Prof. Safari ajiondoa CUF; Atafakari pa kwenda!

Watu wengine ovyoooooooo, hata uwezo wao wa kufikiri ni mdogo, sana, Yaani Profesa Safari ANUNULIWE na kanisa ili iweje, ?, kiufupi Kama profesa safari atahamia CDM, litakuwa pigo kubwa sana kwa CUF, watake wasitake.
Hilo ndio tatizo la foolhardy CDM christian supporters, mliodhani hata kuchochea mauji Arusha kungewapa umaarufu! Nasema Prof Safari akihimia CDM itakuwa a minus to CDM, kuna malalamiko mengi (founded kabisa) ya ukanisa ndani ya CDM akijifanya haoni atakuwa kanunuliwa! Waachie wenyewe chama chao!
 
Ni rafiki wa watu wa chini,mtaani kwake utamkuta kaka kijiweni kama jobless na anaongea na watu wa pato la chini kama vile yeye nae ni wa chini.Anafaa kujiunga na vugu vugu la mageuzi CDM.
 
prof. safari karibu cdm kwenye jeshi la ukombozi.ungana na wasomi wenzako katika kutetea taifa na kutafuta uhuru wa kweli
 
Lets all welcome Prof. Safari in CDM - that is a place that suits him much
Welcome Prof.
 
Prof' tunakukaribisha kwa mikono miwili coz tunajua kuwa wewe ni mpiganaji mwenzetu.
Karibu nyumbani kwetu ushirikiane na watu weledi na wenye ahadi zilizo na mashiko kwa mustakabari wa Taifa letu tulipendalo sisi watetezi wa wanyonge na tunaosimama kidete kupigania rasilimali za Nchi hii.
 
Anahitajika na taifa sio CHADEMA pekee.

Ni suala la kimfumo zaidi na mikakati kuwa ni wapi atakuwa "more effective".
 
Profesa Safari ang'atuka CUF
Monday, 17 January 2011 20:12

Sadick Mtulya
ALIYEWAHI kupambana na Profesa Ibrahim Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CUF,
Profesa Abdallah Safari, amejivua uanachama wa chama hicho.

Taarifa ambazo zilipatikana jana na baadaye kuthibitishwa na Profesa Safari, hazikubainisha sababu za kujitoa kwake kwenye chama hicho na kwamba, anapanga kuanika hadharani keshokutwa.

"Pamoja na kwamba zipo sababu za mimi kufikia uamuzi huu, lakini kwa leo (jana) siwezi kueleza chochote zaidi ya kutangaza nimejiondoa CUF,'' alisema Profesa Safari na kuongeza: "Kesho kutwa (Alhamisi) nitatangaza rasmi azma yangu ya kujivua uanachama wa CUF.'' Profesa Safari ambaye ni mwanazuoni aliyebobea kwenye taaluma ya sheria, alijiunga CUF mwaka 2005 na Februari 2009, aliwania uenyekiti na Profesa Lipumba akaambulia ushindi kura sita.

Alisema amefikia uamuzi wake huo kwa utashi wake, bila kushinikizwa na mtu. "Napenda wananchi waelewe kuwa uamuzi huu, nimeufikia bila shinikizo lolote,'' alisema Profesa Safari.

Hata hivyo, Profesa Safari alieleza kuwa pamoja na kung'atuka kwake CUF, ataendelea kuwa mwanasiasa bila kueleza atashabikia chama atakachoshabikia. Uamuzi huo ameufikia ikiwa ni takriban mwaka mmoja na nusu baada ya kuangushwa vibaya kwenye kinyang'anyiro cha uenyekiti wa CUF na Profesa Lipumba aliyepata kura 646.

Kufuatia matokeo hayo, Profesa Safari aliwashtumu wajumbe wa mkutano mkuu kuwa, walimdhalilisha na angeandaa kitabu kueleza udhalilishaji huo. Februari 23, 2009 wakati Profesa Safari akijieleza katika mkutano mkuu wa kuchagua mwenyekiti wa CUF, wajumbe walikuwa wakimzomea na baadaye kumrushia maswali yaliyomtingisha, ikiwamo kumtaka kutaja jina la katibu wa tawi lake. "Nimedhalilishwa; nimezomewa; nimeulizwa maswali ya kipuuzi.

Ule ni uhuni hakuna kitu pale," alisema Profesa Safari na kuongeza: "Wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF wamepotosha na kuharibu maana ya demokrasia ndani ya CUF na kutumia vibaya nafasi hiyo ya kuchagua viongozi." Alipobanwa kueleza iwapo anafikiria kuwania tena nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho, Profesa Safari alisema hawezi na hana nia ya kuwania uongozi wa chama hicho.

Hata hivyo, taarifa ambazo zilikuwa zikisikika ni kwamba, Profesa Safari alikuwa haelewani na uongozi wa CUF hasa baada ya kuhoji taratibu zilizotumika kati ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kusaini mkataba wa siri kuunda ya umoja.
 
Ukweli ni kuwa CUF inaendeshwa kama shamba la Bibi.....halina mfumo wowote ule wa kidemokrasia shirikishi.........................
 
Mwanachama mwanazuoni wa CUF aliyewahi kupambana na Profesa Ibrahim Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CUF na kuambulia kuzomewa, Profesa Abdallah Safari, amejivua uanachama wa chama hicho na inasemekana yuko mbioni kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Hizo nguvu kwa nini zionekanie chadema na sio cuf aliko kuwa kama anazo kweli?
 
Mimi simkaribishi mpaka tumjue-anaweza kuwa ama wa RA/EL/AC au sisisiemu kwenye ngozi ya rangi nzuri??????????!!!!!!!!!!!
 
it is good for diversity within Chadema
Geza Ulole, nakuunga mkono, Divesity hii ni muhimu sana kwa Chadema, haswa wakati huu, kuliko wakati mwingine wowote, ila pia
Prof. Safari ni mbishi na king'ang'anizi. Akiwa CUF hata baada ya kutambua Lipumba ni rais wa maisha wa CUF na mgombea urais wa kudumu wa chama hicho, bado aligombea nae. huu ni ubishi. Zitto alipogombea na Mbowe alijitumbukiza kugombea kiubishi ubishi tuu, lakini aliposhinikizwa kuondoa jina lake, aliywea na alaliondoa, Prof. Safari sio mtu wa kunywea ni mtu wa kukomaa nao. Sasa Chadema wako tayari kwa divesity ya namna hii?.
 
Sikujua kumbe vyama vinafanya usajili eti kununuliwa.ssssssssssssssssssssss....................type
 
i'm waiting for comment from zomba, where is maralia sugu? i'm missing him on JF!!!!!!
 
Hataanzisha ugomvi na Marando?

Never, the guy is good. I knew hawezi kukaa CUF kwa jinsi alivyo threat kwa Lipumba ideologically, non-ufisadi and education wise. but natilia shaka affiliations zake za udini udini
 
KWA TAARIFA NILIZOPATA KUTOKA CHANZO CHA KUAMINIKA PROF SAFARI ATAHAMIA CHADEMA HIVI KARIBUNI
EMBU WADaU TUCHAMBUE CV YA HUYU MWANAZUONI ATALETA NINI CDM?

Profesa Safari alizaliwa June 3, 1951.

Education background:
1972- Secondary,
1979- University of Dar es salaam shahada ya sheria (LLB),
1985- Master (LLM),
1995- (PhD) University of Sussex England.Baada ya kupata shahada hiyo
alibaki England akawa anafundisha,
2000- Alitunukiwa u Profesa.

Work Experience
1972-1974 Matafiti msaidizi katika taasisi ya Institutes of Kiswahili Research
1974-1976 Mhariri katika kampuni ya Tanzania Publishing House
1979-1986 Wakili wa serikali katika wizara ya sheria
1988-1991 Afisa Mtafiti na uchapishaji katika kituo cha Uhisiano wa nje then
Mhadhiri mwandamizi wa sheria katika kituo hicho Nyazifa(Vyeo)
alivyowahi kushika;
1978-1986 Mwenyekiti wa Chama cha wanasheria wa chuo Kikuu cha Dar es
Salaam
1982-1984 Mhadhiri wa sheria university of Dar es Salaam
1983-1986 Mkuu wa Kitengo cha sheria ,wizara ya sheria
1984-1986 Mwakilishi wa wizara ya sheria katika baraza la elimu ya sheria
Africa Mashariki
1990-1991 Kaimu Mkurugenzi wa masomo na program katika kituo cha
mahusiano ya kimataifa
1996-Hadi sasa, Mwenyekiti wa chama cha wandishi wa Vitabu Tanzania
(UWAVITA),pia Mkurugenzi wa Masomo na programu wa kituo cha
uhusiano wa Kimataifa
1999-Hadi sasa, Katibu Mkuu wa Tanzania Center for Conflict Resolution,
also Mkurugenzi wa bodi ya hakimiliki(COSOTA)

Makongamano:
1978-Alihudhuria mikutano kadhaa ya Kimataifa kuhusiana na mambo ya
sheria barani Africa huko Nairobi (All African Law Students Association)
Aidha,amewahi kuhudhuria makongamano mbalimbali yaliyohusu
mambo ya sheria katika sehemu zifuatazo,Africa
Kusini,Sweden,Geneva,Botswana,Uganda na Marekani.

Tuzo alizowahi kupata:
1991-alitunukiwa tuzo iitwayo Ford Foundation Scholarship for Doctor of
Philosophy programme
1999-2001, Shaaban Robert Literary

Maisha yake:
Ameoa na ana watoto wawili.
 
Mwanachama mwanazuoni wa CUF aliyewahi kupambana na Profesa Ibrahim Lipumba kwenye kinyang'anyiro cha kugombea nafasi ya mwenyekiti wa CUF na kuambulia kuzomewa, Profesa Abdallah Safari, amejivua uanachama wa chama hicho na inasemekana yuko mbioni kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.

Karibu sana Prof. zingatia tu zile kitu zetu , our rules of the game in the Party
 
Mimi simkaribishi mpaka tumjue-anaweza kuwa ama wa RA/EL/AC au sisisiemu kwenye ngozi ya rangi nzuri??????????!!!!!!!!!!!

Usiwe na mashaka nae, angekuwa kibaraka wa ccm wasingemnyima mkataba wa kuendelea kufundisha chuo cha diplomasia pale kurasini, huyo wamemfanyia kama alivyofanyiwa profesa Baregu na Tido Mhando. ila amechelewa sana kusoma alama za nyakati. mwenzake marando ndio alikuwa na perfect timing.
 
Profile:

Back
Top Bottom