Nantahulila
JF-Expert Member
- Sep 20, 2018
- 2,338
- 1,987
Mwanadamu anapigania dini ya Mungu wake.Kwa Nini Mungu mwenye uwezo asiwaadhibu hao wanaokula kinyume na maamrisho yake?Kuhusu watu kuadhibiwa kula hadharani ZANZIBAR hilo naliunga mkono. Imani za watu ziheshimiwe
Unajua nashindwa kuelewa watu wanatokwa na povu kwa suala dogo kama hili kwani haswa wakati taratibu za wenzetu zipo wazi?
ZANZIBAR hakuna aliyelazimishwa kufunga ispokua utaratibu wa kule unakataza mtu kula hadharani hasa kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan
Na mnajua ZANZIBAR asilimia 99.999 ni waislam, na lazima tamaduni za watu ziheshimiwe kama unataka kula mchana we kula tu lakini sio vizuri kula hadharani maana yake utakua unafundisha nini jamii?
Kwa huku bara hata mtu ukila ni sawa tu maana humu tumechanganyikana watu wa dini tofauti ZANZIBAR wengi ni waislam na nashangaa watu mnatokwa na mapovu kwenye hili
Ni ushetani mkubwa kutokua na haya na kwenda kula public mwezi wa ramadhan katika jamii ambayo ni waislam watupu kwanini usitafute mahala kwako au ndani kwako ukala?Kwanini ule hadharani?
Kuna mtu kahoji kwahiyo mbona sisi kwaresma huwa hatuwagusi waislam ambao unakuta hawajafunga?Swali ni mkristo yupi anafungaga kwaresma?Mimi nimekulia sehemu zenye Christian majority sijawahi kuona mtu kafunga hata kwa bahati mbaya....Kwahyo msipende kucompare dini za watu, kama mnaridhika imani zenu kuchezewachezewa kwasababu zishakua "imani cheap" ni nyie ila sio uislam.
Uislam sio dini ya masihara na mchezomchezo ndo maana ndo dini inakua kwa kasi kidunia na ipo tokea karne pamoja na kupigwa vita vya kimwili na kiroho.Watu washaacha dini yao ishaharibiwa huko na kuchezewa vya kutosha sasa wanataka uislam iwe dini ya hivyo hilo No!!
Mnaotokwa na mapovu kuhusu sakata la kula kumbukeni ZANZIBAR asilimia 99 ni waislam kwahyo tamaduni za walowengi ziheshimiwe..
Kama ulikua na mikiu yako ya kula minguruwe yako ungeenda kujifungia ndani ule kwa raha zako!! Msipende kuwaponza waliofunga!!Mimi naunga mkono wachapwe tu.kila mtu aheshimu imani ya mwenzake kama ambavyo yake huheshimiwa.
Binafsi yangu nimeishi kwenye jamii nyingine ambazo ni za imani tofauti na mimi au tamaduni tofauti ila nilifanikiwa pakubwa kuishi nao kwasababu niliishi kwa kutii taratibu zao na mambo yalienda vizuri tu.