo.

Amesema dunia ya sasa imegeuka na madini mengi yanayotarajiwa Tanzania yapo lakini wengine wameelekeza kwenye dhahabu, Tanzanite na madini mengine ya zamani lakini wanaacha kuangalia madini mapya ambayo yataliingizia Taifa fedha nyingi.


NB: Baada ya Dkt. Magufuli kuondoka sasa kila mtu CCM rangi yake ya zamani imeanza kurudi

Hivi kweli mmeanza kupinga project ya Rufiji baada ya Dkt. Magufuli kudondoka

CCM acheni unafiki
una ujinga mahali fulan, we unazan maisha yote utabak kuwa na maji tiririka?huon mabadiliko ya hewa dunian? acha kufanya mawazo ya kibogoyo bro
 
Ila alichosema ni ukweli..klabdaarne hii kuanza kuangaika na umeme wa maji ni kupoteza muda tu
Naona sasa ni wazi kuwa walioteseka kipindi cha magu wanaanza kufufuka,muulizeni swali katika dunia hii umeme wa bei rais unatokana na nini? na pia muulizeni ni nchi gani duniani inaongoza kwa Kuzalisha umeme wa gas na inazalisha kwa kiwango gani?
 
Hesabu za Pole pole za hizi hazijaiva, hizi zimeiva na unaenda na tatu kichwani sio hesabu za mambo serious kama haya.
Umeme wa maji ndiyo nishaji yenye gharama nafuu duniani. Ukisikia mtu anajiita profesa anauponda cha kutilia shaka ni vyeti vyake tu.

Kwa hesabu ndogo tu Megawati 2,100 ni sawa na kilowati 2,100,000 Unit za umeme ni kilowati moja ikitembea kwa saa moja.

Sasa ukiwa na kilowatt milioni mbili na laki moja zikatembeza mitambo kwa masaa 24 unapata unit za umeme milioni 50.4. Ukiuza umeme huu kwa wateja angalau kwa unit moja shilingi 100

Mtambo unaweza kutoa mapato ya bilioni 5 kwa siku. Ukitoa mwezi mmoja kwa mwaka kwa ajili ya "maintenance" ukatembea miezi 11 unaweza kupata trilioni 1.7 kwa mwaka Tumeujenga kwa shilingi trilioni 7. Almost 5 years mradi kama utakuwa full operational unarudisha gharama.

Kama taifa lazima tujue wataalamu wetu ndiyo wamekuwa wakitupotosha na tatizo ni elimu yetu ndiyo mbovu.

Ukichukua mtu aliyesoma miaka ya 70, nchi haina wataalamu huku kwenye elimu ya chini, wanasema nyumba ni msingi hivyo ukikosa basic education huko juu mtu anaenda tu. So unaweza kuta mtu ni profesa but anafanya maamuzi au ushauri wa ajabu.

Labda tujenge mradi but mashine tusifunge megawati zote 2100 kwa kuwa kwa sasa hatuna soko la kutosha.

Kadiri tunavyoongeza ndivyo tutakavyoongeza kufunga mashine.

Umeme wa maji unategemea jiografia hivyo wengi hawatumii kwa kuwa jiografia haziwaruhusu.

Chukua mfano mdogo tu wa gari, Gharama ya kuendesha gari kwa kunua mafuta ndiyo gharama ya juu kuliko gharama ya kununua gari lenyewe.

Mmfano umenunua gari la milioni 12 kama ukiweka mafuta ya 20,000 kwa siku ndani ya mwaka utaweka mafuta ya 7,300,000 (milioni saba na laki tatu)

Ukikaa nalo miaka 10 utatumia mafuta ya milioni 73.

Lakini sasa anakuja mtu ana gari anauza milioni 16 lakini unaedesha kwa kutumia maji.

Ndani ya miaka 10 la mafuta kununua na mafuta ya uendeshaji ni milioni 85 wakati la maji ni milioni 16.73

Hivi ndivyo umeme wa maji ulivyo nafuu kulinganisha na umeme wa mafuta au diezeli.

Mashine zinazungushwa na maji hahuhitaji kununua nishati ya kuendesha.
 
Dooh nimecheka saana haya watu wanafufuka mmoja moja wanaaanza upya kuchomoa makucha yao.
Hawana tena cha kuhofia mana enzi za shamba la bibi zinarudi kila mtu anaanzisha ubunifu mpya wa kupiga pesa.

Huyu ni Muhongo bado namsubiri Ngereja naye atakuja na lipi.

Na muda si mwingi tutasikia Accacia nayo imefufuliwa upya na kupewa mgodi huko geita kwasababu nchi inahitaji zaidi wawekezaji kuliko wao wanavyo tuhitaji.
Huyo magu mwenuewe fisadi kubwa
 
Umeme wa maji ndiyo nishaji yenye gharama nafuu duniani.

ukisikia mtu anajiita profesa anauponda cha kutilia shaka ni vyeti vyake tu.

kwa hesabu ndogo tu

megawati 2,100 ni sawa na kilowati 2,100,000

unit za umeme ni kilowati moja ikitembea kwa saa moja.

sasa ukiwa na kilowatt milioni mbili na laki moja zikatembeza mitambo kwa masaa 24 unapata unit za umeme milioni 50.4

ukiuza umeme huu kwa wateja angalau kwa unit moja shilingi 100

mtambo unaweza kutoa mapato ya bilioni 5 kwa siku.

ukitoa mwezi mmoja kwa mwaka kwa ajili ya "maintenance" ukatembea miezi 11

unaweza kupata trilioni 1.7 kwa mwaka

tumeujenga kwa shilingi trilioni 7

almost 5 years mradi kama utakuwa full operational unarudisha gharama.

kama taifa lazima tujue wataalamu wetu ndiyo wamekuwa wakitupotosha na tatizo ni elimu yetu ndiyo mbovu.

ukichukua mtu aliyesoma miaka ya 70, nchi haina wataalamu huku kwenye elimu ya chini, wanasema nyumba ni msingi hivyo ukikosa basic education huko juu mtu anaenda tu. So unaweza kuta mtu ni profesa but anafanya maamuzi au ushauri wa ajabu.

labda tujenge mradi but mashine tusifunge megawati zote 2100 kwa kuwa kwa sasa hatuna soko la kutosha.

kadiri tunavyoongeza ndivyo tutakavyoongeza kufunga mashine.

umeme wa maji unategemea jiografia hivyo wengi hawatumii kwa kuwa jiografia haziwaruhusu.



chukua mfano mdogo tu wa gari,

gharama ya kuendesha gari kwa kunua mafuta ndiyo gharama ya juu kuliko gharama ya kununua gari lenyewe.

mfano umenunua gari la milioni 12 kama ukiweka mafuta ya 20,000 kwa siku ndani ya mwaka utaweka mafuta ya 7,300,000 (milioni saba na laki tatu)

ukikaa nalo miaka 10 utatumia mafuta ya milioni 73.

lakini sasa anakuja mtu ana gari anauza milioni 16 lakini unaedesha kwa kutumia maji.

ndani ya miaka 10 la mafuta kununua na mafuta ya uendeshaji ni milioni 85

wakati la maji ni milioni 16.73

hivi ndivyo umeme wa maji ulivyo nafuu kulinganisha na umeme wa mafuta au diezeli.

mashine zinazungushwa na maji hahuhitaji kununua nishati ya kuendesha.


Mkuu nimeishia hapa:

"unit za umeme ni kilowati moja ikitembea kwa saa moja."

Pako fyongo sana hapo. Japo unge Google basi angalau kujua nini maana ya kilowatt.

Ukizidiasha mahaba zaidi ya facts mchuzi unadoda!

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom