Polisi yajitakasa isishitakiwe ICC kwa kuua

PMNBuko

JF-Expert Member
Dec 27, 2010
967
154
Tokea Jana Usiku tumeshuhudia Jeshi la Polisi likituonesha picha za video kuhusu tukio la Arusha, Januari 5 mwaka huu ambapo Mtangazaji wake anaonesha umma kwamba CHADEMA wanahitaji kulaumiwa kwa kuchochea vurugu. Taarifa hii imeacha maswali mengi kichwani mwangu bila majibu.

Je, kwa nini jeshi lisitaje sheria inasemaje kuhusu kuzuia maandamano muda mchache kabla ya maandamano kuanza?

Je, kwanini Jeshi la Polisi liue watu badala ya kutumia mabomu ya machozi na virungu kama ilivyozoeleka?

Wana JF nani anawajibika kwa vurugu za Arusha? Wananchi wanaweza kugeuza mawazo na maoni yao kutokana na taarifa ya Jeshi hilo linalojaribu kujisafisha kwa kutumia gharama kubwa za fedha za walipakodi ambao ndio baadhi yao wameuwawa na Jeshi hilo?
 
Polisi hawawezi kukurupuka tu kwenda kuuwa. Kwanini husemi ni nani aliamrisha maandamano? Kwa nini husemi ni nani aliamrisha kundi la watu waende polisi wakitokea kwenye mkutano wa chadema? Au yote hayo huyajui?
 
Zomba acha ushabiki,maandamano ni haki ya msingi ya wananchi na cdm kama chama cha siasa,na cdm walikuwa na barua waliyokubaliana na polisi njia ya kupita iliyosaniwa na OCD,IGP hana mamlaka kisheria wala kipolisi,na pia ni uhuni na wendawazimu IGP kupiga marufuku maandamano kwenye vyombo vya habari badala ya kuandika barua kwa cdm.,Pili cdm walitembea zaidi ya km 3 ndipo polisi waakanza kutumia risasi za moto kuwatawanya,,Tatu kwenda kuchoma kituo cha polisi ni uzushi maana utachomaje kituo wakati viongozi wakuu wa cdm wapo ndani?taarifa ya jana imechakachuliwa ili kujisafisha,ila ukweli una tabia moja ya kujitetea na katika hili time will always determine the truth
 
Polisi hawawezi kukurupuka tu kwenda kuuwa. Kwanini husemi ni nani aliamrisha maandamano? Kwa nini husemi ni nani aliamrisha kundi la watu waende polisi wakitokea kwenye mkutano wa chadema? Au yote hayo huyajui?

Zomba kama unaweza kuangalia Euro news!(leo).nadhani utaona umuhimu na faida ya maandamano.Vile vile utaona jinsi gani polisi wanavyosaidia ili hayo maandamano yawe ya utulivu.
 
zomba ni mnafiki na kibaraka wa mafisadi na ccm, hata kama watu wangeandamana bila kua na kibali hakuna sheria yeyote inayowaruhu polise kuwashambulia waandamanaji kwa risasi za moto wakati waandamanaji hao hawana silaha. Kazi wanayo hata wachakachueje habari wananchi tayari wanaujua ukweli na jeshi la police limesha jiharibia reputation yake kwa wananchi.
 
Polisi hawawezi kukurupuka tu kwenda kuuwa. Kwanini husemi ni nani aliamrisha maandamano? Kwa nini husemi ni nani aliamrisha kundi la watu waende polisi wakitokea kwenye mkutano wa chadema? Au yote hayo huyajui?

The example of Tunisia shows that authoritarian regimes promise only a false sense of stability.
 
Polisi hawawezi kukurupuka tu kwenda kuuwa. Kwanini husemi ni nani aliamrisha maandamano? Kwa nini husemi ni nani aliamrisha kundi la watu waende polisi wakitokea kwenye mkutano wa chadema? Au yote hayo huyajui?

Mauaji ya raia kwasababu mbalimbali hayajaanza Arusha. Zipo sheria ambazo kama polisi wangeziheshimu na wanaoomba kuandamana nao wangeziheshimu. Sasa polisi wanajipa madaraka ya kuamua either wakubali au kukataa maandamano bila sababu ya msingi.
Huko ndiko kulikopelekea watu kuchukua sheria mkononi. Jamani Tanzania inabadilika. Enzi za kuendesha mambo kwa mikwala na mizengwe ziko mbioni kupita zake.
Polisi wa leo ni tool za kuwalinda wanasiasa wababaishaji badala ya wananchi walio wengi. Ipo mifano mingi tu ambayo inalitia doa jeshi la polisi jinsi linavyoweza kusimamia sheria. Kwani ile issue ya Mbeya nayo ikoje? polisi walikuwa hawajui mahangaiko ya wale wanakijiji dhii ya the so called mwekezaji aliyekuwa anajipendelea?
Nakuhakikishia kwa hili la Arusha, loser ni jeshi la polisi hata wafanye propaganda gani. Ndio maana nafikiri polisi ya sasa ijengwe na watu wenye uwezo wa kufikiri na kusimamia sheria. Enzi za yes afande tu zimepitwa na wakati.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, kimeelezewa kuandaa mashitaka dhidi ya Serikali katika Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia Makosa ya Jinai (ICC), kutokana na kusababisha mauaji ya raia watatu wasio na hatia akiwemo raia mmoja wa Kenya yaliyofanywa hivi karibuni na Jeshi la Polisi huko mkoani Arusha.

Pia chama hicho kimepanga kuifikisha na kuishitaki serikali kwenye Jumuiya ya Ulaya EU, iwapo haitawajibika kumfukuza kazi kama Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema, atashindwa kujiuzulu mwenyewe kutokana na kashfa hiyo.

Aidha, CHADEMA kinasema vielezo muhimu wanavyo zikiwemo picha za video na ushahidi wa wazi unaonyesha mauaji hayo yalikuwa na baraka kutoka kwa viongozi wa ngazi ya juu ya serikali ambao ndio waliomshauri Kamanda Mwema kuzuia maandamano hayo muda mfupi na kusababisha ghasia na mauaji hayo.

Tamko hilo limetolewa juzi na Mkurugenzi wa Oganizesheni wa chama hicho, Ignas Karashani, wakati akizungumza na waandishi wa habari kulaani mauaji hayo.

My take: Serikali isipuuzie hatua hii ya Chadema inaweza kuiweka serikali kwenye image mbaya kimataifa.
 
wana uzoefu wa kutosha kudeal na mamabo kama haya, si waliwahi kushtakiwa na cuf akama sikosei baada ya mauaji yale ya pemba? ni busara tu ndizo zitakazoepusha hili. lets wait & see
 
Zomba zomba,zomba,,,usishabikie uhalifu huu dhidi ya binadamu,,,utalaaniwa,,,kuna wengi walipigwa risasi zaidi ya km 3 kutoka eneo la mkutano,na kituo cha polisi,kama umetumwa shauri yako laana na damu zilizomwagika bure zitakuwa juu yako,,,
 
Jamani naomba kujua ukweli je wale waliopigwa risasi ni kweli walipigiwa risasi polisi kituoni? au niulize je ni hao wawili ndio waliokuwa wamekwenda kuvunja kituo kuondoa viongozi wa chadema? Je wote waliopigwa huko mabarabarani walikuwa wanavamia kituo cha polisi? Na je kweli polisi wetu wanadhani kama watu wote waliohudhulia mazishi wangekwenda kituoni kuwaondoa viongozi wao wangeshindwa kwa sababu ya bunduki za polisi? Naomba kujua hili plz!
 
wana uzoefu wa kutosha kudeal na mamabo kama haya, si waliwahi kushtakiwa na cuf akama sikosei baada ya mauaji yale ya pemba? ni busara tu ndizo zitakazoepusha hili. lets wait & see

Bahati mbaya image ya cuf ilikuwa questionable mbele ya Jumuiya ya Kimataifa, ie kilikuwa na element za ugaidi! Kwa cdm mambo tofauti kabisa, ccm wasipokuwa makini JK ataachia ikulu kabla ya 2015 kama rais wa Tunisia!
 
Kama sheria na taratibu za ICC zinaruhusu, hii ni golden opportunity kwa CHADEMA.
 
Kama sheria na taratibu za ICC zinaruhusu, hii ni golden opportunity kwa CHADEMA.
Mara nyingi huwa nawaambia wachezaji wangu keep the ball away from your penalty area, acha wao wa-defend kuliko wewe ku-defend. Nimeona wameanza kujitetea kwa kuchakachua picha TBC 1 wakidhani itasaidia, labda ingekuwa zamani enzi za magazeti ya Uhuru na Mfanyakazi na RTD tu lakini leo hawamdanganyi mtu.
 
occampo hawezi kuhongwa? Any way kama wana vielelezo ni bora kuwashtaki ili ukweli uonekane. huz
 
Polisi hawawezi kukurupuka tu kwenda kuuwa. Kwanini husemi ni nani aliamrisha maandamano? Kwa nini husemi ni nani aliamrisha kundi la watu waende polisi wakitokea kwenye mkutano wa chadema? Au yote hayo huyajui?

Nilifikiri wewe ni ZOMBA kumbe jina lako litamkwe bila "M" between
 
Polisi hawawezi kukurupuka tu kwenda kuuwa. Kwanini husemi ni nani aliamrisha maandamano? Kwa nini husemi ni nani aliamrisha kundi la watu waende polisi wakitokea kwenye mkutano wa chadema? Au yote hayo huyajui?

uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo?
 
Kama sheria na taratibu za ICC zinaruhusu, hii ni golden opportunity kwa CHADEMA.

Golden opportunity ya kuafanya nini? kujitangaza kimataifa au? this is shit! EU wanashindwa kusimamisha mauaji ya halaiki palestina yanayofanywa na israel, waje kuisaidia CDM? you are not serious! hao EU una waona wasafi?

sana sana kuwaomba wasitoe misaada yao kwa TZ wataadhirika watanzania wote including wana CDM na hata sikumoja EU haiwezi kupindua serikali ya TZ! wala haitawapa umaarufu mnaofikiria.

ICC ndio kabisa haita saidia chochote maana kama wa kufungwa ni Dr. Slaa, maana amri katoa yeye watu wakavamie kituo cha police. wacha waende yetu macho kwanza CDM watafundishwa namna ya ku control mobs zao.
 
Back
Top Bottom