Polisi wafanye kazi yao ya kupambana na Wahalifu Dar

Mkuu tuarudi pale pale.

Hili halijagusa masilahi ya siasa na wanasiasa, hakuna anayejali.

Leo wakisikia ACT au CUF wanafanya mkutano utasikia serikali nzima iNaacha kazi na kzungumzia amani na utulivu. Hivi hawa wananchi wanaoteseka namna hii wana amani na utulivu gani

Katika hili si waziri, si mkuu wa mkoa si Polisi anayesimama na kusema hali ni mbaya sana

Kuna kundi jingine la wanafiki na hapa nimualike ndugu yangu Kiranga ambaye amelikomalia kweli kweli, teh teh teh

Hili ni kundi la watu wanaoitwa viongozi wa dini.

Majuzi wakati wa UKUTA tumewasikia wakizungumzia amani na utulivu.

Waliunda kamati n.k. Hawa wanaishi huko mitaani na wanayaona haya, kwa unafiki wa kundi hili hakuna anayeiambia serikali kuna tatizo mitaani, hali inatisha! hakuna ! si jambo la siasa hili hawana masilahi

Halafu utawasikia kwenye vilinge na madhabahuni wakihubiri amani na utulivu
Viongozi wa dini wanaamini amani na utulivu ni kuzuia mikutano ya siasa!

Wao wanasubiri intelejensia iseme kuna mkutano jangwani, basi utawasikia wakihangaika utadhani mikutano ya siasa ni tatizo.

Intelejensia inayobaini uvunjifu wa amani kwa vyama vya siasa na ambayo imefeli kupambana na vibaka!

Watu wanaumizwa, hakuna anayejali kabisa! watu wanaishi kwa hofu hakuna anayejali
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nguruvi3

Tuna mchanganyiko wa mmomonyoko wa maadili, ukosefu wa elimu, umangimeza na ubinafsi na kuendekeza maigizo zaidi ya vitu vya msingi, pamoja na vingine vingi.

Kuna muongezeko wa tofauti kati ya walio nacho na wasio nacho kiasi cha kufanya makundi mawili haya kama hayaishi katika nchi moja. Mtu mwenye kampuni ya Ulinzi yenye makao makuu Uingereza inayomlindia kasri lake Oysterbay ataweza vipi ku identify na matatizo ya Waswahili wa kwa mfuga mbwa huko?

I remember back in the days, natoka kanisani na mshua Jumapili, mshua kakutana na Waziri wake Mzee Mustapha Nyang'anyi kwenye mataa ya Salendar Bridge. Mshua akawa anampungia, anasema yule Waziri wangu. Mzee Nyang'anyi anampungia back, alikuwa na Rahma in the back seat, kwenye Volswagen Beetle. Waziri huyo, so down to earth kama mtu wa kawaida. Leo hii hawa wanasiasa wamejipaza na kujilimbikizia privileges to an absurd level. Waziri mmoja wa Afrika alienda Sweden, akawa hosted na Foreign Minister wa Sweden kwenye flat ya Foreign Minister. Wamekaa wanakunywa vinywaji, Waziri wa Afrika akamuuliza nyumba yako iko wapi? Waziri wa Sweden akashangaa, akasema hii ndiyo nyumba yangu, hapa ndipo kwangu naishi. Waziri wa Afrika akashangaa, akasema hii si guest house tu ya kupokea wageni? Akaambiwa hapana, hapa ndipo naishi. Waziri wa Afrika alipaona simple sana. Hapo utaona anayesaidiwa anafanya anasa kuliko mtoa msaada.

Huku kwetu tumekaa kibinafsi zaidi. Watu wanajali chama zaidi kuliko maslahi ya nchi. Katika chama hicho nacho kuna makundi. Mtu kama Kikwete amepata urais kwa kujipendekeza na kujionesha mtoto mzuri zaidi ya uwezo wa kuongoza, no wonder amekuwa disaster. Na yeye sasa watu wanamuona afadhali kwa namna fulani kwa sababu tuliye naye sasa hata anapotaka kufanya mazuri anayafanya kwa jazba na bila mipango kiasi cha kuharibu matokeo na mchakato.

Uongozi unahitaji humility. Uongozi unahitaji inclusivity. Uongozi unahitaji tactful strategies. Uongozi unahitaji genuine compassion. Uongozi unahitaji clarity of thought. Sio kupiga wapinzani tu, wapinzani ni sehemu ya sauti inayotakiwa kusikilizwa ili kuendesha nchi. Moja ya sababu zilizotufanya tuchelewe kwenye maendeleo ni kuwepo na kikundi kidogo cha watu kinafanya maamuzi ya watu wengi sana bila hata kuwa na wajibu wa kiukweli kwa wananchi hao. Mtu anasaini kkataba wa mamilioni ya dola na makampuni ya kimataifa, wakati hapo huo mkataba ni siri, mkataba kuwa siri tu ni mwanya wa rushwa. Kwa nini tunafanya siri? Mpaka World Bank tunayoilaumu kama chombo cha ukandamizaji siku hizi wanasema mikataba ya siri haitakiwi na ni mwanya wa rushwa, kwa nini sisi bado tunaikumbatia?

So many things to say right now.
 
Mkuu Nguruvi3

Ninakubaliana kwa kiwango fulani katika angalizo lako lakini pia kumbuka ulinzi unaanzia ndani ya familia zetu.

Badala ya kuanza kulaumu polisi, ingefaa kwanza kuangalia kwa upana malezi ya hao watenda maovu.

Kama kuna broken families/society usitegemee polisi wanaweza kumaliza hilo tatizo hata kama wanatenda kile ambacho unakisema kwa sababu broken families/society ni kiwanda cha kuzalisha watoto ambao wanakuwa wezi au majambazi ya kesho.

Ni sawa na kujaribu kuzuia madawa ya kulevya kwa kumatama wauzaji au watumiaji wakati mashamba au viwanda vya kuzalisha vikiwa vinaendelea kuzalisha.

Tatizo ninaloliona hili suala unaliangalia kwa kutumia macho ya matokeo badala ya kutumia macho ya chanzo.

Kama mmonyoko wa maadili utaendelea kuzalishwa kuanzia kwenye familia tusitegemee polisi wanaweza kumaliza hili tatizo la vijana kujiingiza kwenye kazi za wizi au ujambazi.
 
Kupambana na uhalifu ni jukumu la kila mmoja ukiwemo wewe mtoa bango.Polisi waliopo ni wachache kuliko mahitaji halisi.
Wewe unapingana na Mh Raisi? Alisema police wapo wa kutosha kabisa, tena kasema police jamii waondolewe kabisa. Hali ni mbaya sana huku kwetu MJOMBA, maeneo yote ya kipunguni, machimbo, Moshi bar, Kwamkoremba, KWA Diwani, bomba mbili, KWA Mpemba nenda hadi Chanika ni hatari sana hasa KWA wageni wanaohamia na kufungua biashara ni lazma wasulubiwe na nao vibaka, tena wanakuvamia Kundi kubwa hata majirani hawazubutu kutoka ni shida sana, kesho LA police wanabidi wafanye juhudi za maksudi haraka sana kinyume cha hapo KWA kweli hali inazidi kuwa mbaya kila siku.
 
Wewe unapingana na Mh Raisi? Alisema police wapo wa kutosha kabisa, tena kasema police jamii waondolewe kabisa. Hali ni mbaya sana huku kwetu MJOMBA, maeneo yote ya kipunguni, machimbo, Moshi bar, Kwamkoremba, KWA Diwani, bomba mbili, KWA Mpemba nenda hadi Chanika ni hatari sana hasa KWA wageni wanaohamia na kufungua biashara ni lazma wasulubiwe na nao vibaka, tena wanakuvamia Kundi kubwa hata majirani hawazubutu kutoka ni shida sana, kesho LA police wanabidi wafanye juhudi za maksudi haraka sana kinyume cha hapo KWA kweli hali inazidi kuwa mbaya kila siku.
Watashughulikiwa utoe ushirikiano km ulivyoutoa hapa JF
 
Mkuu Kiranga
Kuna vitu ukiviangalia unajiuliza hivi sisi Waafrika tuna matatizo gani?

Hatuonekani kujifunza au kuwa na mitazamo tofauti

Nikikumbuka miezi miwili, polisi walitangaza hali ya usalama mbaya.

Tuliona wanasiasa wakikamatwa, kuwekewa mabango yakionyesha umri na makosa yao. Ilikua na maana gani? kwanini tusione vibaka wakitendewa hayo?

Kwamba mwanasiasa ni mhalifu sana kuliko vibaya!

Walisema wana taarifa za kiintelejensia kuhusu jambo kadha wa kadha
Leo wanaomba ushirikiano kwa wananchi! intelejenesia iko wapi?

Ukiangalia ngazi zote za uongozi zilikuwa zinafoka utadhani dunia inakwisha
Hao hao hao hakuna anayesimama kuzungumzia vibaka na ujambazi

Utashangaa watu waliouawa kwa ujambazi tangu mwaka huu ni wengi.
Hakuna mtu aliyeuawa kwasababu za mikutano ya siasa hata mmoja

Watu waliokufa kwa ajali kuanzia January 2016 ni karibia ya elfu
Hakuna mtu aliyaeuawa kwasababu ya mikutano ya siasa hata mmoja

Tulidhani vipaumbele vingekuwa mambo yanayogusa maisha ya wananchi.

Kinyume chake tunasikia marufuku ya mikutano,mazoezi mitaani n.k.
Mambo yasiyo na madhara hata kwa mtu mmoja

Mikutano ya siasa ni sehemu ya domo tu, watu wanazungumza wanaondoka.
Haijaleta madhara kama ya vibaka na mjambazi

Hakuna mwananchi anayemwoga mwanasiasa kuliko wanavyoogopa vibaka

Hakuna anayejali kwasababu si sehemu ya masilahi ya kisiasa

Wako wapi ? watu wanateswa na vibaka!

Hatumsikii yoyote, wamezikimbia TV walizokuwa wanazitumia kueleza mikakati ya kupambana na mikutano ya siasa tu
 
Panya Road waacha vilio tamasha la singeli

Kwanini katika sherehe kama hizi Polisi wanakosekana ili kuhakikisha ulinzi kwa wahudhuriaji?

Mkuu yale mazoezi ya askari mitaani, pikipiki, maderaya n.k. yalilenga nini ?

Pili, malezi ni suala moja, usimamizi ni suala jingine. Yuko wapi Makonda wa UKUTA? Yuko wapi kamishna wa operesheni maalum za Polisi? Yuko wapi kamanda wa kanda maalumu? Yuko wapi IGP?
Yuko wapi waziri wa mambo ya ndani? Yuko wapi Rais?

Mbona walikuwepo wakati wa UKUTA wakitumia kila resources?

Leo inageukaje suala la malezi?

Mkuu wa mkoa anapopanda miti , watu wakicharangwa mapanga ina picha gani?

Mkuu wa mkoa anaposema wanajipanga, walikuwa wapi siku zote?

Mkuu tatizo si malezi, hayo ni sehemu tu ya jamii.

Tatizo ni viongozi kujishughulisha na mambo trivial na kuacha majukumu yao.

Hakuna mtu aliyekufa katika mikutano ya siasa mwaka huu mzima.

Ni wangapi wamekufa kwa ujambazi? Ni wangapi wamekufa kwa ajali?

Haya yanaeleza kufeli na lazima tukubali kusimama pamoja na kuwaambia, wanafeli na tuna feli kama Taifa

Tuwaambie wazi, mikutano ya jangwani si tatizo, tatizo ni mapanga , visu wanavyopambana navyo wananchi kule mitaani.

Ni akina hofu waliyo nayo akina mama kule mitaani. Hata kutembea na pochi katika nchi wanayolipa kodi sasa ni 'privilege' .

Leo askari wetu yupo Lugalo si kwasababu nyingine bali vibaka wa nchi yetu. Inauma sana. Tunafeli hatukubali

Wanafeli, tunafeli kama Taifa, inasikitisha sana!

Tukubali kuwa tunafeli , tukae pamoja kuangalia kwanini tuna feli. Lakini ukweli kuwa yunafeli hatuwezi kuukwepa!
 
Ujambazi wakutisha Dar



*Yafunga mtaa kwa saa mbili, yapora mamilioni

Na ARODIA PETER-DAR ES SALAAM

NI ujambazi wa kutisha. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na kuibuka na wizi unaofanywa na majambazi katika maeneo mbalimbali nchini.

Hatua hiyo inatokana na majambazi hao kuibuka na mbinu mpya kila kukicha katika matukio mbalimbali ambayo sasa yamekuwa yakishika kasi.

Mbali na mbinu ya kutumia pikipiki, majambazi hayo pia huvamia vibanda vya kutoa huduma za fedha, kuiba magari na hata wakati mwingine kuua.

Katika hali iliyovuta hisia za watu wengi, juzi usiku majambazi yalifunga mtaa kwa saa mbili na kupora fedha kwa watoa huduma ya fedha kwa njia ya simu katika eneo la Tabata jijini Dar es Salaam.

Mbali na maduka, watu wengine waliokuwa nje nao pia waliporwa simu na fedha. Hata hivyo thamani ya fedha na vitu vilivyoporwa havikujulikana mara moja.

Tukio hilo lililoshtua wakazi wengi wa mitaa ya Kimanga na Kisukuru wilayani Ilala, Dar es Salaam, ni la pili kutokea ndani ya kipindi cha mwezi mmoja.

Awali mwezi uliopita, majambazi wenye silaha walimuua kwa risasi askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na baadaye kumpora fedha Sh milioni tano, nje ya geti la nyumbani kwake Mtaa wa Kimanga, saa tano asubuhi.

Tukio la juzi lilitokea katika moja ya maduka yaliyoko pembezoni mwa kituo cha daladala cha Jiandae kilichopo Tabata Kimanga, ambako majambazi wanaokadiriwa kuwa zaidi ya wanne yaliingia dukani na kuwaamuru wafanyakazi kutoa fedha zote za mauzo ya siku, huku wakiwatishia kwa mapanga na bastola.

Mmoja wa wafanyakazi wa kike katika maduka hayo alipoteza fahamu baada ya tukio hilo na alikimbizwa hospitali kwa matibabu.

Licha ya idadi kubwa ya watu katika eneo hilo lenye biashara mbalimbali wakati wa jioni, majambazi hao hawakujali, walifanya uporaji huo na baadaye kutokomea kwa kutumia pikipiki aina ya Boxer.

Mashuhuda wa tukio hilo waliliambia MTANZANIA jana kuwa kwa muda wa dakika tano hakuna gari iliyoruhusiwa kwenda au kutoka Kimanga.

“Majambazi waliwaamuru wenye magari kutokukatiza eneo hilo, huku waenda kwa miguu wakiamriwa kuondoka haraka.

“Katika hali ya kawaida ni vigumu kuamini kama majambazi wanaweza kuvamia na kupora vitu katika maduka matatu kwa mpigo halafu wakatoweka bila kukamatwa,” alisema shuhuda huyo aliyekataa kutajwa jina.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga, Manase Mjema, alipoulizwa kuhusu tukio hilo, alisema majambazi hao yalikuwa yamejiandaa na yalitumia silaha kubwa.

“Awali kabla ya kufyatua risasi yaliwaamuru wafanyakazi wa maduka yanayofanya biashara kupitia miamala ya simu kutoa fedha zote za mauzo, vijana walikuwa ngangari kidogo, hivyo majambazi waliamua kupiga risasi tatu hewani ndipo waliamua kutoa fedha walizokuwa nazo,” alisema.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alikiri kuwapo kwa ulinzi hafifu katika mtaa wake, huku pia akishauri Jeshi la Polisi kuimarisha doria mitaani kwa kuongeza askari wasiokuwa na sare ili wasitambulike kwa urahisi.

“Nikiri kwamba ulinzi wetu wa mtaa wakati wa usiku bado ni mdogo, tunaomba polisi nao waangalie mbinu mbadala za kukabiliana na uhalifu, na hasa ujambazi huu wa kutumia silaha za moto. Eneo la Tabata hivi sasa limekumbwa na matukio mengi ya ujambazi, kwa hiyo lazima mbinu nazo zibadilike,” alisema Mjema ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kimanga (Chadema).

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Lucas Mkondya, alikiri kupokea taarifa za ujambazi na tayari askari wake wameanza uchunguzi ili kuwabaini wahalifu hao.

“Nitoe ombi na nisisitize wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kutokomeza vitendo vyote vya uhalifu. Viongozi wote wa mitaa watupatie taarifa za watu wanaowatilia shaka, nasi tutazifanyia kazi,” alisema Kamanda Mkondya.

Katika siku za hivi karibu kumeibuka matukio ya ujambazi katika maeneo mbalimbali nchini huku wakiibua mbinu mpya za kufanikisha wizi huo.

Kutokana na hali hiyo majambazi hao wamekuwa wakitumia pikipiki kwa ajili ya kutekeleza uvamizi kwenye matukio hayo na hata wakati mwingine kuua watu na kujeruhi.

Katika mfululizo wa matukio ya ujambazi jijini Dar es Salaam, Agosti 23, mwaka huu, askari wanne wa Jeshi la Polisi waliuawa baada ya majambazi kuvamia Tawi la Benki ya CRDB lililopo Mbande, wilayani Temeke.
Majambazi hao wanaokadiriwa kufikia 14, wakati askari hao wakibadilishana lindo, waliibuka ghafla na kuanza kurusha risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia.

Kutokana na foleni katika barabara nyingi za Dar es Salaam pamoja na miundombinu ya makazi yasiyokuwa rasmi, matukio mengi ya ujambazi yanayoripotiwa ni ya kutumia pikipiki, hivyo kuwapa wakati mgumu polisi ambao mara nyingi wanatumia magari ya doria.

Mapema mwaka huu Rais Dk. John Magufuli aliliagiza Jeshi la Polisi kutumia mbinu za kisasa katika kukabiliana na uhalifu na kuifanya nchi kuwa sehemu salama nyakati zote.

Dk Magufuli alionesha kushangazwa na askari wa Jeshi la Polisi kunyang’anywa silaha yake na majambazi na wakati mwingine kuuliwa na majambazi, akihoji uwezo wa majambazi kiasi cha kuwatesa polisi kiasi hicho.

Rais alikuwa akizindua Mpango wa kuboresha usalama wa jamii na mali zao, ambao una dhamira ya kupunguza uhalifu ambapo ameliagiza jeshi hilo kuwahi kushughulikia majambazi kabla ya wenyewe kushughulikiwa na majambazi hayo.

Pamoja na hali hiyo Jeshi la Polisi lilitangaza mikakati mbalimbali ikiwamo ukaguzi maalumu wa bodaboda na kufunga kamera za CCTV katika miji mikuu ili kufuatilia matukio mbalimbali.

Majambazi hao ambao kwa muda sasa wamekuwa wakiibuka na mbinu mpya ikiwamo ya kutumia bodaboda kuvamia benki na wanaotoka benki na kuwapora fedha.

Licha ya polisi kuweka ulinzi maalumu na waendesha bodaboda watakaoonekana kupakia kitu chochote na kukiweka mbele (katika tenki la mafuta) au kiti cha nyuma, ikiwemo kusimamishwa na kupekuliwa lakini bado mbinu hiyo imekuwa ikifeli na watu wakijikuta wakidhurika.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya mara kwa mara ya wananchi kuvamiwa na kuporwa fedha, ikiwa ni muda mfupi baada ya kuzichukua benki huku wafanyakazi wa benki wakidaiwa kuhusika kutoa taarifa za wateja.

Mara zote majambazi hutumia bodaboda kufanikisha uhalifu huo, huku wakiwa na silaha ambazo huzitumia kutishia, kujeruhi na wakati mwingine kuua.

CHANZO: Mtanzania
 
POLISI WANATUMIA NGUVU KUBWA SEHEMU AMBAPO HAKUNA HAJA YA KUTUMIA..MFANO UKIWAONA WANAVYO WAKAMAMATA WANYWA POMBE ASUBUHI ....UTAFIKIRI JAMBAZI ANAVAMIWA...
LAKINI INAPOTOKEA TUKIO LA UJAMBAZI HATA HUWAONI POLISI WAKI RESPOND...

MITAA NA SEHEMU INAYOJULIKANA KWA UHALIFU SANA SANA YA UPORAJI POLISI WANAZIJUA ZOTE!

OVA
 
Mimi ninaushauri kwa ajili ya ufumbuzi wa tatizo. Ninawashauri wananchi wa maeneo husika wapeleke taarifa polisi mapema iwezekanavyo ili vibaka hawa wafutwe mara moja. Kitu cha kuzingatia ni kwamba wasifanye kosa kwa kusema ni vibaka, Bali waseme ni vijana wa ukawa waliosambazwa kufanya uhalifu ili watu walichukie Jeshi la polisi pamoja na serikali. Kwa taarifa kama hii ni lazima wafutwe tu tena defender zitakazotumika zitakuwa sawa kiidadi na wahalifu wenyewe. Kwahiyo kila muhalifu atakuwa na defender yake iliyosheheni askari wa kumshughulikia. Hii ndio njia. Wakifanya kosa waseme ni vibaka basi imekula kwao.
 
Mkuu Nguruvi3 ukipata nafasi pita mtaa huu.
Mkuu yanatokea hakuna anayejisughulisha. Ingalikuwa suala la upinzani tungeona kila aina ya mazoezi na silaha. Hili jambo linasikitisha sana

Tuliambiwa wapo waliokwenda Jordan, picha zikaonekana na misuli ya nguvu

Leo ujambazi umekuwa maisha ya kawaida kana kwamba hakuna ulinzi na usalama

Hawajali, haiwahusu. Wanajali masilahi yao ya kisiasa yanapoguswa! Utawasikia kila siku redioni na katika TV
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Nakubaliana nawe Mkuu pamoja na ukweli wa ulichokiandika kusikitisha na pia kushangaza sana.

Vyombo vya dola ambavyo Watanzania wengi tulidhani kwamba kipaumbele chao cha kwanza ni kulinda usalama na mali za raia wa nchi yetu sasa kipaumbele hicho kimebadilika na sasa kuwa kupambana na vyama vinavyounda UKAWA ili tu kuvinyima haki yao ya kikatiba ya kuandamana na kufanya mikutano popote pale nchini bila kuingiliwa na yeyote yule awe Rais, msajili wa vyama au vyombo vya dola.

Mkuu yanatokea hakuna anayejisughulisha. Ingalikuwa suala la upinzani tungeona kila aina ya mazoezi na silaha. Hili jambo linasikitisha sana

Tuliambiwa wapo waliokwenda Jordan, picha zikaonekana na misuli ya nguvu

Leo ujambazi umekuwa maisha ya kawaida kana kwamba hakuna ulinzi na usalama

Hawajali, haiwahusu. Wanajali masilahi yao ya kisiasa yanapoguswa! Utawasikia kila siku redioni na katika TV
 
Back
Top Bottom