Polisi wa FFU auliwa na Wananchi wenye hasira (Tegeta)

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Polisi mmoja wa kikosi cha FFU ameuliwa wakati wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya leo na raia wenye hasira maeneo ya Tegeta Namanga. Pamoja na skari, kuna raia wawili pila waliouliwa na askari hao wa FFU huku wengine wengi wakiwa wameumizwa vibaya. Hii ilitokea kwenye purukushani iliyoanzhishwa na mmiliki wa kituo cha mafuta aliyeanza kuvunja makazi ya wananchi hao.

Yawezekana wengi wamepoteza maisha yao, ila kwa macho yangu nimemuona Askari mmoja kauliwa na Wananchi wawili ila walioumia ni wengi sana. Hali ilikuwa ni mbaya sijawahi kuona. Nimeona ile kwenye TV. Nilijua tu vitu kama vile vinatokea Afghanistan, Syria na Iraq siyo Tanzania. Mbaya zaidi rais mwenye kapita na kuacha mapambano yakiendelea

Mapambano kati ya polisi na raia yameendelea kwa muda mrefu hata baada ya rais kupita, ambako pia gari la rais na msafara mzima lilirushiwa mawe.....Inabidi polisi waseme ukweli kuhusiana na hili jambo.. hali bado tete kwani wananchi wana hasira na serikali kuruhusu mwekezaji huyu kujichukulia sheria mikononi mwake ya kuwahamisha na kuvunja makazi yao

Chanzo, nilikuwepo eneo la tukio
 
mtoa habari kama una contact za huko tupe habari mambo yakoje saa hizi, nimeona magari ya FFU mengi yakitoka kambini sikujua yanaelekea wapi
 
Hii nchi sasa,hakyamungu watanzania tumekuwa wakimbizi nchini kwetu.ni chama hiki hiki na serikali yake juzi walitamba kutawala milele!yangu macho
 
Haya ndiyo matunda ya kuwa na Kiongozi na Serikali DHAIFU ambayo hata siku moja haiwezi kutetea maslahi ya Watanzania bali ya wale mafisadi wanaojifanya ni "wawekezaji". Tanzania yetu itaendelea kuwa nchi ya amani milele.
 
umedhibitisha vipi idadi hiyo ya vifo? ??????

Nilikuwa natokea boko kuelekea mjini, njiani mume wangu kanipigia simu niwe mwangalifu kwani alisikia tegeta kuna vurugu. Aisee, niligeuza gari nikatembea miguu kuja kwenye eneo la tukio, yaani ilikuwa kama vile Afghanistan.

Nililazimika kugeuza gari na kurudi nyumbani. Polisi walikuwa wakirusha risasi ambazo sijui zilikuwa za moto au za mipira ila pia niliona moshi mwingi unaofanana na ule wa mabomu ya machozi. Polisi aliyeuliwa alivamiwa na mawe.

Pia kuna baadhi yao kadhaa waliojeruhiwa na gari lao kupigwa sana mawe. Kusema kweli hali ilikuwa ni mbaya sana..........Inabidi mkuu wa kaya aingilie swala. Waliowawa nimewaona na macho yangu ila cha kushangaza kamanda wa polisi analificha hili pale alipoongea redioni.
 
Rip wananchi waliofariki na hao maaskari wakafie mbali maana wanatumwa na kujitoa ufahamu!
 
kama ni kweli hii habari na ile ya zanzibar, basi ni jambo jema. kuanzia hapa tunaweza kuanzisha maandamano kila kona ya nchi hii ili polisi wachanganyikiwe. mbeya, mwanza iringa na sehemu zote tuhamasishishane ili tuwaondoe hawa wadhalimu
 
Kweli JK ni dhaif 100%. Jaani hili jambo kalishuhudia na bado limeua? Kwani huyo BigBon ni nani Jamani?
 
Kama hali ndiyo hivyo itabidi waumini wa dini zote tukeshe kwenye maombi, maana kila kukicha ni dhuluma tunazofanyiwa wananchi wanyonge na vyombo vya dola vinavyoendeshwa kwa kodi ya wananchi, jambo ambalo linaweza kujenga chuki kubwa kati ya watawala na watawaliwa! Ee mwenyezi Mungu ibariki nchi yetu na uingilie kati dhuluma hii kubwa inayofanywa na hawa watawala wetu waliolewa madaraka!
 
This is episode two isnt it? ... Mchana episode one ... Si President walimnaniii maeneo hayo hayo ... ?
 
ffu mmoja kauwa na wananchi.
Wananci wawili wamepigwa na live ammunition/bullet na kufa papohapo.
 
Kwa hivo Mwarabu Mmiliki wa vituo vya mafuta ya OILCOM inaonekana anayo HAKIARDHI zaidi ndani ya mipaka hii kuliko wananchi wazawa???????????

Wafiwa na majeruhi kwa mpigo poleni sana; ndio kama hivo taifa limefikishwa hapa na genge la MAFISADI ndani ya CCM.

Taifa linalia kila mahali taifa linavuja damu na kitu HAKI imekua ni msamiati mkubwa ajabu!!!!!!


Polisi mmoja wa kikosi cha FFU ameuliwa wakati wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya leo na raia wenye hasira maeneo ya Tegeta Namanga.

Pamoja na skari, kuna raia wawili pila waliouliwa na askari hao wa FFU huku wengine wengi wakiwa wameumizwa vibaya. Hii ilitokea kwenye purukushani iliyoanzhishwa na mmiliki wa kituo cha mafuta aliyeanza kuvunja makazi ya wananchi hao.

Mapambano kati ya polisi na raia yameendelea kwa muda mrefu hata baada ya rais kupita, ambako pia gari la rais na msafara mzima lilirushiwa mawe.....Inabidi polisi waseme ukweli kuhusiana na hili jambo.. hali bado tete kwani wananchi wana hasira na serikali kuruhusu mwekezaji huyu kujichukulia sheria mikononi mwake ya kuwahamisha na kuvunja makazi yao

Chanzo, nilikuwepo eneo la tukio
 
Back
Top Bottom