Prof. Kabudi: Sheria mpya za madini hazitahusu migodi inayoendelea

Eti msema ukweli ni mpnz wa Mungu, huenda huwa anamaanisha mungu wa usukumani. Kwa maigizo haya ipo siku hata zile akili mfu za Lumumba zitagundua dreva wa Lori lao ni Tazeze
 
Sasa kama sheria hazihusu mikataba ya nyuma, na ndipo raslimali nyingi zilipo, hii sheria wamemtungia nani?? Na kwa nini ziwe za hati ya dharura? Nimechoka na hii serikali. Sjui niende nchi gani
hivi kuna madini tena yaliyobaki?!!!!!
twende zetu msumbiji ndg'angu, naona kidogo wanajielewa....
 
HEbu acha kujitoa fahamu wewe!
Wapi huko ambako kuna madini mengi kama kwenye hiyo migodi inayoelekea kuisha?
Wapi ambako wanataka kuanza kuchimba haraka kiasi kwamba kutulazimisha tusaini sheria kwa hati ya dharula?
Mkuu watu wa Lumumba ni wazma kimwili ila kifikra ni maiti....asikupotezee muda huyo
 
Mikataba iliyoingiwa kipindi cha nyuma haitaguswa"

Yale maandamano ya kumpongeza Mkuu Nchi nzima yamefikia wapi? Sasa Makinikia tumeyazuia kwa nini kama yanabebwa as per previous terms and conditions?
 
Akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali ya wajumbe wa Kamati ya Madini ya Bunge,Prof.Kabudi amesema kwamba sheria huanzia pale ilipotungwa kwenda mbele na sio kurudi nyuma. Akifafanua swala hilo waziri anasema kuwa mikataba iliyokwisha ingiwa kipindi kilichopita haitaguswa na sheria mpya ya madini. Waziri ameongeza kuwa kutafanyika majadili na makampuni hayo kuona jinsi ya kuweka mambo sawa.

Hivyo sheria mpya ya 2017 itahusu kampuni zitakazofuata.

Hii inamaana kuwa migodi mikubwa kama Geita,Buzwagi,Mwadui,Tarime itaendelea kuibiwa kwa sababu ina mikataba tayari ambayo imeingiwa na CCM

Mjumbe wa kamati Mh.Mnyika ameomba kuwa kama base ya sheria mpya ya madini ni ripoti ya makinikia basi ripoti hiyo wapatiwe wabunge ili waone kama recommendations za Kamati ya Makinikia zimezingatiwa. Akijibu swali hilo Kabudi amejibu kwamba ripoti hiyo ni ya Mh.Rais hivyo haitatolewa kwa mtu yeyote

My Take
Namuelewa sana Tundu Lissu mpaka naumia. Lakini kama mnasema ripoti za makinikia ni za rais kwa nini mlitutangazia kila mkoa kujitokeza kwenye TV kumtazama rais?si ilimaanisha ni ripoti ya wanananchi walioibiwa?
Dah! hii nchi kila Rais anayeingia madarakani naye anatafuta "ULAJI"! "Eti mabadiliko haya hayahusu mikataba ambayo tayari ilishaingiwa" Jamani haya ndiyo maneno ya Professor wetu tunayeambiwa ni mbobezi wa sheria!, Mfano rahisi ukimpangisha mtu kitalu chako basi hutakiwi ku-review hata kiwango cha kodi unachotoza. Kwa muktadha huu tayari tumeshajua JPM na Acacia wameshamalizana kimyakimya. Zile zilikuwa ni kelele tu za kutafuta "chake". Wahenga hawakukosea waliposema "Wajinga ndiyo waliwao" WANA LUMUMBA MPOOOOO nyie endeleeeni kutoa lugha chafu wakati tupo kwenye kapu moja
 
HEbu acha kujitoa fahamu wewe!
Wapi huko ambako kuna madini mengi kama kwenye hiyo migodi inayoelekea kuisha?
Wapi ambako wanataka kuanza kuchimba haraka kiasi kwamba kutulazimisha tusaini sheria kwa hati ya dharula?
Wewe unajifanya mjuaji wakati hujui kitu alafu upo kwenye mode ya kubisha, so hata nikikuelezea, will not make sense, unajua kuna helium mining itafanyika Tz, na IPO pending kuna uranium etc. Unajua kwanini Mwalimu Nyerere alijenga uwanja wa kia lile eneo, mind you ni karibu sana mererani, same geology. Mambo ni mengi, hii nchi kubwa sana and it is still virgin.
 
Duh! Wewe lazima utakuwa mojawapo katika washauri wa Rais! Kwa hiyo unaunga mkono mikataba yote ya madini tuliyoingia, yaendelee hivyo hivyo kwani ni asilimia 4% ya akiba yetu. Kwa nini basi tunalilia makinikia...je hayo makinikia ni asili mia ngapi ya akiba yetu? Kutetea ujinga pia kunahitaji ujasiri, ujasiri usio wa kawaida unaopatikana tu katika viwanja vya Lumumba.
Angalia kwanza bandiko langu nilikuwa najibu nini,ndio maana mnafeli kwa uwezo wenu mdogo wa kuchambua mabo
 
Maajabu ya Tanzania,sheria ya bodi ya mikopo imetungwa mwaka jana lkn inawahusu waliohitimu vyuo vikuu kuanzia mwaka 1994 na wanakatwa asilimia 15 badala ya 8 waliyosaini.Hii ya madini yenyewe inaanza kuanzia ilipotungwa kwenda mbele hairudi nyuma na haitayahusu makampuni ambayo yanaendelea na uchimbaji!Hivi inaingia akilini kweli?wanasheria humu jukwaani saidieni kunielewesha hapa
Subili rais wa wanyonge JPM atakuja kukuelimisha mkuu!!
 
Kama ndiyo hivyo, dharula ya nini? Kama sheria MPYA itahusu migodi mipya ambayo kwa sasa haipo, hati ya dharula INA mantiki IPI?
Yaani sheria MPYA haitukwamui kwenye kuibiwa!
 
Wewe unajifanya mjuaji wakati hujui kitu alafu upo kwenye mode ya kubisha, so hata nikikuelezea, will not make sense, unajua kuna helium mining itafanyika Tz, na IPO pending kuna uranium etc. Unajua kwanini Mwalimu Nyerere alijenga uwanja wa kia lile eneo, mind you ni karibu sana mererani, same geology. Mambo ni mengi, hii nchi kubwa sana and it is still virgin.
Makinikia ilikuwa .nini kama si usanii. Aisee heri uwe mfaidika wa hayo unless .
 
Ilikuwa retrospective kwasababu kipindi hicho serikali ilikuwa inahaha na ukata, wakaona watafute namna. Wakasema potelea mbali, after all wahusika au waathirika ni wajinga tu hawatafanya lolote. Wakakandamizia hapo hapo na wameendelea kukusanya hela zao, just a daylight robbery.
kama ilivyo kwenye kodi za majengo kwenye maeneo ambayo hayatambuliki kisheria za Aridhi na mipango miji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom