Prof. Safari ajiondoa CUF; Atafakari pa kwenda!

Ni msomi na mwanasiasa aliyebobea, gud opportunity kwa CHADEMA kumpata huyu....
Amefanya nini huko alikotoka? Ni msomi, msomi wa nini, siasa za vyama vingi?

CHADEMA walishajifunza kutoka NCCR ya Mrema, kwamba ukitegemea individual personalities then you are only as good as the mood of that personality on any given Sunday. Akigombana na mkewe nyumbani akaja kuzua tafrani ofisini chama zima linayumba.

CHADEMA wameshatuma ujumbe wa wazi kabisa, mara nyingi, consistently, when their prima donna personalities zikitingisha viberiti, huwa wanawavua madaraka, hapendwi mtu mmoja mmoja, CHADEMA ni chama cha sera, si personalities.
 
Huyrrrrrrrrrrrrrrrraaaaaaaaaaaaaaaaaayyyyyyyyyyyyyy nasikia raha mie!!!

Karibu sana profesa!!!!!

Hiyo ndiyo safu ya 2015 imeanza!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Chadema hoyeeeeeeeeeeeeee!
 
Mwanachama mwanazuoni wa CUF aliyewahi kupambana na Profesa Ibrahim Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CUF na kuambulia kuzomewa, Profesa Abdallah Safari, amejivua uanachama wa chama hicho na inasemekana yuko mbioni kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

IF TRUE! ITS VERY GOOD!
This guy is very clever, visionary and stubbornly fighting for equality and good direction, which all are not available through CUF, but only CDM.

\Na pia jamaa anajua sana kusoma nyakati, maana CUF wanajua Lipumba na Hamad walishakubali kutokukabiliana hata kama mmojawapo anaingizwa chaka na CCM -kama ilivyo kwa Hamadi kwa sasa, na jambo hili prof Safari hawezi kuendelea kulivumilia.

Welcome Prof, ukae na wakombozi kuiokoa nchi hii ya Maziwa na Asali, ila collective responsibility is CDM's norms and get in track.
 
ni mwanamapinduzi wa kweli na ni mfuasi wa sera za ujamaa za mwalimu,hivyo atakuwa amefika pahala husika na safari ya ukombozi inazidi kunoga,
na akiondoka rasmi ataongea na waandishi wa habari na kuweka kila kitu bayana siku sio nyingi,kwani cuf sio chama cha upinzani tena bali ni pandikizi la ccm.
habari zaidi atatoa yeye mwenyewe akiongea na wanahabari...................:car:
 
Bad timing! Kila mmoja atajua kuwa amenunuliwa na KANISA ili ku-balance mambo kwenye CDM. Atadharauliwa hata na nzi! Asubiri upepo wa udini upungue CDM

Yaelekea humfahamu Prof Safari wewe.
Je alikuwa amenunuliwa na MSIKITI gani wewee ili ku-balance mambo huko CUF?

Pole kwa udini wako. Kwa kifupi, Prof Safari ana mtazamo na misimamo yake. Hanunuliki kihivyo.
 
Uanachama katika Chama chochote ni kama imani fulani. Sasa unapotoka inabidi ubadili imani yako je hili ni jambo rahisi kweli?

Mie kwa mtizamo wangu, mtu akiachia ngazi chama kimoja asikimbilie kingine maana tayari imani aliyokuwa nayo imemtoka bora akae apange mambo mengine. Mie nawaogopa sana watu wa CUF kwa itikadi zao wasije kuingia CDM na kuanza kutuvuruga esp. watu wenye misimamo mikali kama Prof.

Mie ningemshauri ajiunge na wanaharakati kuliko kukimbilia CDM au CCM

Haya ni maoni yangu binafsi na hayana shinikizo kutoka kokote.
 
Professor Safari was in a very wrong part ambacho some positions are untouchable. I can tell you, Seif will never give his position as a Secretary General of the CUF even when he gets another full time job, he will retain his full time job in CUF. Now he has full time job as a first Vice President of Zanzibar, yest He has still remained with his job as a Secretary General of CUF. CUF ina wenyewe, Professor Safari played a very wrong card. I can tell you, hata Julius Mtatiro will be thrown just like James Mapalala, Rwakatware and the likes.
 
Uanachama katika Chama chochote ni kama imani fulani. Sasa unapotoka inabidi ubadili imani yako je hili ni jambo rahisi kweli?

Mie kwa mtizamo wangu, mtu akiachia ngazi chama kimoja asikimbilie kingine maana tayari imani aliyokuwa nayo imemtoka bora akae apange mambo mengine. Mie nawaogopa sana watu wa CUF kwa itikadi zao wasije kuingia CDM na kuanza kutuvuruga esp. watu wenye misimamo mikali kama Prof.

Mie ningemshauri ajiunge na wanaharakati kuliko kukimbilia CDM au CCM

Haya ni maoni yangu binafsi na hayana shinikizo kutoka kokote.
Kwani imani kukutoka inaanza siku unapotangaza kujitoa au kabla ya hapo, mtu akitangaza ujue hiyo ni hatua ya mwisho kabisa inawezekana amekuwa na wazo hilo kwa miaka mingi.
 
KWA TAARIFA NILIZOPATA KUTOKA CHANZO CHA KUAMINIKA PROF SAFARI ATAHAMIA CHADEMA HIVI KARIBUNI
EMBU WADaU TUCHAMBUE CV YA HUYU MWANAZUONI ATALETA NINI CDM?

Profesa Safari alizaliwa June 3, 1951.

Education background:
1972- Secondary,
1979- University of Dar es salaam shahada ya sheria (LLB),
1985- Master (LLM),
1995- (PhD) University of Sussex England.Baada ya kupata shahada hiyo
alibaki England akawa anafundisha,
2000- Alitunukiwa u Profesa.

Work Experience
1972-1974 Matafiti msaidizi katika taasisi ya Institutes of Kiswahili Research
1974-1976 Mhariri katika kampuni ya Tanzania Publishing House
1979-1986 Wakili wa serikali katika wizara ya sheria
1988-1991 Afisa Mtafiti na uchapishaji katika kituo cha Uhisiano wa nje then
Mhadhiri mwandamizi wa sheria katika kituo hicho Nyazifa(Vyeo)
alivyowahi kushika;
1978-1986 Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wa chuo Kikuu cha Dar es
Salaam
1982-1984 Mhadhiri wa sheria university of Dar es Salaam
1983-1986 Mkuu wa Kitengo cha sheria ,wizara ya sheria
1984-1986 Mwakilishi wa wizara ya sheria katika baraza la elimu ya sheria
Africa Mashariki
1990-1991 Kaimu Mkurugenzi wa masomo na program katika kituo cha
mahusiano ya kimataifa
1996-Hadi sasa, Mwenyekiti wa chama cha wandishi wa Vitabu Tanzania
(UWAVITA),pia Mkurugenzi wa Masomo na programu wa kituo cha
uhusiano wa Kimataifa
1999-Hadi sasa, Katibu Mkuu wa Tanzania Center for Conflict Resolution,
also Mkurugenzi wa bodi ya hakimiliki(COSOTA)

Makongamano:
1978-Alihudhuria mikutano kadhaa ya Kimataifa kuhusiana na mambo ya
sheria barani Africa huko Nairobi (All African Law Students Association)
Aidha,amewahi kuhudhuria makongamano mbalimbali yaliyohusu
mambo ya sheria katika sehemu zifuatazo,Africa
Kusini,Sweden,Geneva,Botswana,Uganda na Marekani.

Tuzo alizowahi kupata:
1991-alitunukiwa tuzo iitwayo Ford Foundation Scholarship for Doctor of
Philosophy programme
1999-2001, Shaaban Robert Literary

Maisha yake:
Ameoa na ana watoto wawili.

Kweli huyu jamaa ni kifaa yaani hata Dr.Slaa haoni ndani. Huyu ni potentio Presida hebu tumpokee tumuandae kugombea urais 2015
 
Karibu kwenye dimbwi la mabadiliko..

Karibu chama cha watanzania halisi, wapenda maendeleo na wachukia ufisadi...
 
Bila ya wasiwasi wala shaka anakuja kwa tamaa ileile ya kugombea Uraisi 2015 ,hivyo wale wenye nia ya kugombea kupitia CDM wakae mkao wa kupata mgombea mwingine.:amen:
 
Back
Top Bottom