Bunge la 12: Prof. Kitila: Uchumi wa Tanzania unakua kwa Wastani wa 6% kwa Mwaka ndani ya Miaka 20 iliyopita

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 13, Kikao cha 6, leo Novemba 6, 2023.


View: https://www.youtube.com/live/5b96dhbHqyo?si=pgTrPHJvwGnYJKTO



SPIKA TULIA: WABUNGE MARUFUKU KUZUNGUMZA NA SIMU BUNGENI, HESHIMUNI SEHEMU YA KAZI
Spika wa Bunge, Tulia Ackson amekumbushia katazo lake kwa Wabunge kutakiwa kutozungumza na simu Bungeni wakati mijadala inapokuwa inaendelea ambapo amewataka kuheshimu sehemu hiyo kwa kuwa ni eneo lao la kazi, ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 6, 2023.

Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, akiwasilisha Bungeni Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2024/2025.
3a60b940-23d2-46fc-a049-5a8371cdd17a.jpeg

Amesema tathmini ya muda mrefu inaonesha uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa kiwango cha wastani wa asilimia sita kwa mwaka katika kipindi cha miaka 20 iliyopita. Aidha, uchumi wa Tanzania ulionesha hali kubwa ya ustahimilivu hata katika kipindi cha misukosuko mikubwa ya kiuchumi duniani, ikiwemo wakati wa janga la ugonjwa wa UVIKO - 19 na vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine. 15.

Aidha, katika kipindi cha miaka 20 iliyopita aina ya bidhaa tunazouza nje na nchi tunazofanya nazo biashara zimebadilika sana. Miaka 20 iliyopita tuliuza zaidi mazao ya kilimo wakati sasa mauzo yetu ya nje yanatawaliwa zaidi na mauzo ya madini. Aidha, miaka 20 iliyopita tuliuza zaidi bidhaa zetu katika masoko ya Ulaya, Marekani na Afrika, lakini kwa sasa tunauza zaidi katika masoko ya nchi za Asia (China, India, n.k.), Afrika na Mashariki ya Kati.


PROF. KITILA: UTOSHELEVU WA CHAKULA NCHINI UMEFIKIA 124%
Akizungumza sehemu ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2022/2023 na Robo ya Kwanza ya Mpango wa Mwaka 2023/2024, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema kuna ongezeko la matumizi ya mbolea katika kilimo kwa 46% kutoka Tani 363,599 Mwaka 2021/2022 hadi Tani 531,091 Mwaka 2022/2023.

Amesema hiyo imesababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka Tani 17,148, 290 (2021/2022) hadi Tani 20,402,014 (2022/2023), hivyo utoshelevu wa chakula umefikia 124% ikilinganishwa na lengo la kufikia 130% ifikapo 2025/2026.

PROF. KITILA: VIFO VYA WATOTO NCHINI VIMEPUNGUA KWA 36%
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo amesema “Vifo vya Watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano vimepungua kwa 36% kutoka vifo 67 kwa vizazi hai 1,000 Mwaka 2015/2016 hadi kufikia vifo 43 kwa vizazi hai 1,000 Mwaka 2022.”

Ameongeza kuwa “Idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 Mwaka 2014/2015 hadi kufikia vifo 104 kwa kila vizazi 100,000 Mwaka 2022, ikiwa tumevuka lengo la kupunguza vifo kufikia 180 ifikapo Mwaka 2025/2026. Katika eneo hili tumepiga hatua kubwa sana.”

Idadi ya Watalii imeongezeka kutoka 1,711,625 hadi 3,818,080
Prof. Kitila Mkumbo anasema idadi ya watalii imeongezeka kutoka Watalii 1,711,625 Mwaka 2021 na kufikia Watalii 3,818,080 Mwaka 2022, ikilinganishwa na lengo la kufikia Watalii milioni tano ifikapo Mwaka 2025/2026. Hii imesababisha kuongezeka kwa mapato ya utalii kutoka Dola za Kimarekani bilioni 1.31 mwaka 2021 hadi kufikia Dola za Kimarekani bilioni 2.53 Mwaka 2022, sawa na ongezeko la 93.1%

Kuongezeka kwa fedha za kigeni kutokana na mauzo ya madini kutoka Dola za Kimarekani bilioni 3.1 Mwaka 2021 hadi Dola za Kimarekani bilioni 3.4 Mwaka 2022, na kuchangia asilimia 56 ya mauzo yote ya nje, ikilinganishwa na lengo kuchangia asilimia 50.5 ifikapo mwaka 2025/2026.

Uandikishaji wa Wanafunzi wa Sekondari na Msingi umeongezeka
Anasema "Tumevuka malengo katika uandikishaji wa wanafunzi katika Elimu ya Msingi na Sekondari hata kabla ya kufika mwaka 2025/2026. Kiwango cha uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya msingi kimefikia asilimia 108.5 ikilinganishwa na lengo la kufikia asilimia 100 ifikapo mwaka 2025/2026.

"Aidha, kiwango cha uandikishaji wa Wanafunzi wa Sekondari kimeongezeka kutoka asilimia 47.4 mwaka 2021 hadi asilimia 48.2 mwaka 2022, ikiwa ni zaidi ya lengo la kufikia asilimia 48 ifikapo mwaka 2025/2026."

24810591-6de1-4c73-963b-a0249af82e69.jpeg
Malengo ya jumla ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2024/2025 ni:
Kuendelea kulinda mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano iliyopita.

Kuendelea na juhudi za kujitosheleza kwa mahitaji ya chakula nchini kwa kuendelea kuongeza matumizi ya mbolea, mbegu bora na kilimo cha umwagiliaji.

Kuongeza uzalishaji na uuzaji wa bidhaa (pamoja na huduma) nje ya nchi kupitia sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu na madini.

Kuweka mkazo wa pekee katika kuongeza thamani katika mazao yanayozalishwa kupitia sekta za kilimo, ufugaji, uvuvi, misitu na madini

Kuendelea kuongeza, kuboresha na kuimarisha ubora wa huduma za jamii, ikiwa ni pamoja na elimu, afya, maji na umeme.

Kuendelea kupanua na kuimarisha miundombinu ya usafiri wa barabara, reli, anga, na majini, na utunzaji endelevu wa mazingira.

Kujielekeza kwenye kufungua fursa katika sekta za madini ya kimkakati (critical minerals), uvuvi wa bahari kuu (deep sea fishing), uchumi wa kijani (green economy) na uchumi wa kidigitali (digital economy). Maeneo haya matatu, ni maeneo yanayokamata kasi duniani kwa sasa, na ambayo kwa upande wetu hatujavuna ipasavyo.
 
Wana hasara gani wakati posho ya kukaa kwenye hivyo viti vya kunesa na kiyoyozi ishaingia mifukoni mwao? Kwanini wasipigiane simu na mademu zao nje ya ukumbi wasikilize kamba tunazofungwa watz kuhusu uchumi kukua! 😀😀😀
 
Back
Top Bottom