Posho na Mishahara ya wabunge...

Hawa watu wa CCM sijui wako vipi,hawana malengo na ustawi wa nchi hii!Wanaila ikiisha wanapotelea ughaibuni!Shame on them!
 
Ni wazi sasa Bunge limekuwa kimbilio la kila anaetaka Utajiri wa Haraka. tatizio hapa sio kutumikia wananchi au Kuonekna kama mkuu ktk Jamii bali ni kimbilio la Kutafuta posho kubwa sana huku kazi inayofanywa ni ndogo sana na haindenai na Kipato cha kazi ya yenyewe.
Ikiwa Leo Prof anaesomesha Chuo kikuu hupata Robo tu ya Posho ya Mbunge aliefika F4 au F6 ni wazi taifa linapoenda sipo.
Wabunge wawe wazalendo. waangalie maslahi ya taifa. waangalie umaskini wa Watz.
Kwa hapa naungana na Chadema na wale wote wanaotaka wabunge waondoshewe POSHO.
nchi maskini, wabunge matajiri.
hospital hakuna dawa. Wabunge wanakoga pesa.
Shule hakuna madawati. wabunge wanachota mapesa.
Walimu wanakimbia kusomesha. wabunge wanauana wanataka nafasi ya kwenda kuchota pesa bungeni.
Polisi hawana vitendea kazi. Wabunge wanaenda kuvuta mshiko mkubwa bungeni
maskini unaengezeka. wabunge wanatanua Mijengoni.
Wanafunzi wanakosa Ada. wabunge wanasomesha watoto wao nje ya nchi
Ikipita miaka 5 tu. mbunge huwa billionea. lkn mwanajeshi mkuu huambulia pesa za Chai na Chakula cha Jioni.
NI WAZI SASA WABUNGE WA CCM TUANGALIE TAIFA BADALA MTU BINAFSI
Na subiri Masa aje akugongee li Thanks...Lol
 
Kuna haja ya mabadiliko yakaanza kwa mtu mmoja mmoja kubadilika.Operation vua gamba ianze pia kwa wabunge wa ccm kuisimamia serikali yake hasa katika suala la matumizi ya fedha za umma.Pia na wao wakatae posho ambazo zinamfanya bibi angu aliyeko kule kamachumu kukosa hata ambulence moja ya kumkimbiza hospitali pale anapozidiwa au mjukuu wake anapotaka kujifungua.Lets change our minds tanzabians !
 
Wanahofu kule bungeni wananchi watawaona wakipinga hatua hii na itazidisha hasira za wananchi dhidi yao

Welawelaaaa,umewadia mda wa wazee wa ndioooo kula kwao tena maana CDM watakuwa wanachomeka wao wanapinga kila jambo la CDM...spika akijifanya anaweka mambo sawa atawahoji na wao bila kujua watasema ndioooo,kwa namna hii CDM tutakuwa tunafunga magoli hata kwa kutambaa na bunge hili lefu CDM tunatarajia kufunga magoli ya kutosha sanaaaa

Naomba CCM waendelee kupinga hoja za CDM ili izidi kula kwao.,baadae utamsikia Manyanya anasema 'mh.spika CDM wanalidharau bunge lako tukufu...wachukuliwe hatua za kinidhamu' jamani labda Tanesco watunyime kabisa umeme vinginevyo tutarajie kuona taarabu za akina Cheyo,Ahmad,Bulaya,Kigwangwala n.k


CDM fanyeni kama kawaida yenu,teamwork,courageous,confidentl.ALL THE BEST CDM!!
 
Watanzania tumekuwa watu wa ajabu sana. Namshangaa mtoa mada anamwita Zitto mnafiki. Ningekuona wa maana kama ungempongeza kwanza then ungeshauri njia bora za matumizi ya hizi pesa, sio kumkejeli. Lazima tukubali kwamba this is a step in the right direction. Inaonekana kwako unaona ni sawa tu, tena kuna wabunge wengine useless hata michango huwa hawatoi, kazi wanayofanya ni kula posho tu.
 
Ukijua mchezo wa wanasiasa utakuwa unataka kujua kwa nini kwa kila jambo wanalofanya kabla ya kutoa maelezo. Politicians wengi wanafanya mambo kwa ajili ya public populality. Najua watanzania wengi ni watu wa matukio. Leo Zitto katoa hii basi wamesahau hata kufikiri kabisa zaidi ya kupongeza tu. Nauliza Zitto amekuwa bungeni kwa muda gani? Ana kiasi gani mpaka sasa kwenye akaunti yake? Ameshibaa?
 
kuna watu ni vijana lakini wanazeeka kimtazamo kama huyu bibi,
166588_172760082761015_100000810726317_328362_4539846_n.jpg
 
Wanasiasa wanawageuza wananchi kuwa wajinga, na bahati mbaya tunaponzwa na ushabiki wa vyama. Akishasema kiongozi wangu wa chama ni sahihi hakuna kuquestion.

Ukisoma Habari Leo, ya leo Mbowe anasema Shangingi lake (V8) hawezi kuacha kulitumia sababu tayari kashapewa, anasahau katibu wake (Dr.Slaa) alivomshambulia W/Mkuu kuwa anatumia gari la kifahari.
Na kwa nini ruzuku za vyama zisivutwe, wanachama ndio wachangie vyama vyao? Tunapoteza pesa nyingi kwa vyama ambavyo mi naona wengi ni kunufaisha viongozi wa vyama vya siasa. Hili hawataki kabisa.
Ukiangalia kwa undani unaona kuwa hatujawa na viongozi wenye nia ya dhati. Wengi ni makelele ya kutafuta umaarufu na kuchumia matumbo yao.
 
Source gazeti huru la Mwananchi.

MBOWE ASEMA NI WIZI WA KITAASISI,MKULO AWAANDALIA MTEGO CHADEMA

WAKATI Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiunga mkono hoja ya Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe ya kutaka kufutwa kwa posho za vikao kwa wabunge na watumishi wote wa umma, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo amesema anasubiri hoja hiyo itakapowasilishwa bungeni.Mbowe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kikao cha ndani cha wabunge wa chama hicho alisema hoja ya kufutwa kwa posho siyo ya Zitto peke yake na kwamba mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini anasakamwa bure kwa kudhaniwa kwamba anatafuta umaarufu wake binafsi.

Wabunge wa CCM na Chadema jana wakuwa na vikao vya ndani kwa ajili ya kuweka mikakati ya kujadili Bajeti Kuu ya Serikali, iliyowasilishwa bungeni Jumatano iliyopita. Mjadala wa bajeti unatarajiwa kuanza rasmi Jumatano ijayo.

Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni alisema posho zinazotakiwa kufutwa ni kwa watumishi wote wa umma ambao wamekuwa wakilipwa fedha za vikao hata wanapokuwa katika mazingira ya kutekeleza wajibu wao wa kila siku.

"Tumekokotoa na tunaendelea kukokotoa na inaelekea tunaweza kuokoa hadi kiasi cha Sh900 bilioni ikiwa posho zote zitafutwa, hili linawezekana kama tutakavyoonyesha katika bajeti yetu mbadala tutakayowasilisha Jumanne ijayo," alisema Mbowe.

Mwenyekiti huyo wa Chadema alisema wabunge wamekuwa wakilipwa mishahara kwa mwezi pamoja na fedha za kujikimu (per diem) wanapokuwa nje ya majimbo yao kikazi na kwamba wanachopinga ni "posho za vikao" (sitting allowance) ambazo ni kikwazo cha utekelezaji wa kazi za Serikali na majukumu mengine katika ofisi za umma.

Alisema utoaji wa fedha za vikao uliasisiwa na Bunge na umesambaa taratibu katika taasisi nyingine za umma na kusababisha watendaji kutunga semina na vikao vingi alimradi wanapata posho huku kazi nyingine zikiendelea kulala.

"Kwa mfano, mimi ni mjumbe wa Kamati ya Uongozi (ya Bunge), nasaini 'sitting allowance' katika kikao cha Bunge, nikiitwa katika kikao cha kamati ya uongozi nasaini tena sitting allowance na hata kama kutakuwa na kikao kingine jioni naweza kulipwa, sasa kama huo siyo wizi ni nini?"

"Huu ni wizi wa fedha za umma ambao umetaasisiwa na sasa unaathiri utendaji katika mfumo mzima wa serikali, si fedha tu kwani hata kazi zinalala kwani watendaji wote wanakimbilia kwenye vikao vya kutunga kwa sababu kuna posho na si vinginevyo."

Alisema hoja si malipo ya posho kwa wabunge wa Chadema pekee, bali kwa watumishi wa nchi nzima ambao ni zaidi ya 500,000 na kwamba malipo ya posho hizo yamesababisha kuwepo kwa tofauti kubwa ya kipato baina ya watu walioko kwenye menejimenti na watumishi wengine.

"Hawa wakubwa, wakurugenzi na wakuu wa idara wanapokutana kwenye vikao vyao na kulipana posho, tujiulize madereva na wafagiaji wanakutana lini na wanalipana nini? Haya ndiyo mambo yanayoleta chuki katika utendaji kwani wengine wanakuwa matajiri huku wengine wakibaki mafukara," alisema.

Alisema pamoja na kwamba wabunge wa Chadema akiwamo yeye wanachukua posho hizo, kamwe hawataacha kusema kwani tatizo si wao kuchukua, bali sera inayoruhusu ufujaji huo wa mali ya umma.

Mbowe alisema kama suala ni mishahara midogo hilo ni jambo linalozungumzika na kwamba Serikali inaweza kujenga hoja na kuipandisha kwa kiwango kitakachowezesha watumishi wa umma wakiwamo wabunge kujikimu, lakini si kuweka posho ambazo zinawanufaisha wachache na kujenga matabaka miongoni mwa watumishi wa umma.

Alisema katika bajeti yao mbadala watatoa mapendekezo magumu ambayo watendaji wa serikali hawajazoea kuyatekeleza na kwamba ikiwa hoja zao zitakataliwa, watakuwa wametimiza jukumu lao ndani ya Bunge.

"Wao ni wengi, wanaweza kukataa hoja hizi ndani ya Bunge, lakini sisi tunafanya siasa ndani na nje ya Bunge, sasa kama wao ni wengi kuliko hao walioko huko nje basi tutajua," alisisitiza.

Kauli ya Mkulo
Mapema Waziri Mkulo kwa upande wake alisema: "Nawasubiri ndani ya Bunge, kwa sababu waziri kivuli ni ndani ya Bunge, sasa kama wakileta mapendekezo hayo mimi nimejiandaa tayari maana huu ni unafiki tu."

Mkulo aliyewasilisha Bajeti ya Serikali bungeni siku tatu zilizopita, alisema ikiwa wapinzani watabeba ajenda hiyo, basi atawaandalia fomu kwa wale wasiotaka posho ili wakajaze na fedha hizo zipelekwe kwa wahitaji wa misaada mbalimbali.

"Nitakapohitimisha hatua yangu nitawaandalia fomu kwa Katibu Mkuu Hazina na nitawaelekeza kama hawataki posho hizo basi wakajaze fomu tuone kama kuna mtu atakayekwenda," alisema Mkulo na kuongeza kuwa kauli ya Zitto ni ya kutafuta umaarufu usiokuwa na msingi.

Alisema Zitto si mkweli kwani mapendekezo ya posho za vikao hupitishwa na kikao cha Kamati ya Uongozi ambacho pia huwashirikisha wapinzani na kwamba kiasi cha Sh70,000 kwa siku wanacholipwa wabunge kilipitia katika mfumo huo unaowashirikisha wapinzani.

"Sasa huu ni mchezo wa ajabu, maana kule wanakaa wanapitisha halafu huku mtu anageuka na kusema hataki," alisema Mkulo.

Akizungumzia tamko la Zitto kuhusu madai ya upotoshaji katika bajeti, Mkulo alikiri kwamba kulikuwa na makosa katika suala la faini ya Sheria ya Usalama Barabarani na kwamba mabadiliko aliyoyasoma hayakuwa yamechapishwa kwenye vitabu kutokana na marekebisho kufanywa dakika za mwisho.

"Tulipokea ushauri wa polisi kuhusu suala hili na baada ya Cabinet (Baraza la Mawaziri), kupitisha mabadiliko hayo tulipeleka taarifa Ofisi za bunge, sema tu kwamba vitabu vilikuwa vimeshachapishwa," alisema.

Kuhusu fedha zilizotengwa kwa ajili ya umeme, Waziri huyo alisema si kweli kwamba hakutakuwa na miradi mipya kama Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alivyodai katika taarifa yake, bali alisema fedha nyingi zimewekwa Hazina badala ya kuwekwa katika wizara za kisekta kutokana na masharti yaliyotokana na jinsi zilivyopatikana.

"Kwa mfano hata fedha za Millenium Challenge Account (MCA), kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya kule Sumbawanga, haziko kwenye akaunti ya Wizara ya Ujenzi, haziwezi kuwa huko kwani masharti yake hayaruhusu, sasa watu hawa jamani wasome Bajeti na maelezo mengine ya ziada," alisema Mkulo.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema ni mapema kuzungumzia hoja ya Chadema kuhusu posho, lakini akaahidi kwamba anasubiri hadi itakapowasilishwa rasmi bungeni na upande huo wa upinzani.

"Si vizuri nikaanza kujibizana na mbunge mmoja mmoja, lakini kwa sababu wamesema wataileta kama kambi ya upinzani hapo itakuwa hoja rasmi, tusubiri wakati huo," alisema Ndugai.


My take:Good movie chadema magamba watapinga sana lkn mmeonesha njia kwa watz kuwa mnachokisema ndicho mnachokisimamia kwa vitendo. Iwapo kweli mmeamua kuwa wamoja tena katika hili. Najua mmefanya sadaka kwa niaba wa mamilioni ya watz ambao ni hoehae. Kama nchi zote kubwa duniani wanazungumzia kubana matumizi sie tunaohitaji misaada kutoka kwao tunamatumizi ya kijinga kama haya sidhani kama wanatuelewa.
 
Tangu uchaguzi hadi leo tumeshuhudia mengi hadi tunashindwa kushika lipi. Tuacheni sasa akili zetu zitulie tufikirie na kuchambua bajeti
 
Eti posho ya Wabunge haitoshi????!!!! Hiki ni kichekesho coz, posho wanaopewa kwa siku ni Mshahara wa Mtu kwa Mwezi mzima....sasa hawa wabunge wetu kama hawako Bungeni kuyawakilisha matumbo yao wao wanafikiri wanamuwakilisha nani???Hivi hawa wabunge wanajua kuna watu wanalazimika kula saa kumi na mbili jioni coz, wanakose hela ya kununu mafuta taa???? Hini ninyi wabunge mnajua kuna watu wanakunywa uji usio na sukari na si kama wanafuata taratibu za kiafya la hasha ni kuwa hawana hela ya kununulia sukari??? Acheni kufikiri kwa kutumia matumbo...Tumieni kichwa nchi hii ni yetu sote kama kuna hali ngumu basi tuisikie wote.
 
mjadala unaoendelea sahv itv kasema kunamambo mengi ya kusema kwautajili wa nchi yetu na si vposho vdogo wakati matrilion mapesa yanapotea kwawawekezaji
 
Tangu uchaguzi hadi leo tumeshuhudia mengi hadi tunashindwa kushika lipi. Tuacheni sasa akili zetu zitulie tufikirie na kuchambua bajeti

mkuu in the model world you head should be multi-task hata simu siku hizi ni multi-task hacha uvivu
 
hiyo form ya mkullo anayosema imekaa kichama zaidi kuliko kiserikali kama anapitisha form iwe kwa wabunge wote na mimi ninavyoiona ccm ya mpasuko kuna wengi tu wanaimwaga hiyo posho.
lakini pia kwa sababu ni ya wabunge wa chadema wao ndio wanapaswa kuhamua itumikeje kijamii ili jamaa ijue hiyo pesa imetoka wapi ?
huyu jamaa ni wa kutupia rwanda wakamtie adabu anadharau sana
 
Back
Top Bottom