Heche: Kama Bodaboda ni Ajira tunawataka Ridhiwani Kikwete na January Makamba wawe Bodaboda!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,137
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema mh John Heche amesema kama Bodaboda ni Ajira tena iliyo nzuri basi tunawataka Ridhiwani Kikwete na January Makamba wawe Bodaboda

Heche amesema Chadema itaendelea kusisitiza kwamba Bodaboda Siyo Ajira

Source: Arusha One Tv

My take: Chadema hubirini na mambo mengine sasa
 
Hoja ya kitoto mno hiyo, hapo ndipo UVCCM inapoiacha BAVICHA na CHADEMA kwa mbali kwenye eneo la kujenga hoja. Heche ni mwepesi mno kichwani kwamba mzee Kikwete na mzee Makamba walipambana ujanani mwao ili na watoto wao waje kuteseka?

Spika Tulia kuna siku alisema alikuwa anauza maandazi baada ya kumaliza chuo lakini akapambana akawa spika. Pia Kuna wengine kwa sababu ya kukabiliana na ukosefu wa ajira wamejiajiri kwenye bodaboda wakitegesha michogo mingine. Unapowaambia vijana wasiwe bodaboda una lengo lipi? Uhalifu, wizi na uhuni uongezeke?
 
Tanzania imegawanyika katika madaraja mbalimbali. Kuna madaraja katika jamii yetu, huwezi kuwakuta watoto wa wakubwa.

Hivyo tukubaliane tu na uhalisia. Bodaboda ni kazi inayofanywa na watu waliokosa fursa nyingine za kujitafutia kipato katika jamii.
 
Karibu vijana wote wa bodaboda Manzese wanavuta bangi.

45% ya waathirika hospital ya mifupa MoI wanatokana na ajali za bodaboda.

Ukiwa unaendesha hizi boxer uwe na bima kubwa ya afya kwani vyuma vya kuunga mifupa ni adimu na ghali sana
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema mh John Heche amesema kama Bodaboda ni Ajira tena iliyo nzuri basi tunawataka Ridhiwani Kikwete na January Makamba wawe Bodaboda

Heche amesema Chadema itaendelea kusisitiza kwamba Bodaboda Siyo Ajira

Source: Arusha One Tv

My take: Chadema hubirini na mambo mengine sasa
Huyu Jamaa ana hoja nyepesi namna hii..... Jamaa ana akili ndogo sana.
 
..Hapo ndipo utakapojua jinsi Ccm walivyo wabinafsi.

..CCM sio chama cha wanyonge tena, ni chama cha mabwanyenye.
 
Maskini mwingine wa fikra huyo hapo

Kweli Tz tutakuwa wa mwisho hata Afrika kwa uelewe na maendeleo
Nchi ya wasiojitambua
Maneno kama haya ya kitoto wala yasingekuwa yanaandikwa

..watu hawataki kuachia misafara ya ma-V8.

..bodaboda, na machinga, ni matokeo ya sera mbaya za uchumi za Ccm.

..ni bahati mbaya kwamba Ccm wanataka kuuaminisha umma kwamba bodaboda ni mafanikio wakati sio.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema mh John Heche amesema kama Bodaboda ni Ajira tena iliyo nzuri basi tunawataka Ridhiwani Kikwete na January Makamba wawe Bodaboda

Heche amesema Chadema itaendelea kusisitiza kwamba Bodaboda Siyo Ajira

Source: Arusha One Tv

My take: Chadema hubirini na mambo mengine sasa
Hawa ndio viongozi wakuu wa chadema wenye mawazo kama haya.INASIKITISHA
 
Back
Top Bottom