Huyu jamaa mwanzoni nilidhani ni mtu anaesimamia ukweli bila kuyumbishwa kumbe nae ilikuwa njaa tu, baada ya kuteuliwa amekuwa mtu mwongo na mnafiki. Ni juzi tu bungeni Tulia alimzima kwa kutetea wizi, na bahati mbaya alichokuwa akikitetea, boss wake yaani Rais Samia alikuwa amekilalamikia kwa mkurugenzi nadhani halmashauri ya Mbeya, kwamba wamebuni mfumo wao wa ukusanyaji mapato nje ya mfumo wa serikali.

Leo amekuja na episode ya asilimia 78 ya maji vijijini. Haogopi kusema uongo. Ukimuuliza atakwambia leta ushahidi. JF, mlioko humu, ni yupi kijijini kwao kuna huduma ya maji safi na salama, labda tuanzie hapo.
Tuanze na yeye kwao kule Singida vijijini Kuna maji?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Profesa atakuwa yuko sahihi kwa sababu kwenye awamu ya kwanza ya utawala wa Hayati JPM yeye ndiyo alikuwa MHASIBU wa Wizara ya Maji
 
Prof. Kitila Alexander Mkumbo (Mb), Waziri Wa Nchi, Ofisi Ya Rais, Mipango Na Uwekezaji, akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2024/2025 amesema Kiwango cha wananchi wanaopata maji safi na salama kimeongezeka hadi kufikia asilimia 88.6 mijini na asilimia 78 vijijini.

Pia ameongeza kuwa idadi ya watalii imeongezeka mara mbili zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.

"Idadi ya watalii imeongezeka kutoka watalii 1,711,625 mwaka 2021 na kufikia watalii 3,818,080 mwaka 2022, ikilinganishwa na lengo la kufikia watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025/2026.

Hii imesababisha kuongezeka kwa mapato ya utalii kutoka Dola za Kimarekani bilioni 1.31 mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2.53 mwaka 2022, sawa na ongezeko la asilimia 93.1."

#KutokaBungeni

Prof. anazungumzia vijiji gani, vya Ulaya?

View attachment 2805901
Mbona kidogo Sana? Target ni 85% by 2025 naona haitafikiwa.
 
Vijiji vipi?
Aache kudanganya
Miaka 60 tangu uhuru hamna kitu ilikuwa nafuu wakati wa mkoloni kuliko tulipo sasa
Una uhakika? Endelea kukariri maisha
Screenshot_20230805-180758.jpg
 
Unapeleka maji vijijini,wakati vijiji Hata havija pimwa
Kutopimwa hakuzuii kujengwa Kwa DP za maji.

Ambae anabisha kwamba hakuna Maji amuulize Mbowe alipokuwa kule kwenye Kijiji alichodai Waasi wa Congo wanakuja kuteka wanavijiji ,muulizeni alikuta Maji yanatoka au hayatoki?

Mwisho Tzn ya Leo sio ya Jana
 
Umeme, maji, Shule, hospital, barabara, ni vigumu kuletwa kama mipango miji haijakamilika
 
Kutopimwa hakuzuii kujengwa Kwa DP za maji.

Ambae anabisha kwamba hakuna Maji amuulize Mbowe alipokuwa kule kwenye Kijiji alichodai Waasi wa Congo wanakuja kuteka wanavijiji ,muulizeni alikuta Maji yanatoka au hayatoki?

Mwisho Tzn ya Leo sio ya Jana
Bro ume panic
 
Pato la ndani limeongezeka mikopo nayo imeongezeka maradufu🤔🤔
Watalii wameongezeka dola imeadimika 🤔🤔
Hiyo asimilia 78 ya maji vijijini imefikiwa lini 🤔🤔 au labda vijiji vyote ninavyo vijua havipo kwenye hizo asilimia 🤔🤔
 
Pato la ndani limeongezeka mikopo nayo imeongezeka maradufu🤔🤔
Watalii wameongezeka dola imeadimika 🤔🤔
Hiyo asimilia 78 ya maji vijijini imefikiwa lini 🤔🤔 au labda vijiji vyote ninavyo vijua havipo kwenye hizo asilimia 🤔🤔
Soma hapa 👇
Screenshot_20230805-180758.jpg
 
Hichi kilikuwa kipindi cha jiwe, Mzee wakupika data
Wewe ni fala,hata tarehe zinakushinda kusoma.

Kama hizo zimepikwa pakua hizi hapa basi
 
Back
Top Bottom