gammaparticles
JF-Expert Member
- Jan 9, 2024
- 1,005
- 1,620
Kama unavyopenda kuwanaga wenzako, na wewe hapa umpuyanga na "logical non sequitur"Waislamu wakienda nchi zenye imani zinazopingana na imani za Kiislamu walazimishwe kufuata hizo imani kwa kuheshinu imani za watu wa nchi hizo?
Au hii habari ya kuheshimu imani za watu wa nchi unayokwenda ni special ukienda nchi za Waislamu tu?
Wakristo wa Italy wakianza kuwachapa bakora Waislamu walio Italy kwa sababu Waislamu wanafunga Ramadhan, Wa Italiano hawafungi, wanawataka Waislamu waheshimu imani za Waitaliano za kutofunga Ramadhani, utakubali Waislamu wapigwe bakora na kulazimishwa kula mchana mwezi wa Ramadhani kwa kuheshinu dini za wakazi wa Italy?
Zanzibar hakuna mtu analazimishwa kufuata imani ya kiislamu na hivyo hivyo ukiwa mfano Dubai, wazungu wanakuja Zanzibar na wanakwenda Dubai, na wanaheshimu kipindi cha mfungo kutokula hovyo hadharani, na pia kuna mahoteli wanaruhusiwa kwenda kula, na sio kwamba kula hairuhusiwi.
Sasa hapa Zanzibar wapo wakristo tokea enzi na pia wazungu wanakuja kutalii tokea zamani, na wanaheshimu kila wakati wa mfungo kuna sehemu maalumu yakwenda kula na sio kula hadharani.
Ni kipindi cha hivi karibuni Zanzibar kuwa na ongezeko la watu wanaotoka Bara, na wanajiona wanaweza kufanya wanavyotaka bila kuheshimu huu utaratibu.
Ni hivi kama hutaki kuufuta hivyo , ondoka au usije Zanzibar haukulazimishwa, ikiwa wakristo wazawa wa Zanzibar tunaishi nao vizuri tu na pia watalii wanafuata utaratibu,