FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 93,086
- 109,462
Zanzibar ni nchi huru yenye, tamaduni, mila na desturi zake. Pia sheria kanuni na katiba yake, wewe kama nani uwaingilie?Zanzibar sio Nchi inayoongozwa na Sheria za Kiislamu, Zanzibar ni nchi inayoongozwa na katiba huru.
Inakuwaje unamkamata mtu kwa sababu ya kutokufunga Ramadhan, ni wapi kwenye katiba wamesema kwamba usipofunga inapaswa kuswekwa Ndani. Mkianza kutuletea sheria za kiarabu Kwenye ardhi za Tanzania basi kuna uwezekano mkaleta pia mambo ya Udini na vikundi vyenye itikadi kali kama ilivyo kwenye majimbo ya Nchi ya Nigeria yanayoongozwa na sheria kali za kiislamu. Na maeneo hayo hayo ndio makazi ya vikundi kama Boko Boys au Boko Haram.
Uwezi kumlazimisha mtu kufunga kwa sababu hiyo ni kati yake yeye na MUNGU wake, ukimpazimisha mtu kufunga kama hajasadiki au kuridhia ni sawa na kutwanga maji tu kwa sababu hatopata swawabu yoyote kwa mujibu wa imani ya kiislamu atafunga kwa kuwaridhisha watu tu. Mwili ni wake, mbona hakikosa chakula hamuwapelekei kuwalazimisha wale kama jinsi mnavyowalazimisha kushinda njaa.
Badala ya kushurutisha watu kushinda njaa kwa lazima, wafundisheni misingi ya Dini ya kiislamu na wafundisheni umuhimu wa mfungo wa ramadhani hili mtu atambue umuhimu wa kufunga na afunge kiroho safi.
Sheria hiyo ya kamata kamata watu wasiofunga inakiuka haki za mtanzania na vifungu vya katiba.
Pia Soma:
- Watu 12 wakamatwa kwa kula hadharani mchana Zanzibar