Prof Haroub Othman na Shivji ni wachochezi?

Why wananchi wasijue kuhusu katiba mpya??why wameamua kufanya hivyo??nadhani hii nchi itakombolewa endapo watatafanya anythin kuhusu hawa watu sidhani kama wananchi watakubali haya matokeo na kukaa kimya tu....
 
That's what you were told; and what did you find out on your own?

This is ridiculous isn't it?- kwenye Majukwaa tunaambiwa na Waunda Azimio, "usawa", "usawa", then many years later wanatuambia, "si usawa kwa maana vidole havilingani".

You ask me what did I find on my own, I just find that we were duped!, a kind of Animal farm where some animals are more equal than others. this kind of flip flop is destined to fail and this is what happened exactly few years later.

ngoja sasa nikuwekee baadhi ya masharti ya Azimio la arusha then utaona kwamba Azimio la Arusha lilihitaji modification katika kipengele cha Maadili ya Viongozi.

kipengele cha 4 kinasema hivi:

ASIWE NA MISHAHARA MIWILI.
Hii ilikuwa inadumaza, inakwaza mtu mwenye uwezo wa kutumikia kazi mbili kwa ufanisi kujiinua, na kutoa mchango mkubwa kwa jamii!, mathalani kuna ubaya gani daktari Bingwa/kiongozi wa idara kuwa daktari na kuwa lecturer na kisha kupokea ujira kwa kazi zake hizo mbili anazofanya?.

Azimio la Zanzibar lilikuja kuondoa discrepancies kama hizi, sasa badala ya watu kuona kwamba ni modification ya msingi kwa sababu Azimio la Arusha siyo Msahafu, wakaona kwamba eti ni kulipinga Azimio Zima, HIYO SI KWELI. bali hayo ni mabadiriko ya msingi ambayo yalibidi yafanywe kutokana na wakati.

kipengele cha Tano cha maadili ya Kiongozi kinasema hivi.
ASIWE NA NYUMBA YA KUPANGISHA
Hii pia ilikuwa ni kikwazo na unnecessary, kama mimi ni mkulima na mfanyakazi nina kipato halali kwa nini nisiweze kuwa na nyumba na nikaipangisha pia?.
Je kama nina nyumba tupu, au nina nyumba ambayo siitumii yote, je siwezi kupangisha vyumba vilivyobaki?.

Mwisho basi, Azimio ni sera ya Chama, na si Watanzania Wote ni wanachama wa vyama vya siasa, hatuwezi kulilia sera ya Chama labda uwe ni mwanachama wa Chama hicho!. Azimio la Arusha ilikuwa ni sera ya TANU/CCM na wanaCCM walikuwa na haki ya kuibadirisha na kusema kweli hicho ndicho walichokifanya Zanzibar mwaka 91, suala ni kujiuliza je hayo mabadiriko waliyoyafanya ni ya msingi au la?. so far mimi ninaona Azimio la Zanzibar lilikuwa halikwepeki na lilikuwa ni la muhimu sana.

Then angalia kipengele cha Sita kinamdefine Kiongozi ni mtu wa Namna gani?
(6) -Viongozi tunaofikiria hapa ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Mawaziri, Wabunge, wakuu wa Vyama vilivyoshirikishwa na TANU,Wakuu wa Mashirika ya Kiserikali, Viongozi kutokana na Kifungu chochote cha Katiba ya TANU, Madiwani, na Watumishi wa Serikali wenye vyeo vya kati na vya juu(Kwa mujibu wa kifungu hiki kiongozi ni mtu au mtu na mkewe au mke na mumewe).

Siyo tu kwamba kifungu hicho kimekosea katika kumdefine Kiongozi ni nani lakini pia ni unfair, Haiwezekani Mke wangu awe kiongozi anayefungwa na Sharti la kutokuwa na hisa kwenye kampuni, asiwe na nyumba ya kupangisha n.k, halafu na mimi nisiye na interest katika mambo ya siasa nifungwe na vifungu hivyo, hicho kipengele ni unjust!

Je Azimio la Zanzibar lilisema watu wawe mafisadi?, la hasha
Je kuna Sheria za kupinga Ufisadi?-ndiyo zipo
Sasa je Azimio la Zanzibar ndilo lililosema mafisadi wasichukuliwe hatua za kisheria?-hapana

Binafsi mimi ninaona jambo la msingi ni la KATIBA NA SHERIA, weka maadili kwenye Katiba na Sheria KISHA HIZO SHERIA UZISIMAMIE KWELI KWELI hapo ndo utakuwa umekata mzizi wa Fitina, otherwise azimio peke yake bila kulipa msingi wa kikatiba ni rahisi kulifuta/kulivunja.
 
mie sijaelewa msingi wa hii sheria!!!, kwanini serikali haitaki wananchi waelimishwe kuhusu hizi sheria za mabadiliko ya katiba???
Je serikali ina nia ya kuwatengenezea katiba au ina timiza matakwa ya katiba ilimradi ionekane ni mpya???
nadhani katiba itakayopatikana itakuwa ni mbovu kuliko tuliyonayo..
 
JK alidai kuwa eti yeye si dikteta! Hivi hajui kwamba Sheria za Kidikteta huleta udikteta?
 
Hii sheria ya kiccm ni sheria ya kipumbavu kama jinsi walio ipitisha walivyo wapumbavu. Hivi wanadhani wao ni watanzania kuliko watanzania wengine?
 
Niliusikiliza mjadala wote jana nilijifunza mambo mengi sana kuhusu mswada ulopiishwa. Nilimsiki Prof.Issa Shivji akitamka waz kuwa yaliyomo hayatufai. Hapo nilijifunza kitu kimoja tu kuhusu watawala wetu kuanzia waliopendekeza, walioupitisha hadi aliyeusaini kuwa wamelewa madaraka na wametawaliwa na unafiki.
 
Niliusikiliza mjadala wote jana nilijifunza mambo mengi sana kuhusu mswada ulopiishwa. Nilimsiki Prof.Issa Shivji akitamka waz kuwa yaliyomo hayatufai. Hapo nilijifunza kitu kimoja tu kuhusu watawala wetu kuanzia waliopendekeza, walioupitisha hadi aliyeusaini kuwa wamelewa madaraka na wametawaliwa na unafiki.

umeona mbali sana kuliko wao.
 
Hizi aina ya sheria zilitungwa ili kufuatwa lakini zina maumbile ya kuvunjwa.... Na ni kama vile zimeandikwa 'bend here to break'
 
Tanzania nchi yangu,nakulilia!
Akina Prof. shivji wameonesha njia,kwamba sheria mbovu si lazima kuzitii.
Na tuwafuate enyi watanzania!
 
Hizi aina ya sheria zilitungwa ili kufuatwa lakini zina maumbile ya kuvunjwa.... Na ni kama vile zimeandikwa 'bend here to break'

Kwa kweli hii sheria ni vituko, ni kama kutaka kuzima moto kwa petrol. Vichekesho vitakuwa pale hizi kesi zitakapoanza...

I can imagine hakimu akitoa hukumu ::
" Mahakama hii imekukuta mtuhumiwa (Prof Issa Shivji) na hatia kwa kosa la KUELIMISHA UMMA KUHUSU KATIBA MPYA kinyume na sheria namba $%##%# ya CCM.."
 
hii nchi saa nyingine,unaweza kutamani uhame... Kakangu alizaliwa UK zaidi ya miaka 40 iliyopita..alilazimika kuukana wa UK miaka 4 iliyopita. Naamini kuna ambao wangechukua wa UK kama ingekuwa wao! Unafiki mwingi nchi hii..
 
Najiuliza sjui mtikila na akina tundu lisu na legal&human rights centre wako wapi.

Kwa sababu hiyo sheria kama iko ivo inakiuka uhuru wa mawazo ndani ya katiba ibara ya 18.
Na ninavofahamu ibara ya 64(5) ya katiba inasema sheria yoyote inayokinzana na haki za msingi ni batili kwa kiwango cha ukinzano huo..(void to the extent of inconsistence)

Na ibara ya 30(3) inasema mtu yeyote anayedai kuwa haki yake kwa mujibu wa sehemu hiyo ya katiba imevunjwa,inavunjwa,ama iko hatarini kuvunjwa anaweza kwenda kuseek redress mahakama kuu ambayo ndiyo yenye original jurisdiction kwny masuala ya haki za binadamu.

Natambua kuwa mtu yeyote anaweza kufungua kesi kwa misingi hiyo nlotaja hapo juu..na kwa kuwa kwny case km hii yenye public interest na yenye haki za binadamu wote tuna locus standi(haki ya kufungua kesi) bila kuonesha moja kwa moja uhusika wetu ama kuathirika kwetu na sheria hii,sisi kama sisi..refer kesi ya takrima

Lakini kwa sababu ya technicalities involved,gharama na utayari kutolewa kafara-nashauri na ninawaomba akina Tundu lisu na LHRC,NOLA na mashirika mengine ya msaada wakisheria kupetition mahakama kuu wao kwa niaba yetu watanzania kama kweli wana nia ya kusaidia jamii yetu.
Ni hayo tu kwa sasa.
 
Du! mungu wangu sijui ccm wanatupeleka wapi sasa???

Hii ni sawa na kusema wanawashitaki waalimu kwa kuwafundisha wanafunzi mpaka wakaelewa (wakafaulu) maanake watanzania hatutakiwi kuelewa. Tubaki mazuzu tu. ZIDUMU FIKRA ZA JK na CCM yake.
 
sheria hii haina tofauti na sheria za makaburu kule afrika ya kusini zilizozuia wazawa (waafrika) kujadili maovu ya serikali ya makaburu.

kwa waliwahi kuona filamu ya sarafina namkumbuka mwl miss masambuga alipokamatwa na kuwekwa kizuizini kwa kosa la kufundisha "the true history of africa"
 
Daudi Mchambuzi

uko sawa mno mkuu hawa jamaa wanachofanya ni unyan'ganyi wa haki zetu ili linchi ni letu watu wachache wanalimung'unya alafu wanatuzibiti na sheria za kifisadi tusioji hapana hii haikubaliki hata kidogo ''natamani kuwa mdunguaji''
 
Last edited by a moderator:
siamnini kama hii nchi itafika 2015 ikiwa salama!!!

hakuna usalama hapo mkuu jiandae kuchimba mahandaki kuficha vifaranga vyako nguvu ya uma hinahitajika sana wakati huu dr anachelewa sana kutoa amri ama kweli miaka hamsini ya uvumilivu vituko vyote hivyo lakini vita hamna?
 
Back
Top Bottom