Polisi wafanye kazi yao ya kupambana na Wahalifu Dar

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
Maeneo haya Dar hatari kwa uporaji

Wenyewe wakikuona kama hujaambulia kibao cha kukupumbaza, utatishiwa na silaha ili utoe ulicho nacho.

Watu hao bila kujali ni asubuhi, mchana au jioni, wamekuwa wakipora na wakati mwingine licha ya kukupora bila kujali kama kuna wapita njia wengine eneo husika, huendelea na shughuli zao badala ya kukimbia kama ilivyozoeleka.

Kundi kubwa ambalo limetajwa kulizwa na waporaji hao ni wanawake kutokana na udhaifu walio nao na mara nyingi vibaka huamini pochi wanazobeba hazikosi chochote.

Vibaka hao wamekuwa wakitumia viwembe, visu, bisibisi, kamba au kumpiga mhusika kwa lengo la kumtisha atoe alicho nacho. Sambamba na silaha hizo, bodaboda pia hutumika katika kufanikisha uhalifu huo.

Maeneo ambayo yametajwa kukithiri vitendo vya uporaji katika wilaya ya Ilala ni Majumba Sita njia panda ya Segerea, Tazara, Msimbazi Centre, ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Coco, Daraja la Salendar, barabara ya Ocean na Majani ya Chai, Lugoda.

Kwa upande wa Kinondoni ni Tanganyika Parkers kuelekea ufukwe wa bahari Kawe, Makuburi, Kinondoni Mkwajuni, kituo cha daladala cha Mwenge, Tandale kwa Mtogole, Mwananyamala A na Mwananyamala kwa Mama Zakaria, maarufu kama mahakama za simu.

Katika wilaya ya Temeke, wananchi wanayataja maeneo ambayo ukipita lazima ukabwe na kuporwa ulicho nacho kuwa ni mataa ya Chang’ombe, BP Kurasini, Temeke Maguruwe, pori la kiwanda cha Bia ambako kuna maficho ya wahalifu na Mbagala Kiburugwa ambako ni maarufu kwa mbwa mwitu. Lipo pia eneo la kati ya Mbagala Kizuiani na Zakhem.

WANANCHI WATOA YA MOYONI
Mkazi wa Kawe Mzimuni, Salum Ali, akizungumza na Nipashe, alisema eneo la Tanganyika Packers limekuwa likitumiwa na kundi la vijana wenye nia ovu ambao wamekuwa wakijificha kwenye vichaka vilivyoko huko kuwapora wapita njia.

Alisema vibaka hao wakati wote wamekuwa wakikaa kwenye vichaka hivyo wakivuta bangi na mara wanapomwona mtu anapita, humfuata na kumkaba.

“Hili eneo lote ni hatari kuanzia kiwanda cha Tanganyika Parkers hadi ufukweni Kawe, mtu ukikatiza tu, wenyewe wakikuona wanakukaba tena wanakwambia tupe mali zetu, yaani utafikiri walishiriki kununua,” alisema.

Anaongeza: “Hawa vibaka hawapori ovyo wakiwa mafichoni wanakutathmini kwanza wewe ni mwenyeji wa eneo hilo au ni mgeni. Wakikubaini ni mgeni, wanakufuata kukutishia na silaha kama kisu, bisibisi, viwembe ili uogope na kutoa uliocho nacho,” alisema.

Aidha, alisema matukio mengi hutokea eneo hilo siku za Jumamosi na Jumapili kwa kuwa watu wengi ambao ni wageni hutumia eneo hilo kama njia ya mkato kwenda ufukweni kwa ajili ya mapumziko.

“Wanaoporwa wengi ni wageni ambao hupita hapa kwenda ufukweni siku za mwisho wa wiki. Njia hii ni fupi ikilinganishwa na hii ya lami, ukibahatika kupita salama mchana na ukarudi salama jioni unatakiwa kumshukuru Mungu.

“Mimi mwenyewe yaliwahi kunikuta. Kuna siku nilikuwa napita kwenda Mji Mpya ulioko nyuma ya kiwanda hiki, ilikuwa jioni. Ghafla nikapigwa na ubapa wa panga, kugeuka akaniambia mshikaji mbona unazingua unapitaje hutoi taarifa kama ni mwenyeji.

Yaani hii ndiyo ilikuwa salama yangu na bahati nzuri kwa sababu nalijua sana eneo hili, sikuwa na chochote mfukoni, basi aliniachia niendelee na safari yangu,” alisema.

ASKARI ASIMULIA
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) (jina linahifadhiwa) aliiambia Nipashe kuwa, siku moja alipita eneo hilo na kukutana na kundi la vijana ambao walikuwa wamekaa kwenye moja ya vichaka na walipomwona walimfuata na kumzingira.

“Nilikuwa napita eneo hili kwenda Mji Mpya ambako ndugu zangu wanaishi. Bila kujua kama pale kuna vibaka, nikiwa na pochi yangu ndogo, nilipofika eneo la Tanganyika Parkers na ilikuwa mchana, nilishtukia vijana wamenizingira na mmoja wao alitoa kisu na kunikaba nacho shingoni aliniumiza kwa kweli. Wakati huyu akinishikilia, wenzake waliniambia niwape mkoba niliokuwa nimebeba.

‘Kabla sijapewa nafasi ya kujitetea, kijana mwingine ambaye alikuwa amesimama mbele yangu aliivuta pochi niliyokuwa nimebeba, wakanivua viatu na vitu vingine nilivyokuwa navyo wakavichukua kisha wakaondoka,” alisema.

Askari huyo alisema wakati tukio hilo likitokea, licha ya kupiga kelele za kuomba msaada kwa watu waliokuwa jirani na hapo, hakuna aliyejitokeza kusaidia.

“Niliishia kuibiwa pochi ambayo ndani yake kulikuwa na biblia, simu yangu, kitambulisho cha kazi na cha mpigakura na hela kidogo iliyokuwa kwenye pochi,” alisema askari huyo.

Ofisa Mtendaji wa Serikali za Mtaa Kawe Mzimuni, Keneth Mazanda, aliliambia gazeti hili kuwa matukio hayo yamekuwa yakijitokeza eneo hilo na kwamba kwa kushirikiana na kikundi cha ulinzi shirikishi cha Mji Mpya na cha waendesha pikipiki, waliwaomba wawe wanapita mara kwa mara eneo hilo.

“Kama unavyofahamu eneo hili ni mali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na ni kubwa limejaa vichaka. Jumamosi iliyopita wananchi tulilazimika kwenda kulifyeka kupunguza maficho ya wahalifu. Ombi langu kwa NHC waongeze walinzi kwa sababu waliowaweka hawatoshi na wawe wanafyeka vichaka vilivyopo,” alisema.

Aidha alitaja maeneo mengine hatari kuwa ni Ufukweni, Nyara, Jeshini Makaburini ambapo vikundi vya waporaji hujificha huko.

NJIA PANDA SEGEREA
Fatuma Athumani mkazi wa eneo hilo alisema kuwa kituo cha mabasi cha njia panda ya Segerea licha ya kuwa karibu na kituo cha polisi, vibaka wamekuwa wakipora vitu mbalimbali, zikiwamo simu za mkononi za abiria na waenda kwa miguu.

“Sitasahau siku moja nilikuwa natoka mjini nimeshuka kwenye kitu hicho. Ilikuwa saa mbili usiku, nilishtukia nimepigwa kibao cha nguvu usoni na mtu aliyekuwa nyuma yangu, kabla sijageuka nilishtukia simu, pochi vyote havipo, yaani hawa watu wanakera wanakuibia simu ya Sh. 500,000 wanaenda kuuza Sh. 50,000,” alisema.

Kondakta wa daladala inalofanya kazi zake Makumbusho -Temeke, Musa Hamisi, alisema mataa ya Chang’ombe (makutano ya barabara za Nyerere na Kawawa, jirani na VETA), abiria wengi hususan wanawake wamekuwa wakilizwa simu zao na vibaka ambao wamekuwa wakipita kwenye foleni.

“Wakishagundua una simu halafu umeiweka holela au unaongea, utashanga uliyekuwa unaongea naye kwenye simu anabaki hewani huku simu ikinyakuliwa na kibaka. Wakiiba hawakimbii sana, anatoka nje ya barabara anaendelea na mishe (mambo) yake,” alisema.

Frank Joseph, mkazi wa Gongo la Mboto, alisema wiki iliyopita akiwa kwenye daladala amekaa kiti cha mwisho, alipofika eneo la Tazara majira ya jioni, simu yake iliita na dakika chache wakati akiendelea na mazungumzo, alishtukia amevutwa shati na mtu aliyekuwa nje na alivyogeuka simu yake iliporwa.

“Yaani ilikuwa kama sinema vile maana eneo hili nalijua lina vibaka kwa hiyo wakati naongea na simu nilikuwa nimekaa siti ya nyuma dirisha la kulia na nilikuwa naongea kwa kutumia sikio la kushoto nikiendelea kuongea shati langu lilivutwa na kitendo cha kugeuka kuangalia aliyefanya hivyo, simu ikaibwa,” alisema.

Alisema licha ya kupiga kelele za mwizi hakuna aliyejishughulisha kumfukuza ili kumkamata.

MKUU WA MKOA ANENA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, alisema mkoa wake umejipanga ipasavyo kukabiliana na vitendo vyote vya kihalifu, wakiwamo vibaka.

Akizungumza wiki moja iliyopita, wakati akikagua upandaji wa miti katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi, Makonda alisema uko mkakati wa kupambana na uhalifu kwa kusogeza huduma za polisi maeneo yanatajwa kuwa ni hatari.

“Juzi tu eneo la ufukwe wa bahari wa Coco tulikamata watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na ukamataji huu ni endelevu kwa sababu tunataka jiji la Dar es Salam liheshimiwe na wahalifu,” alisema.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, aliliambia gazeti hili kuwa wamekuwa wakiwakamata wahalifu mara kwa mara kupitia operesheni zinazofanyika mitaa mbalimbali lakini sheria zilizopo zimekuwa zikiwapa fursa ya kuendelea kuishi mtaani.

“Tunawakamata tunapeleleza na kubaini wana makosa. tunawapeleka mahakamani na kwa sababu makosa wanayokutwa nayo yana dhamana, wanadhaminiwa na kurudi tena mtaani na kuendeleza uhalifu,” alisema .

Aliongeza kuwa: “Mkakati endelevu tulio nao ni kuendelea kufanya doria ya magari na pikipiki ambazo zimekuwa zikipita maeneo mbalimbali ili kuhakikisha usalama wa mali na wananchi unakuwapo,” alisema.

Pia alisema mkakati huo unahusisha mpango unaotekelezwa na ofisi ya Rais kwa kushirikiana na jeshi la polisi wa kuweka vituo vinavyohamishika kwenye maeneo ambayo yamekithiri vitendo vya uhalifu. Mpango huo kwa sasa unatekelezwa katika mkoa wa kipolisi wa Ilala baada ya kukamilika Kinondoni.

“Tunaamini vituo hivi vitatusaidia kutoa taarifa za uhalifu kwenye vituo vikubwa ili wahusika waweze kukamatwa, lakini niwahakikishe wananchi namna tulivyojipanga hakuna maeneo mkoani Ilala ambayo hayapitiki kwa sababu ya vibaka,” alisema.

Hata hivyo, alipotakiwa kutoa takwimu za matukio ambayo yamewahi kuripotiwa polisi, alisema yako machache kwa sababu changamoto iliyopo wengi wanaoporwa hawaripoti polisi.

Chanzo: IPP Media
 
Na si kuvaa vizubao kukimbiza na bodaboda na kukama motor vehicle za magari
 
Kupambana na uhalifu ni jukumu la kila mmoja ukiwemo wewe mtoa bango.Polisi waliopo ni wachache kuliko mahitaji halisi.
Hivi wakati ule wanaanfamana na mavifaa mbalimbali huku wakitamba kuwa wako tayari kwa fyoko fyoko yoyote wewe ulikuwa wapi?
Hilo neno hawatoshi ni lako lakini wao wanasema wako kamili lakini kwa maandamano tuu!
 
Kupambana na uhalifu ni jukumu la kila mmoja ukiwemo wewe mtoa bango.Polisi waliopo ni wachache kuliko mahitaji halisi.
Ilo linafahamika kua ulinzi ni wetu sote ila awa jamaa hawana ushilikiano na ss wanajiona wao miungu mtu na ss tunawaacha ila tunawakumbusha to yakiwafika hapa!!! Ndo wanaanza oooh!!! Nijukumu letu sote
 
Ilo linafahamika kua ulinzi ni wetu sote ila awa jamaa hawana ushilikiano na ss wanajiona wao miungu mtu na ss tunawaacha ila tunawakumbusha to yakiwafika hapa!!! Ndo wanaanza oooh!!! Nijukumu letu sote
Hilo lisikuvunje moyo na likakufanya uache wahalifu watambe mtaani.
 
Mkuu BAK

Tatizo hili ni kufanya mambo kisiasa. Miezi michache iliyopita askari walikuwa na mazoezi ya kupambana na uhalifu kwa mujibu wao.

UKUTA ilipokwisha na mazoezi yakaisha. Jambo la kujiuliza, nini tija ya mazoezi yale?

Je, tatizo la wananchi ni mikutano ya kisiasa au hali inayotisha kaa ilivyoandikwa?

Pili, mkuu wa mkoa yupo bize akipanda miti.
Laiti lingalikuwa jambo la kisiasa leo tungesikia matamako na mbwembwe za kila aina.

Ni huyu mkuu wa mkoa aliwaambia Polisi wachukue hatua bila kusbiri amri wakati wa UKUTA.

Leo nashindwa kuwaambia askari wachukue hatua bila amri kwa vibaka na majamabazi

Unaweza kuona kwanini tuna feli mambo mengi. Viongozi wana interest zao si za public.

Mambo ya siasa yanawagusa watatumia kila resource kukablina nayo, baada ya hapo mengine kama haya ni by the way

Hizi habari za tumejipanga n.k. ni maneno mbadala ya tumeshindwa

Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama si mwenyekiti wa mazingira

Kipaumbele chake ni usalama wa wananchi si kupanda miti

Huku ndiko kufeli kwenyewe.
 
Wakisikia mikutano ya wanasiasa ndio utawaona ,

mbwe mbwe kibao na vitisho vya kila aina,

wakati mtaani watu wanatobolewa Macho.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ahsante sana Mkuu Nguruvi3, nakubaliana nawe katika yote uliyoyaandika kuhusu polisi kujihusisha zaidi na masuala ya kisiasa kuliko kupambana na uhalifu nchini.

Siku zote kuna polisi wa kutosha kupambana na wanasiasa ambao wanafuata katiba ya nchi kufanya kazi zao ikiwemo kufanya mikutano na maandamano sehemu mbali mbali nchini, lakini wakati huo huo kunakuwepo na "upungufu mkubwa" wa polisi inapokuja kwenye kupambana na wahalifu ambao huwaweka wananchi roho juu kwa kutishia usalama wa mali zao na hata uhai wao.

Mkuu BAK

Tatizo hili ni kufanya mambo kisiasa. Miezi michache iliyopita askari walikuwa na mazoezi ya kupambana na uhalifu kwa mujibu wao.

UKUTA ilipokwisha na mazoezi yakaisha. Jambo la kujiuliza, nini tija ya mazoezi yale?

Je, tatizo la wananchi ni mikutano ya kisiasa au hali inayotisha kaa ilivyoandikwa?

Pili, mkuu wa mkoa yupo bize akipanda miti.
Laiti lingalikuwa jambo la kisiasa leo tungesikia matamako na mbwembwe za kila aina.

Ni huyu mkuu wa mkoa aliwaambia Polisi wachukue hatua bila kusbiri amri wakati wa UKUTA.

Leo nashindwa kuwaambia askari wachukue hatua bila amri kwa vibaka na majamabazi

Unaweza kuona kwanini tuna feli mambo mengi. Viongozi wana interest zao si za public.

Mambo ya siasa yanawagusa watatumia kila resource kukablina nayo, baada ya hapo mengine kama haya ni by the way

Hizi habari za tumejipanga n.k. ni maneno mbadala ya tumeshindwa

Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama si mwenyekiti wa mazingira

Kipaumbele chake ni usalama wa wananchi si kupanda miti

Huku ndiko kufeli kwenyewe.
 
Huko tena ndiyo usiseme Mkuu, lakini utaona unafiki wa huu uhakiki maana huko hawataguswa kwa kujua fika moto utakaowaka nchini baada ya wengi kufukuzwa kazi kwa kuwa na vyeti fake.

Na uhakiki wa vyeti ukianza jeshini polisi watakuwa wachache zaidi.
 
Ahsante sana Mkuu Nguruvi3, nakubaliana nawe katika yote uliyoyaandika kuhusu polisi kujihusisha zaidi na masuala ya kisiasa kuliko kupambana na uhalifu nchini.

Siku zote kuna polisi wa kutosha kupambana na wanasiasa ambao wanafuata katiba ya nchi kufanya kazi zao ikiwemo kufanya mikutano na maandamano sehemu mbali mbali nchini, lakini wakati huo huo kunakuwepo na "upungufu mkubwa" wa polisi inapokuja kwenye kupambana na wahalifu ambao huwaweka wananchi roho juu kwa kutishia usalama wa mali zao na hata uhai wao.

Mkuu usipime, polisi wengi ndiyo wamiliki wa magenge ya uhalifu, ninakumbuka hapa hapa JF kuna mkuu alileta thread ya kueleze jinsi alivyoibiwa, asubuhi alikwenda kituoni kufungua jalada, anasema hakuamini sauti ya polisi aliyekuja kumhoji ni ile iliyokuwa ikitoa mwongozo usiku, aliishiwa nguvu na kumwambia atarudi kuna dharura anaiendea.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom