Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,401
- 31,364
Utakumbuka matamko ya mkuu wa mkoa Makonda wakati wa mambo ya kisiasa. Polisi walitanda mitaani wakifanya mazoezi kwa ajili ya wanasiasa wanaofanya kazi zao za siasa. Kazi ya mwanasiasa ni kukutana na watu bila kuwadhuru. Ni hiari isiyomuumiza mtuAhsante sana Mkuu Nguruvi3, nakubaliana nawe katika yote uliyoyaandika kuhusu polisi kujihusisha zaidi na masuala ya kisiasa kuliko kupambana na uhalifu nchini.
Siku zote kuna polisi wa kutosha kupambana na wanasiasa ambao wanafuata katiba ya nchi kufanya kazi zao ikiwemo kufanya mikutano na maandamano sehemu mbali mbali nchini, lakini wakati huo huo kunakuwepo na "upungufu mkubwa" wa polisi inapokuja kwenye kupambana na wahalifu ambao huwaweka wananchi roho juu kwa kutishia usalama wa mali zao na hata uhai wao.
Leo tunasikia anapanda miti! Si kipaumbele chake na hiyo ni kazi yenye mamlaka zake
Wananchi wanaishi kwa hofu ya vibaka, akina mama wakiwa waathirika wakubwa wa unyama unaoendelea mkoa wa Dar es Slaam kupitia vibaka. Kesho utawasikia wanasiasa wakisema 'tulinde Amani na utulivu'
Hivi mtu aliyekatwa na wembe au kisu at bisubisu ambayo imetumika kwa watu wengine ana Amani gani?
Mtu huyo akifikiria magonjwa yanayoweza kupatikana kwa damu za watu ambaye yeye ni sehemu yake ana Amani na utulivu gani?
Amani na utulivu ni pale wanasiasa masilahi yao yanapokuwa salama. Huko mitaani watu wanalala roho juu juu, hawa wana Amani gani
Viongozi hawa wamepataikana kwa njia za kisiasa ndiyo maana utasikia tumejipanga
Hivi Makonda tangu aingie madarakani takribani mwaka bado anajipanga tu. Tatizo la uhalifu linajulikana lakini anaaminisha wananchi anajipanga. Likija la siasa hakuna cha kujipanga ni lake
Tulisema watafeli na Taifa lina feli. Huu ni mwanzo tu wa kufeli
Mkuu wa mkoa anapopanda miti barabarani watu wakichezea bisibisi, viwembe na mapanga ni kufeli kwa kiwango cha juu sana.
Wananchi hawana Amani, tunaambiwa nchi ina amni na utulivu!
Tunafeli kama Taifa kwasababu ya kuwa na viongozi wasiojali. Tunafeli ! tunafeli tunafeli
Wanafeli! mbwembwe na harakati zote sasa Tunafeli sana