Posho za wabunge: Kigwangala on January Makamba

hivi punde mh. Hamis kigwangala ameweka status yake facebook juu ya mh. January makamba:

“mhe. January yusuph makamba (mp, m-cc, mnec) has the following platform ya kuongelea: Bunge, kamati kuu ya ccm, halmashauri kuu ya ccm taifa, sekretariet ya ccm, kamati ya uongozi ya bunge...hivi ni haki na halali kwa yeye na nafasi yake kutoa kauli ya kupinga posho hadharani ilhali ana fursa zote hizi za kuzuia ama kurekebisha? Kama hazitaki hizo posho si angeweza tu kuacha kuzichukua, ama angeweza kushawishi chama na serikali kwamba hazifai na zitolewe ama zisiongezwe! Wenzangu mnaonaje hili! Hivi wana-ccm wenzangu tumerogwa ama?”

zidumu fikra za mwenyekiti
 
Seriousness ya issue inategemea mnaizungunzia wapi. Mkikutana chooni wakati wa kujisaidia, mtakayoyajadili huko no matter how serious they are, yatabaki ni majadiliano ya chooni!.

Yeye ni memba humu na pia ni mfuasi wa fb kama mimi na wewe, yeye kaona hii ni issue inayofit kule fb, unaileta humu ya nini?!. Ili avuliwe nguo na kutembezwa mtupu?!.

Humu watu wanakata issues, kule watu wanauza sura, sasa wewe unaleta issue za wauza kura kwa wakata issue wasioangalia sura!. Si wataipaka ... hiyo sura na kuishia kumchafua!. Fb waachie wauza sura na humu leta za wakata issue!.

Issue haipotezi u-serious wake kama inaongewa vijiweni. Ina maana kuwa wale wanaongea hii ya posho kwenye vijiwe vya uswahilini wanaifa iisue ikose u-serious? Sio watu wote wanaouza sura fesibu. Wako wengi tuu wanaokata issue issue kule. Inategemea marafiki zako mle ni wa aina aina gani. Kama uli-add wa kuuza sura unfortunately hapo utakuwa umeliwa.

BTW kuna watu wengi tuu wanapeleka links za threads za JF kule na zinajadiliwa pia. Kama kule kungekuwa ni "kijiwe" according to your meaning, then watu kama akina Mwanakijiji wasingepeleka threads za JF kujadiliwa mle. Lakini that is not the reason I started this thread.
 
Acha kujipendekeza!! rudi U-Turn mkaongee majungu na washamba wenzako, acha kujipendekeza unatia aibu! Usipende kujioverclassify yourself, hamna mtu yeyote aliyemkandia January, tunamponda Kingwalangwala na useless posts zake.

Kaa pembeni, pisha njia!...... katafute wazungu huko ujione na wewe celebrity.
TOKA HAPA!!! na usirudi tena!!

kwanza mwnamme unafuata nini u-turn kama ww siyo mbeya? mmwanmme wewe utasutwa. kama ni wewe ngeleja basi ujue siku yako inakuja kwa kumchafua shosti wangu mwamvita na kaka yake january na warako feki, heti unanimbia nitoke hapa niende wapi? au na wewe pia unataka mzungu aku cameroon? majitu mingine bwana? Mange yuko Juu na anatisha na mzungu wake msomi, baba Kenzoki, sishangai na wewe pia unatafuta mzungu aku cameroon ili ule celebrity

wivu hilooooo, msonyoooo dandia treni kwa mbele kudadadekiii
 
Hakyanani nyie ccm msipobadilika mtakuwa maroboti hivi karibuni. Mtawaza kama roboti, mtaongea kama roboti, mtatembea kama roboti, mtapiga meza (kule bungeni) kama roboti, na mtafanya kila kitu kama roboti! Chama kinachonyima watu uhuru wa kufikiri na kuongea independently kitageuka kuwa kama roboti very soon.
 
Kigwangala anachemsha ..

Ni wendawazimu kutetea posho ya wabunge..

January yuko sawa, vipi mtu anayezungumza mambo ya msingi akuudhi wewe MP halafu kijana what a shame??
Kumbe huwa mnapinga hoja za msingi kwa vile tu zimeletwa na Chadema unafiki wenu ndio unaanza kuonekana.
 
Kigwangala anachemsha ..

Ni wendawazimu kutetea posho ya wabunge..

January yuko sawa, vipi mtu anayezungumza mambo ya msingi akuudhi wewe MP halafu kijana what a shame??
Kumbe huwa mnabisha hoja za msingi kwa vile tu zimeletwa na upinzani sasa mmeanza kuonyesha unafiki wenu wazi.
 
EMT, kwa nini unaleta issues za kijiweni kwenye serious talk?. Dr. Bagaile ni member humu, angekuwa na serious issue si angepost humu?.

Sasa yeye amepost kule fb kwenye kuimbiana mapambio, kwa nini ulete issues za fb humu au unataka huyu imposter aendelee kuvuliwa nguo humu?!.

Mule mjengoni kuna wabunge watumishi wa watu na kuna wabunge wanaotumikia matumbo yao 'gold diggers'. Utawatambua kwa kauli zao!.
Pasco jadili hoja na si mleta hoja wala sehemu ilikotoka.
 
EMT heshima yako ndugu yangu! @ Pasco Heshima ikurudie mkuu wangu sana!
I like Kigwangala, ila ameteleza kidogo ishu ya posho ni ya Taifa sio ya chama chochote cha siasa ni haki kwa Januari, kusemea popote anapotaka!
 
Yakiletwa mabandiko ya Zitto na Dr.Slaa kutoka Facebook ni hoja ya kujadiliwa JF, likiwa la Kingwangwala ni "habari za kijiweni" !

Kingwangwala yeye anamsimamo gani juu ya posho?
 
Wakati wawakilishi wa wafadhili wetu wanaotupatia sehemu kubwa ya bajeti yetu kama Representative Gabrielle Giffords wa Arizona, USA wanaongelea kupendekeza kupunguziwa mishahara, na Malkia wa Uingereza anapunguza gharama zinazoendana na kuikimu familia yake kutoka hela za walipa kodi wa Uingereza, mpaka kufikia kuzunguka Buckingham Palace akizima taa mwenyewe, sisi nchi masikini tutaona vipi ajabu kuongelea jambo hili?

Utumishi wa umma ni wito, na ingawa mkono mtupu haulambwi hata kwa kazi ya wito, lakini mtumishi wa umma kwa nchi maskini kama Tanzania kuwa na mshahara ulio wa juu sana kulinganishwa na mtumishi mwingine wa umma (mbunge/ mwalimu) kunaleta maswali mengi.

Kulilia mishahara minono sana kwa mbunge kunatupa shaka juu ya nia ya huyu mbunge kwenda bungeni. Je kaenda kupigania wananchi au kuchukua mshahara mnono na marupurupu mazuri?

Gabrielle Giffords: Slash lawmaker pay
Gabrielle Giffords: Slash lawmaker pay - Jonathan Allen - POLITICO.com

Gabrielle Giffords' Office Urges Super Committee To Cut Lawmakers' Pay
Gabrielle Giffords' Office Urges Super Committee To Cut Lawmakers' Pay

Queen Elizabeth II takes a pay cut
Queen Elizabeth II takes a pay cut - NY Daily News
 
Wakuu hata mimi sijaona mantiki ya yeye kwenda kuandika hayo Fesibuku. Si angemtafuta tuu Makamba mwenyewe na kumweleza dukuduku lake? Au kama Kigwangala anaona kuwa Makamba angetumia hivyo vyombo husika, kwa nini yeye (Kigwangala) hakuwasiliana na hivyo vyombo husika kuelezea dukuduku zake? Yaani hapo ni kama anachopinga Mkamba kukifanya, ndicho hasa Kigwangala amekifanya.

Afadhali hata angekuja hapa, lakini anajua hapa watu huwa hawakopeshi, hivyo akaona bora aende FB.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
hivi ni haki na halali kwa yeye na nafasi yake kutoa kauli ya kupinga posho hadharani

Kigs anaonekana ile memo ya "Uwazi" hakuipata, anaendeleza habari za siasa za closed doors. Sasa maana ya mbunge kuwa na Facebook page ni nini kama si kutoa msimamo wake hadharani wananchi wampe feedback? Unataka apeleke hoja kwenye kikao cha bunge kama kamati ya chama mumpige chini kabla hajamaliza sentensi?

ilhali ana fursa zote hizi za kuzuia ama kurekebisha?

This is the age of information, hata kama anapeleka hoja kwenye vikao huko, kitendo cha kutoa msimamo wake kwa Wananchi kinafaa, kaonyesha msimamo wake in principle. Kesho tunaweza hata kumfuata na kumwambia mbunge sasa tunajua hoja yako haijapita, basi kile cha juu tukipeleke kwenye mpango wa maendeleo jimboni. Anayetoa principle na kushindwa kuitekeleza kwa kukosa mandate si sawa na anayetetea usiri.

Kama hazitaki hizo posho si angeweza tu kuacha kuzichukua,

Kuacha kuzichukua ni kususa, na kama kitu si haramu kususa si tija. Unajuaje kama akizichukua hazifanyii kazi ambayo alifikiri inabidi ifanywe na serikali badala ya kuwapa wabunge posho?

ama angeweza kushawishi chama na serikali kwamba hazifai na zitolewe ama zisiongezwe!

Kushawishi chama na serikali kunaanza na kushawishi popular support, ambayo sehemu moja ni Facebook. Mwenzako kashaona this is a popular cause, kwa hiyo yuko tayari kuachia posho ili ajenge capital kubwa ya kuaminika miongoni mwa watu. Wewe na njaa yako unaona posho ndiyo muhimu zaidi ya kuonyesha solidarity na wananchi masikini.

Wenzangu mnaonaje hili! Hivi wana-CCM wenzangu tumerogwa ama?"

Tatizo upeo hapa unaonekana mdogo, kwanza issue tayari ishaangaliwa katika miwani ya chama wakati isue ni ya kiuchumi na inahusisha populism katika nchi ambayo watu wengi hawana chama. Pili wana CCM wengi masikini na ukiwaambia wabunge wapunguziwe posho ama la wengi watakubali wapunguziwe.Tatu Dr. mzima conclusion yako ushirikina shirikina tu.

Hawa ndio wabunge wetu wasomi jamani? Mimi nilitegemea nishushiwe "An Analysis of the Effect of Global Austerity Measures on Parliamentarians Pay ". Complete with Bluebooks budgetary boomerangs.

Ooovyo!
 
Wakuu hata mimi sijaona mantiki ya yeye kwenda kuandika hayo Fesibuku. Si angemtafuta tuu Makamba mwenyewe na kumweleza dukuduku lake? Au kama Kigwangala anaona kuwa Makamba angetumia hivyo vyombo husika, kwa nini yeye (Kigwangala) hakuwasiliana na hivyo vyombo husika kuelezea dukuduku zake? Yaani hapo ni kama anachopinga Mkamba kukifanya, ndicho hasa Kigwangala amekifanya.

Not a January fan here, strictly on the issues.

Bonge la point, umemkamata kwenye axiomatic fallacy. Wanasema umemfunga kwa sheria yake mwenyewe.

Basically anamlaumu January kwa kuzungumza mambo ya ndani nje, wakati huo huo, yeye mwenyewe anavyomlaumu anasema mambo ya ndani nje.

Kama kweli Kigs anaamini katika vikao vya chama kumaliza haya mambo, kwa nini hakungojea mpaka kikao cha chama ndio aende kusema haya, kaja kusema Facebook ?

Baniani mbaya, kiatu chake dawa.

Facebook ikitumika ku rally paycut kwa wabunge vibaya, lakini kushambulia wanao rally behind paycut vizuri.

Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.
 
guys dont forget huyu jamaa alifanya kampeni zake kwa kutumia helkopta ..sasa pesa yake atairudishaje?and it seems that the guy is not planning and he know that he will never win again this post.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Waache wakao kimwaka 47...hawajui nguvu ya social media! nadhani pia ana mawazo ya habari ni hadi zikatolewe ukumbi wa habari maelezo!
 
Tungepata kwanza sifa za FB against JF ndio tungejua kwanin kakimbilia kule.
FB unachagua marafiki wa kuweza kuona status/thread yako, so kama mtu anakupinga unaweza kum-unfriend au kum-block asikuone kabisa ukabaki na wale wa dizaini ya "ndio mzee"
FB unaruhusiwa kuwa na member wasiozidi 5,000 so pumba zozote utakazoandika tegemea kupata upinzani wa maximum watu 5,000 kama wote wakijibu wakati hapa ni zaidi ya mara kumi yake.
FB ipo ki-sura zaidi so hata michango mengine utafikiri watu wapo kitandani wakati hapa ni "nondo" kwa kwenda mbele.
Lakin cha kujiuliza, Kig anamsema January kwa kutotumia vikao halali kupinga posho, yeye hiyo FB ndio kaona ni kikao halali??
 
Back
Top Bottom